Mzunguko wa hewa huwa sio mzuri ndani ya Bus zenye viyoyozi (AC), bora kufungua vioo tu

Mzunguko wa hewa huwa sio mzuri ndani ya Bus zenye viyoyozi (AC), bora kufungua vioo tu

Wewe hujaelewa ila sasa naona kama hutotaka kuelewa.

Basi ukifunga vioo hewa inayoingia ili ichakatwe na AC ni chache ukilinganisha na idadi ya watu humo ndani na AC haina uwezo wa kuongeza oxygen, ndo maana tunasema inashauriwa kufungua madirisha nyakati fulani iwapo basi limetembea umbali mrefu bila kusimama. Nyumba ina space kubwa pia ina vents nyingi, AC inapata hewa mpya ya kuichakata wakati wote. Kama huamini, jaribu kutafiti iwapo AC ikifungwa sehemu kuna 0 oxygen kama itafanya kazi.
Nani alikwambia AC ya kwenye basi haiendani na capacity? Hebu tuongee kitaalamu.

Kwa hiyo unataka kusema haya mabasi yote yenye AC yanabeba idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wa AC zake? 😅
 
Kabla ya kuunga mkono fikiri kwanza, Tanzania hakuna basi linalosafiri kwa saa nane likiwa limefungwa madirisha na milango! Mabasi yote husimama kila baada ya muda kwa ajili ya kushusha na kupanda na kujisaidia abiria, milango ni lazima ifunguliwe.
Kitaratibu tu, Hewa ya Artificial kwenye ma-bus huku Africa haitakiwi tu, kwa sababu hatujafika kiwango cha kukosa hewa ya oxygen ya asili.

Kusimama kwa ma-bus ni kwenye route moja haiwezi kuzidi mara tatu au nne napo ni dakika kumi tu, so ukizidisha hapo Milango inakuwa wazi ndani ya dakika 40 kwa safari ya masaa 12-14.

Madhara ya hewa artificial hasa kwa wenye matatizo ya moyo, shida ya upumuaji, na hypotension au hypertension( watu hawa huhitaji hewa safi na asili ya oxygen na siyo ya kutengeneza). Kwa hiyo ukifunga vioo mda mwingi watu wa Aina hii hukosa upumuaji mzuri.

Hopefully umenielewa. 🤝
 
Ukikwea mwewe pia usisahau kumwambia mhudumu akufungulie kioo ila uapte hewa safi ya angani
 
AC inazungusha hewa iliyopo ndani iliyoingia kupitia vents au tube au mfumo wowote kisha inaichakata. Tukijazana sehemu fulani kisha AC ikafungwa ila oxygen haitoshi, bado tutakuwa na tatizo la oxygen pamoja na uwepo wa AC.
Okay
 
Wewe mchina pori hakuna mtu anaweza kukaa kwenye kiti cha ofisi masaa mawili mfululizo hajaenda chooni, kunywa chai, kula, kuvuta sigara n.k hapo bado hujazingatia nyumba haziwi airtight kama bus za Wachina wako zinapofungwa vioo na milango.
Halafu shida yangu mimi sio AC bali ni kulazmisha abiria wote 50 kufunga madirisha yote kwa masaa kadhaa ili wategeme vi AC uchwara.
Wewe ndio abiria uchwara, hakuna basi lenye AC uchwara kama haina matatizo yoyote ya kiufundi kwenye mfumo wa AC na kiwango cha ubaridi ni sahihi.

Kila basi lenye AC wamezingatia capacity na uwezo wa AC hakuna chombo cha moto kinaingia kwenye soko la dunia bila kufanyiwa testing

Ukiona mabasi yenye AC hauyawezi panda gonga nyundo vioo ninafunguliwa mwanzo wa safari hadi mwisho mixer vumbi la nje
 
Nani alikwambia AC ya kwenye basi haiendani na capacity? Hebu tuongee kitaalamu.

Kwa hiyo unataka kusema haya mabasi yote yenye AC yanabeba idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wa AC zake? 😅
Bus za Wachina wako zina mfumo AC na sio HVAC so hoja zako hata hazina mashiko.
 
Umetumia AI ila ime "prompt" isivyo, nimetumia AI pia nikiilezea itumie taarifa za kisayansi na haya ndiyo majibu yake kwa kirefu.

Hii ni hoja ya kiufundi na kimsingi ya kisayansi kuhusu mifumo ya kiyoyozi (AC) kwenye mabasi ya abiria:

1. Mfumo wa Uzungushaji Hewa (Air Recirculation vs Fresh Air Intake)​

  • Mifumo mingi ya AC ya mabasi ya kisasaina modes mbili:
    1. Recirculation mode – inazungusha tena hewa ile ile ya ndani ya basi. Hii husaidia baridi kufanikishwa haraka na inapunguza matumizi ya mafuta kwa sababu mfumo haulazimiki kupooza hewa moto kutoka nje.
    2. Fresh air intake mode – huchukua hewa safi kutoka nje, kui-filter, kisha kuichanganya na hewa ya ndani.
  • Kihandisi, mabasi ya masafa marefu huwa na mchanganyiko wa hewa safi na recirculated air (kwa mfano, 20–30% fresh air + 70–80% recirculation). Hii inalenga kudumisha kiwango cha oksijeni na kupunguza accumulation ya kabondioksaidi (CO₂).

