Tofauti inakuja kwenye aina ya gari. Unaona hizi Carina za zamani, Hiace na magari kama hayo zinatoa hadi harufu ya combustion ndani. Unasafiri unasikia harufu ya mafuta na moshi.
Ukija kwa gari za kisasa kabisa hasa standards za Ulaya unakuta mifumo ya kusafisha hewa kama HEPA kutoa vumbi, pollen za maua, hewa chafu ya exhaust uko barabarani.
Sasa hawa Wachina kina Yutong unakuta basi lina watu 55 kuna Wamasai humo wamejipaka mafuta ya ng’ombe, Wasukuma watakula mahindi ya kuchoma na karanga na Waha wamebeba mifuko ya mikate. Hiyo harufu yote mkianza nayo safari, hadi mmalize nayo. Ikitokea mtoto kaharisha mnaanza safari, mnamaliza safari na hiyo harufu.
Sasa mtu anayelinganisha bus na ndege yenye pressurized cabin pamoja na mifumo ya kisasa kabisa ya kubadilisha hewa anatakiwa kutandikwa viboko. Unajua hata kama mtu ni maskini, inabidi uwe na class na common sense ya kutambua luxuries na comforts.