Mzungu ana nyota kali ya mvuto? Kwanini watanzania wengi huwanyenyekea na hujipendekeza kwao?

Mzungu ana nyota kali ya mvuto? Kwanini watanzania wengi huwanyenyekea na hujipendekeza kwao?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Si mara moja wala mara mbili nimekuwa nikiiona hii hali kwenye sehemu tofauti.

Unakuta mzungu akienda ofisi ya serikali anashughulikiwa ki V.I.P unakuta swala lake linahughulikiwa kwaumakini wa hali ya juu sana.

Akipita mtaani watu anaopishana nao wanampa sana salamu na hata wale wa mbali wanamsalimia. mzungu mambo, mzungu nipe tano, mzungu uko poa.

Kukiwa na foleni, unakuta mzungu anaweza kupishwa kwamba ana haraka na watu wakakubali kiroho safi, huwa wanatembea njiani na mzungu, n.k.

Mtu akiwa na rafiki wa kizungu inakuwa ni kama kacheo flani hivi kwamba anatembelewa na mzungu nyumbani kwake.

Mzungu akiendesha basi hata akikimbiza, abiria watalala fofofo, wanasema ni mtaalam wa magari.
 
hahahaha kuna wazungu wamechakaa hadi unawaonea huruma

wengi wapo bukoba,mtwara huko
 
Unazungumzia mdhunguuu dejani wa KOLO WIZARDS fc au .....
 
Kuna kaukweli lakini kachungu kukubali, ila tulioishi ughaibuni na wazungu kwa miaka mingi hii haituhusu
 
Kwa waarabu huwa ni wachumba tu hao wazungu, sema huku AFILIKA wengi wao hawajiamini, ni watu ambao yani akimuona mzungu anapigwa butwaa na kujihisi yeye si lolote.

Bhujiku ng'waka
 
Kwa waarabu huwa ni wachumba tu hao wazungu, sema huku AFILIKA wengi wao hawajiamini, ni watu ambao yani akimuona mzungu anapigwa butwaa na kujihisi yeye si lolote.

Bhujiku ng'waka
Iwe ni mchina, mwarabu, mhindi, n.k. Mzungu ana title yake aisee.... yani mzungu akienda china, india, uarabuni, n.k. huwa jamii inamchukulia ki v.i.p sema huku tumezidi sana .... kacheki documentaries uone hii ishu..
 
Ulichokiongea kinaukweli
Hawa watu kwakiasi Fulani wanachukuliwa VIP kwa sababu..
Wanajielewa Sana afrika Ni kama nyumbu tu.
Wazungu wanajali sana muda hawana muda wa umbea umbea Kama sisi

Natamani waingereza waje watutawale Tena.

Waafrika tuna roho mbaya Sana Tena Sana. Sio wananchi Wala viongozi.

Wizi, Tamaa, uchawi, chuki, ubinafisi, lawama, tunajificha kwenye kichaka Cha dini kumbe ndi bure kabisa ( hapa Mungu atatuhukumu kwa unafiki )
 
Wanathaminika kutokana na waliyoyafanya katika ulimwengu huu,

, na wala hatujipendekezi bure " we angalia kati ya mzungu ama muhindi ama mwarabu jumlisha mwafrika ni yupi akifungua kampuni ama kiwanda na
Kuajiri watu " watu watafaidika wapi kama sio kwa mzungu ....

angalia hata migodi aliyowekeza nchini watu wanafaidika moja kwa moja , vp kwa mchina , mwarabu ,muhindi , mtu mweusi n.k... wapeni heshima yao bana , acheni roho za kwanini"

alokutangulia amekutangulia tu huitaji kumchukia ili nawe umfikie bali ujenge urafiki akuoneshe njia na sioni Kama ni kujipendekeza.
 
Back
Top Bottom