Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Umeongea point ya maana sana, kama professor wa political science! - nguvu ya Makonda iko katika ujinga wake mwenyewe, na ujinga wa Watanzania

Makonda na Watanzania wanahitaji kuelimika. Nani atatusaidia katika hili?

Lakini nahisi bado kuna zaidi ya ujinga wa Watanzania na wa Makonda vinavyomfanya ajiamini kiasi hiki.
 
🪑🇹🇿
Iyena iyena !!
Mafisadi Chamani kama wapo wataisoma namba !!
Makonda shikilia hapo hapo 😅😅🙏🙏🔥
 
Kama Ulimwelewa TPDF Kwenye Ile Kauli Yao Basi Uipeleke Na Huku 75% ya Akili Yako
 
🪑🇹🇿
Iyena iyena !!
Mafisadi Chamani kama wapo wataisoma namba !!
Makonda shikilia hapo hapo 😅😅🙏🙏🔥
Jibu lako ni signature yangu; Usimdharau mjinga, mwelimishe. La sivyo atajikusanya na wajinga wenzake na watatumia nguvu yao ya wajinga wengi kukuchagulia mbunge au hata raisi mjinga kama wao .
 
Wahenga walisemaga “ there is no great genius without some touch of madness “ 😅🙏🙏
 
Anachokifanya Makonda ni kuendelea kuivua chupi serikali na chama chake.

CCM ndio wenye Dola Kwa maana ya serikali na watendaji wote wako chini ya serikali ya CCM, kushindwa kufanya kazi kwa hao wafanyakazi na kuleta matokeo ni failure ya CCM na Serikali yake.

Ujinga uliopandikizwa na CCM kwenye jamii ndio unaofanya hao watendaji na Makonda wawe salama huko barabarani, vinginevyo kwa madhara waliosababisha walipaswa kupigwa mawe kila wapitapo.
 
Nakubaliana na wewe kwamba,kichwa kimezidi urefu wa mikono.Lakini naomba uwe muwazi tu,mbona Makonda wananchi wanamkubali sana,ni nini kipo nyuma ya kupendwa kwake na wananchi wa kawaida?
Ni ukweli ulio wazi kwamba ameziba pengo lililoachwa wazi na watawala,ambao kimsingi wameshinwa kabisa kutimiza wajibu wao.Aliyemtuma sina shaka yeyote kwamba analijua hili na kwa makusudi kabisa,anamtoa Makonda kafara ili afanye kazi ambayo yeye kashindwa.

Makusudi ni nini?Makusudi ni kujiweka mbali na wapigaji(kundi la wahuni),ili itakapofika 2025 aongeze nafasi yake ya kushinda uchaguzi.Kama atafanikiwa sijui,lakini Magufuli alipendwa na wananchi wa kawaida sana kwa sababu aliji-identify nao.Labda niseme wazi bila kumung'unya maneno,Makonda anapata nguvu kutoka kwa kiongozi wajuu kabisa wa nchi,Samia.
 
Sahihi kabisa !
 
Makonda katumwa na Samia ili kulaghai watu waone kuwa kumbe raia ni kiongozi mzuri sana ila tu watu aliowachagua ndiyo wabaya. Kwa kifupi anajaribu kutenganisha failures za serikali na rais ili ionekane kwamba tuna rais mzuri sana ila wateule wake siyo wazuri. Anatumia zile technique za Magufuli baada ya kuona kuwa watu walizipenda sana. Tatizo lililojitokeza ni kwamba Samia kama rais, hana uwezo na stamina ya kuzunguka huko na huko huku akifanya ghilba za aina hiyo. Akaona njia rahisi ni kumchukuwa mjinga mjinga fulani ili amtumie kama ''mbwa''. Nakuhakikishia hiyo kazi angepewa mtu mwenye akili na busara zake, asingekubali kufanya maigizo ya kijinga namna hii. Kwanza anatengeza uadui na watu wengi sana ambao hajui kesho wanaweza kuja kuwa na vyeo na uwezo wa kumshughulikia. Samia ni binadamu, wiki ijayo anaweza asiwepo, Makonda ataweka wapi uso wake? Si watagawana nyama wamle?
 
Hakika Umenena !
Hapo ile kambi mbaya inayotaka kuleta kauzibe itakuwa imeshaufyata !
Everything is happening for a reason !!
 
Hiyo Nguvu Imeonekana Wazi Wazi Ila Ndiyo Itakayokipasua Chama Vipande Viwili
Kwasasa Wote Wapo Kimya Ila Wanangoja 2025 Ndiyo Watatoa Kucha Zot
Kugombea Fito Za Nafasi Ya Rais Wa JMT, Subirini Muda Utaongea Yote
Mnayoyajua /Msiyoyajua Yatawekwa Hadharani Na Mtashangaa Sana
 
Inawezekana. Mara nyingine naamini walokole wanatumia nguvu fulani zilizojificha kufanya mambo yao! Lakini chama chenye mchanganyiko wa dini mbalimbali, haikiwezi kudumu kwa kuendeshwa na nguvu za kilokole!
Nani mlokole??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…