2. Hatari ya Kushuka kwa Oksijeni Ndani ya Basi​

  • Kisayansi: Binadamu anapumua, hewa ya oksijeni (O₂) hupungua na kabondioksaidi (CO₂) huongezeka.
  • Ikiwa basi litakuwa limefungwa kabisa na AC ikawa kwenye full recirculation kwa muda mrefu (bila fresh air intake), kiwango cha O₂ kinaweza kushuka taratibu huku CO₂ ikipanda.
  • Dalili za viwango vya juu vya CO₂ (>1,000 ppm) ni uchovu, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, na kupoteza umakini. Kwa viwango vya juu zaidi, inaweza kuleta madhara makubwa kiafya.
  • Hata hivyo, mifumo ya mabasi ya abiria mara nyingi huundwa kuhakikisha kuna kiwango fulani cha hewa mpya kinachoingia, ili kuzuia tatizo hili.

3. Ushauri Kuhusu Matumizi ya AC Katika Mabasi ya Masafa Marefu​

  • Kitaalamu inashauriwa:
    • AC iwe inafanya kazi muda wote wa safari ili kudumisha joto na unyevunyevu salama kwa abiria.
    • Kwenye masafa marefu, mfumo uwe ume-set kwenye mixed mode (fresh air + recirculation). Hii inahakikisha kuna mzunguko endelevu wa hewa safi kuzuia upungufu wa oksijeni na kuondoa gesi chafu.
    • Kuepuka full recirculation kwa masafa marefu (zaidi ya dakika 30–60 mfululizo) bila kuingiza fresh air.
    • Wakati wa mapumziko (mfano basi likisimama kituo), madirisha au milango inaweza kufunguliwa kwa muda mfupi ili kuongeza hewa safi zaidi.

4. Hitimisho​

  • AC ya basi haisababishi hewa kukosekana endapo imewekwa kwa mpangilio sahihi, kwa sababu inaingiza kiasi cha hewa mpya.
  • Hatari ipo tu endapo basi litakuwa kwenye 100% recirculation mode kwa muda mrefu bila fresh air intake.
  • Kwa usalama wa kiafya na faraja ya abiria, inashauriwa AC iendelee kuwashwa safari nzima, lakini ikiwa katika mpangilio wa kuchanganya hewa ya ndani na hewa mpya ya nje.
Mbona imesema kitu hicho hicho ila kwa lugha ya kiswahili? Inaonyesha wazi kabisa AC inazungusha hewa haiongezi hewa ila mpangilio wa hewa ya ndani na hewa mpya ya nje ukiwa vizuri hakuna tatizo.
 
Katika maendeleo ya usafiri ambayo sijaona umuhimu wake ni bus zenye vyoo ndani na AC, nikipinda hizi bus hasa safari za mchana huwa nahisi hewa nzito sana ndani ya gari. Sijui kama kisayansi ni sahihi au inashauriwa kusafiri watu 50 masaa nane ndani ya Bus ambalo mmesongamana mkiwa mmefunga vioo eti mnategemea AC. Mimi huwa naona bora kufungua tu vioo kupata hewa natural ila tatizo makonda huwa wanalazimisha kufunga vioo vyote.

Inawezekana sababu nyingine ya watu kuchoka sana kwenye hizi safari za bus kama walikuwa wanalima mashamba ni pamoja na mzunguko mbaya wa hewa kwenye hizi bus.
Inazuia watu kupenya madirishani kwa sababu hayo mabasi hayatumii madilisha yenye kufunguka pia yanakuwa na low noise kwa sababu madirisha yake yame banwa vilivyo yasipige kelele kutokana na mitetemo ya gari
 
Nani alikwambia AC ya kwenye basi haiendani na capacity? Hebu tuongee kitaalamu.

Kwa hiyo unataka kusema haya mabasi yote yenye AC yanabeba idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wa AC zake? 😅
Tunatofautiana sehemu ndogo sana. Kwanza tukubaliane kama AC ina tengeneza oxygen au inazungusha oxygen iliyopo? Either oxygen iwe imepita kutumia vents au space yoyote. Tuwekane sawa hapa kwanza ndo tuendelee.
 
Bus za Wachina wako zina mfumo AC na sio HVAC so hoja zako hata hazina mashiko.
Screenshot_20250824-104339_Chrome.jpg


Kati ya mimi na wewe nani hoja zake hazina mashiko bwana Yoda ?
 
