Mzunguko wa hewa huwa sio mzuri ndani ya Bus zenye viyoyozi (AC), bora kufungua vioo tu

Sijawahi mkuu? Jibu swali uliloulizwa.
Ndege zina mfumo maalum wa kuchakata hewa na kuingiza oxygen ndani ya ndege na pia kutoa hewa chafu ndani ya ndege, unaitwa Environmental Control System(ECS)
 
Hakuna mikweche barabara ya Dar-Arusha.
hatari sana mkuu, kwahiyo hapa ni mfumo mbovu wa hizi a/c au ni nini hasa


kwa sababu naamini kitendo cha kuwekwa a/c maana yake inabidi itumike kwa kufunga madirisha
 
Upo sawa.
Binafsi pia sipendelei AC hata nikiwa kwenye gari binafsi. Huwa tunabishana na mama watoto tukitumia gari moja, ni mpenzi wa kufunga vioo AC iwe on wakati mimi napenda upepo.
Unakuta mtu mwingine kwenye gari private tena tinted na ni usiku, kafunga vioo vyote anakula AC yaani ajari nje nje.
 
Reactions: Tsh
Au hata ukute Wachina safari za kilometa zaidi ya 800 kwa bus lazima walale njiani siku moja au mbili, kama mtu ana haraka anapanda treni au ndege.
 
Usiombe watu wakishakula masaa mawili baadae.
Ile hewa inakuwaga nzito balaa.
 
 
Kwa hiyo kwenye mabus hewa chafu hua haitolewi nje?,
Inashangaza sana. Yaani hajui kuwa AC inatoa hewa nje na kuingiza fresh air kutoka nje. BTW kuna options mbili, ya kuzungusha hewa ya ndani au kuingiza hewa ya nje kwemye system ya upoozaji.
 
Kwa hiyo kwenye mabus hewa chafu hua haitolewi nje?,
Haitoki. AC haina uwezo huo. Huwa tunavuta ile ile. Unless basi liwe equiped na ECS.
ECS = AC + pressure + filtration + humidity + oxygen control wakati AC= cooling/heating + air circulation.
 
Inashangaza sana. Yaani hajui kuwa AC inatoa hewa nje na kuingiza fresh air kutoka nje. BTW kuna options mbili, ya kuzungusha hewa ya ndani au kuingiza hewa ya nje kwemye system ya upoozaji.
Hapana mkuu. AC haitoi hewa nje. Inazungusha hewa ile ile bana. Embu tugoogle kujiridhisha.
 
Ndege zina mfumo maalum wa kuchakata hewa na kuingiza oxygen ndani ya ndege na pia kutoa hewa chafu ndani ya ndege, unaitwa Environmental Control System(ECS)
Mkuu kwenye ndege kuna mfumo huo kwasababu over 10,000ft hakuna oxygen na ndege iko pressurized. Gari iko ardhini kuna oxygen ya kutosha.
Usichokijuq ni kuwa air conditioning system ya kwenye gari ina circulate hewa. Inatoa na kuingiza. Sio kwamba inatumia hewa hio hio ya kwemye cabin. Actually kuna option ya kuzungusha hewa ya cabin au kuingiza fresh air kutoka nje. Waliotengezeza AC kwemye gari hawawezi kuwa wajinga hivyo.
 
Shubamiit. Mara kadhaa nimepanda hizi Yutong unakuta ni mpya tu ila nateseka kweli, najiuliza mbona huwa sina tatizo nikiwa nasafiri imekuaje? Sasa umenipa jibu.
Mi mwenyewe huwa sina tatizo la kujiskia vibaya nikisafiri ila mara ya mwisho nilipanda bus safari fupi tu ya Babati-Arusha ila hali ilinishinda nikafunga vent nikawa mara kwa mara nafungua kioo na kufunga ndo nikatoboa, wahudumu wa gari hawataki abiria wafungue vioo
 
Hilo basi la wapi linalosafiri kwa saa nane mkiwa mmejifungia ndani! Mabasi yote huwa yanasimama kila baada ya muda mfupi kwa ajili ya abiria kupanda, kushuka, kula na kujisaidia, hakuna basi litatoka Dar mpaka Dodoma bila kutimiza niliyoyataja, wewe ni mmoja wa wale wasio safiri kwa kukosa ndugu au shughuri mikoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…