Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Ataweza kuwafikia na kutatua matatizo ya masikini wangapi? Nchi ina watu >60 million. Halafu, atatatua matatizo kwa kutumia watendaji hao hao “walioshindwa kazi” kwenye mfumo rasmi chini ya uongozi wa CCM? Halafu pia kwa gharama gani? Misafara yote hiyo?

Au ni kuwapa faraja ya kisaikolojia tu kama ile wanayotoa waganga wa kienyeji, mitume na manabii baada ya mifumo rasmi kushindwa kuwaponya/kuwafanikisha kama ilivyotarajiwa?

Kwa kweli huwa nastaajabu sana kuona kumbe kweli kuna watu wengi nchini wanaoamini kuwa kiongozi bora ni yule ambaye muda mwingi anazunguka kusikiliza matatizo ya mtu mmoja mmoja kwenye mikutano ya hadhara kisha kuagiza kupitia media watendaji husika wayatatue! Ukiondoa shere iliyomo katika hilo tukio-kituko, sijui Watanzania wangapi wanajiuliza gharama za hiyo misafara, tija yake, na hasara inayopatikana kwenye uchumi hasa ukifikiria suala la opportunity cost. Yaani yote hiyo ni ili kuwazuga na kuwapa faraja “wajinga”! Very sad!

Yaani kama vile hatukwenda shule wala kuelimika? Hatujui kabisa serikali ni kitu gani na inatakiwa kufanya kazi vipi? Kweli tunahitaji hizi exorbitant charades za kina Makonda?
 
Hio mifumo tayari ipo,
Ila wenye dhamana hawawajibiki positively!
Anatakiwa mtu anayewateua awe imara kuwasimamia Basi!
 
Ninyi ndio wajinga lakini watanzania siyo wajinga . Watanzania wanatambua kazi njema na yakutuka inayofanywa na Mheshimiwa Makonda katika kuwatetea na kuwasemea watanzania.watanzania wanaona namna ziara za Mheshimiwa Makonda zilivyochochea uwajibikaji kwa viongozi mbalimbali waliokuwa wanafanya kazi kwa mazoea na kukaa maofisini tu bila kutoka kwenda kuwasikiliza wananchi.

Hata hivyo napenda kukwambia kuwa kaa ukijiandaa maana huyo ipo siku moja utamtizama kupitia Tv akiapishwa kuwa Rais wa Tanzania.
 
Bila shaka wewe ni wala viongozi wavivu,wazembe na waliokuwa wanafanya kazi kwa mazoea.ndio maana unatetea ujinga wa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kufanya ufisadi katika ofisi za umma,kudhulumu wananchi haki zao.kufanya hujuma na kila aina ya uozo.watanzania ambao ndio wenye nchi wataet kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya na pia watanzania wataendelea kuwapiga vita na kuwapuuza watu aina yako na wenye mawazo finyu kama wewe.
 
Mawazo huru!

Dola itakua imemwambia mama hatoshi,Kuna mtu anahitajika afanye kazi yako ,mtu kivuli,yaani Raise kiutendaji lakini sio kikatiba!!

Ndio makonda akaonekana anafaa na yeye ndio ana sauti nani apite au akatwe hapo 2025!!

Makonda ni Raid kivuli kabla hajawa Rais rasmi!

Source:- trust me broo!
 
Acha ujinga wako wa kiwango cha juu.yaani wewe ni mtu wa hovyoo sana ,sijuwi hata kama unajielewa. Kwa hiyo Mheshimiwa Makonda ashindwe na aogope kufanya kazi kwa weledi na kuwabana wezi,wala rushwa ,wazembe kazini na mafisadi eti kwa kuogopa kwamba kesho watakuwa ni viongozi? Kwa hiyo wewe kwako cheo ni muhimu sana kuliko maisha ya mama ya watanzania? Kwako cheo kinacholihakikishia shibe tumbo lako mwenyewe ndio furaha kwako kuliko mateso ya wananchi wanaodhulumiwa haki zao na kunyanyaswa?

Huu ujinga mnauandika na kuwaza mkiwa mmelewa? Umeandika huu ujinga ukiwa mgonjwa au mzima? Kwa hiyo wewe unataka watumishi wazembe na wasiotimiza majukumu yao wachekewe tu kwa kuogopa kukosana nao? Kwanini unamawazo ya kijinga kiasi hiki? Wewe hufai hata kuongoza familia yako maana mawazo yako ni mfu na hujitambui kabisa. Halafu ukome kutukana viongozi wetu.
 
Acha kujidanganya wewe. Fomu ya urais ndani ya CCM Ni moja tu kwa ajili ya Rais Samia.
 
Inawezekana. Mara nyingine naamini walokole wanatumia nguvu fulani zilizojificha kufanya mambo yao! Lakini chama chenye mchanganyiko wa dini mbalimbali, haikiwezi kudumu kwa kuendeshwa na nguvu za kilokole!
hakuna kitu kiitwacho "nguvu za kilokole". Kuna nguvu za Mungu Aliye hai, Yehova.

KWA BWANA YESU KILA GOTI LITAPIGWA!
 
Hio mifumo tayari ipo,
Ila wenye dhamana hawawajibiki positively!
Anatakiwa mtu anayewateua awe imara kuwasimamia Basi!
Mifumo ipo lakini haiendani na uhalisia. It is a top bottom approach, and the president acts as a micro-chip, which controls everything! Inatakiwa wananchi wawe ndiyo wanaochagua na kuwajibisha viongozi wao wa karibu. Haya mambo ya rais kuteua na kuwapelekea wananchi viongozi haufanyi kazi na ndicho kinachotokea sasa.
 
Kwa wewe unayetegemea watu ill maisha yako yaende kulamba makalio sawa! Makonda anamtegemea Mungu!
 
We umeingia chaka. Kuna nani mwenye nguvu nchi hii zaidi ya Rais? Msitafute namna ya kukweza hilo kabila lenu la kishamba. Yule mtu wenu aliyewakweza ameshatutoka au hamuamini bado?
Mtu ajikweze halafu ajiite muuaji akili huna wasukuma ndo hawataki hiyo comment
 
Mleta mada ni mtu asiejua chochote kuhusu nafasi za kiuongozi ndani ya ccm,yaani umesema mwenyekiti wa ccm mkoa ni mkubwa kuliko katibu wa Nec,itikadi,mafunzo na uenezi?,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…