Katika maendeleo ya usafiri ambayo sijaona umuhimu wake ni bus zenye vyoo ndani na AC, nikipinda hizi bus hasa safari za mchana huwa nahisi hewa nzito sana ndani ya gari. Sijui kama kisayansi ni sahihi au inashauriwa kusafiri watu 50 masaa nane ndani ya Bus ambalo mmesongamana mkiwa mmefunga vioo eti mnategemea AC. Mimi huwa naona bora kufungua tu vioo kupata hewa natural ila tatizo makonda huwa wanalazimisha kufunga vioo vyote.

Inawezekana sababu nyingine ya watu kuchoka sana kwenye hizi safari za bus kama walikuwa wanalima mashamba ni pamoja na mzunguko mbaya wa hewa kwenye hizi bus.
Uko sahihi binafsi kusafir kwenye bus lenye Ac huwa najihisi kufakufa, hata kwenye boti hizi za Zanzibar -Dar huwa sikai mule ndani kabisa huwa nashangaa watu wanakaaje mule ndani yaan dk 2 nyingi nikahisi ile harufu naweza tapika sana
 
View attachment 3451036

Kati ya mimi na wewe nani hoja zake hazina mashiko bwana Yoda ?
Hoja zako hazina mashiko, watu zaidi ya kumi kwenye uzi wamethibitisha bus zikifungwa vioo na AC uchwara kufunguliwa hewa huwa inakuwa nzito sana na wengine hata mimi huumwa vichwa, mchina ni tapeli na bus zake.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Tunatofautiana sehemu ndogo sana. Kwanza tukubaliane kama AC ina tengeneza oxygen au inazungusha oxygen iliyopo? Either oxygen iwe imepita kutumia vents au space yoyote. Tuwekane sawa hapa kwanza ndo tuendelee.
Labda hoja yako ni nini hasa kwenye huu uzi?

Maana tumetoka kwenye uhusiano kati ya AC na capacity ya bus, AC na afya za watumiaji na sasa tunaingia kwenye how does AC work? 😅

Kwa hiyo tuhamie kwenye AC hufanyaje kazi sawa tu, tuanze na hoja zako sasa
 
Achana na swala la hewa, yupo mwamba frani alikaa siti ya dirishani anagoma kufungua kioo hrf anakula mayai asee alichokifanya ni aibu sijui alivimbiwa? Maana alijijaza tope ghafla ikabid kondakta amaindi Ile mbaya, sasa ndani ya gari harufu ikaenea na Kuna joto balaaaa aseee ilikuwa adhabu Sanaa abiria ni matusi tuu, yaan nahis mwamba alivuliwa ubingwa ujue mtu kutoa tope ghafla sio mchezo inamaana mifereji ipo losses.
 
Hoja zako hazina mashiko, watu zaidi ya kumi kwenye uzi wamethibitisha bus zikifungwa vioo na AC uchwara kufunguliwa hewa huwa inakuwa nzito sana na wengine hata mimi huumwa vichwa, mchina ni tapeli na bus zake.
Kumbe ni vita vya utetezi wa mchina? Aisee Xi Jinping binafsi sijamshambulia mchina, nimesema tu kuna nyakati Yutong hewa ni ndogo ukifunga madirisha halafu basi limejaa.
 
Hoja zako hazina mashiko, watu zaidi ya kumi kwenye uzi wamethibitisha bus zikifungwa vioo na AC uchwara kufunguliwa hewa huwa inakuwa nzito sana na wengine hata mimi huumwa vichwa, mchina ni tapeli na bus zake.
Kwa hiyo kwenye basi za Kichina kutokuwa na HVAC tumekubaliana kuwa ulikuwa unataka kutudanganya tuliweke hili sawa kwanza ili twende mbele
 
Labda hoja yako ni nini hasa kwenye huu uzi?

Maana tumetoka kwenye relationship kati ya AC na bus capacity, AC na afya za watumiaji na sasa tunaingia kwenye how does AC work? 😅

Kwa hiyo tuhamie kwenye jinsi AC hufanya kazi sawa tu, tuanze na hoja zako sasa
Tukikubaliana kwamba AC haina uwezo wa kuongeza oxygen ila inazungusha oxygen iliyopo kupitia vents na open space naamini tutafikia muafaka na kuelewana tunapopishana. Sasa je, AC ina uwezo wa kuongeza oxygen?
 
Labda hoja yako ni nini hasa kwenye huu uzi?

Maana tumetoka kwenye relationship kati ya AC na bus capacity, AC na afya za watumiaji na sasa tunaingia kwenye how does AC work? 😅

Kwa hiyo tuhamie kwenye jinsi AC hufanya kazi sawa tu, tuanze na hoja zako sasa
Hoja ya huu uzi ni hewa haitoshi au inakuwa nzito sana kwa abiria vioo vyote vya kwenye bus vikifungwa ili watu 50 wategemee AC ya bus. Watu zaidi ya 10 wamethibitisha uzoefu huo na hadi wengine hadi huwa wanagombana na makonda au abiria wenzao wanapofungua madirisha wapate hewa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom