Na hizi ndio NDOA ZENU: Mwamba kashaangukiwa na chuma kizito

Na hizi ndio NDOA ZENU: Mwamba kashaangukiwa na chuma kizito

Kuoa ni njema kama utapata mwanamke, mwema mwenye busara upendo na uvimilivu..... Kuolewa ni kuzuri kama ukipata mwanaume mwenye upendo, utimamu na mwenye kuijua thamani ya mwanamke......Kuoa au Kuolewa hua ni bahati njema ikidondokea kwa watu wema..... Lkn ikidondokea kwa watu majeuri hakuna ndoa hapo..... Kweny swala la ndoa kuvunjika na kuvurugika... Huenda huyo rafik ako pia alikua chanzo cha ndoa yake kuharibika...... Haya mambo ni kuomba tu Mungu.... Tusiwashauri vijana wenzetu wasiingie kweny ndoa tuwahimize upendo, uvimilivu na hekima.... Na tuwape mifano ya ndoa ambazo zimedumu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Was waiting for this comment...
 
Sikia hii habari

INTRO
Nyie mabaharia kwani u-single unawashinda nini? Hivi mnajua kuoa ni kutafuta matatizo. Kuna baharia mwenzetu yashamkuta huku.

FLASH BACK
Nilianza kumjua 2019 baada ya kuhamia pale ofisini. Alikuja akiwa na demu (mchumba) kwa kipindi hicho walikua na miaka mi3 wapo pamoja.

2020 akaleta kadi za harusi/michango anataka kumuoa. Kwenye mahojiano yetu as "Men talks" alisema kashamchunguza vya kutosha hivyo anataka kumuoa.

Huyo mwanamke ni mwalimu na kwa madai yake "Walimu ndio huwa wake Bora"

Michango tukatoa na harusi ikafanyika, ila mi nilimuonea huruma sanaa mwamba kwa kuamua kuoa.

SCENARIO
1. Mwaka jana kwenye mwezi wa 10 nilianza kuhisi utofauti wa yule demu/mwalimu/shemeji.

Kuna siku nilikua nakula zangu mingo nikamkuta kavaa blauzi ya net na suruali ya mchaniko mapajani. Kwa hiyo brauzi ya net aliyoivaa ilikua unaona kila kitu kasoro vile vilivyofunikwa na sidiria tu.

Sasa Kwa ninavyomjua mwamba ni mtu strictly sanaa, nikawaza "Mwamba kamruhusu mke avae nguo hizi kweli halafu atembee nazo mjini!"

Zile nguo za ajabu ziliendelea siku baada ya siku, raia tukawa tuna shangaa na kujiuliza maswali yasiyo na majibu!

Kwa kuwa hayanihusu "Nilipiga buyuuu"

2. Mwaka huu mwamba alianza kubadilika kimisemo.

Katikati ya maongezi yetu alikua anatoa kauli nzito na ngumu hasaaa..

Alikua akitoa kauli kama:

i. Ndoa muda mwengine ni upuuzi tu
ii. Wengine tupo kwenye ndoa sababu ya watoto tu.
iii. Mlioa nawashauri msioe
iv. Wanawake wapuuzi sanaa.

Mnaweza kuwa kwenye utani wanaume mnaongelea mademu ye akatoa kauli ngumu hasaaa.

THE TRUTH
Siku hizi braza anapost sanaa majuto ya ndoa kwenye WhatsApp status yake.
Hii inajidhihirisha kuwa kwenye ndoa yake "Kuna Majanga"

Status zake za WhatsApp ni manung'uniko na majuto ya ndoa. Kila siku lazima atoe dongo.

Na jana nilivyoona zimezidi ili bidi nimfate inbox na alichonijibu "Braza mi sina ndoa Tena!"

UBISHI
Huyu mwamba aliishi na demu miaka mi3.
Alihisi miaka mi3 inatosha kumjua mwalimu na kumuoa.

Mwalimu alivyoolewa ndani ya miaka mi2 akaamua kuonyesha mapembe. Na sasa mapembe yanamuumiza baharia mwenzangu.

Huyu ni mmoja wa wanaume wabishi ambao waligoma kuelewa ile slogan ya "USIOE" ye akahisi sisi ambao ambao hatujaoa ni mapimbii na sasa yamemkuta.

Na asichokujua hili limeanza kumuumiza mpaka kazini, maana ofisini hakai, na akikaa hakuna anachofanya. Dah kwakuwa wanaume huwa tunabebana then huwa tunafanya mpaka Kazi zake!

Mkiambiwa msioe muwe mnaelewa.

FINALIZING
Anyway tuendelee kutafuta hela.
If you think money does not bring happiness, nenda kawaulize waliopata ajira za TRA juzi hapo!

Money brings everything in life!

#YNWA
Liverpool, you will never walk alone.
 
Trust me bro, kuoa ni kuzuri, ila kupata mwanamke (mke) sahihi ndio ngumu. Kuna watu wanapata tabu, acha tu. Mke ni sehemu ya mali zako. Kama utakuwa na nyumba, gari na asset nyingine uongeze na mke sehemu ya hizo mali. Gari ikikusumbua ifanyie matengenezo. Nyumba iki crack fanya repairing. Mke akikusumbua control her feeling, thought na mahitaji yake.
Gari ikizidi kukusumbua uza. Isipouzika park. Mke akizidi kukusumbua ......aondoke tu. Japo inahitaji moyo kama mna watoto. Mara nyingi huwa wanatumia watoto kama kinga.
Hata wakitumia watoto kama kinga, lazima watoke tu.
 
Ukipigwa matukio kwenye ndoa au mahusiano ndyo akili inachangamka na kukaa sawa.Mahusiano yakipooza hamtoweza kupambana na hata changamoto ndogondogo.Kuogopa(escapism)kuoa ni udhaifu,uchoyo,ubaguzi na kutoshirikisha kichwa vema kutatua changamoto zako.
Sio uchoyo, sasa hela si ni zangu? Akale za baba yake.
 
Jamaa waliopata ajira juzi Kwa kweli wanna furaha Dana nimeitwa juzi kusherekea wanangu watatu tumefurai japo ni joblesss

Anyway ndoa bado ni mtihani Kwa kweli ila muhimu sana japo sio lazima
Ulihitimu lini chuo? Kozi ipi?
 
Ndoa ni very outdated institution. Asilimia kubwa ya watu wengi huingia huko kwa ssb ya social conformity.
 
Kama rafiki mwema....sikuona haja ya kutoa uzi wa rafiki yako kwa namna ya kumnanga......
Sina urafiki nae, ila ni jamaa yangu tu.
Sio kila mfanyakazi mwenzako ni rafiki yako, huwa ni jamaa tu.

Nimetoa Uzi ili wananchi wa JF wajifunze.

ndoa haina formula......
Inayo formula.
Na formula pekee ni USIOE.
ndio maana unaambiwa ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji......dunia duara,
Sina haja ya kutia maji ikiwa sina mpango wa kuingia saloon.
yaliyomkuta yanaweza kukukuta wewe.....
Hayawezi kwasababu sina mpango wa kuoa.
na makubwa hata zaid yaliyomkuta yeye.....tuwe na huruma kwa wenzetu wanapopitia magumu
Mkiambiwa msioe muwe mnaelewa.

#YNWA
 
Mkuu wewe marafiki zako ni wa hovyo hovyo tu.... Sijui unawatoa wapi....
Mimi naona vijana wanaoa huku wanasaidiana wanapendana, wanafanikiwa kabisa......
Jichuchunguze mkuu....
 
Mkuu wewe marafiki zako ni wa hovyo hovyo tu.... Sijui unawatoa wapi....
Mimi naona vijana wanaoa huku wanasaidiana wanapendana, wanafanikiwa kabisa......
Jichuchunguze mkuu....
Soma tena...
Alihamia kazini then nimemjulia kazini.
Si rafiki yangu kiasi hicho NIMUITE JAMAA.
Tukiwa kazini hatuna marafiki ni majamaa tu.

#YNWA
 
Back
Top Bottom