Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Bro Biblia ilikuwepo miaka 600 kabla ya Qur'an Tukufu, Agano la Kale lilikuwepo Kwa zaidi ya miaka 600 huku Agano Jipya ni miaka 600
 
Mungu Hayupo.

Ni mawazo na imaginations za watu tu.

Baada ya kushindwa kufahamu chanzo cha ulimwengu binadamu waka unda kiumbe na kukipa jina Mungu..
 
:::::NI UONGO SABABU NYINGI NI TAFITI BINAFSI HAZINA USHAHIDI WA KINA
Kwa hiyo Bora uamini Wikipedia ambao Ina magoli ya Ronaldo mpaka ya Jana. Au Bora uamini kitabu ambacho hujui kimeandikwa na Nani au lini, na kinatetea utumwa, uuaji, kinasema dunia ni flat, kinasema mvua Ni madirisha ya mbinguni kufunguliwa. Bora uamini kipi Sayansi ambayo ilimpeleka mzungu mwezini au dini aliyotumia kukutawala na yeye kaiacha huku waafrica wakiendelea kuumizana na kuibiana makanisani
 
Kusema kweli Biblia haijachakachuliwa, maana maandishi ya zamani yaliyokutwa Qumran mwaka 1947 ya zamani sana ya Agano la Kale, walikuta ni maandishi Yale yale sawasawa na Biblia zilizopo.
 
Vyovyote vile. Lakini hatakiwi kumuadhibu mtu kisa makosa yake mwenyewe. Unamuumba mtu na nyege afu akifanya mapenzi Ni dhambi mpaka sijui ndoa. Hizi sheria Ni za makabila ya kale sio Sheria za muumba yote
Sheria hizi Zina Faida kuliko kitu chochote.
Angalia, ukifanya mapenzi na mke wa mtu, utapelekea ndoa kuvunjika na pia malezi ya familia hayatokuwepo.
Leo hii ukitembea na wanawake wengi na ukazaa na Kila mwanamke bila kumuoa, atapatwa na fedheha ambayo itamuumiza nafsi yake na inaweza pelekea ajiue au apate pyschological disorder au watoto wasilelewe vizuri.
Mungu aliona mbali mno kuweka sheria zile angalau zinaleta ustaraabu.
Mfano kama ushoga ungeruhusiwa, unadhani watu wangefika bilioni 8? Unajua hasara ya kukosa rasilimali watu?
 
MUNGU YUPI SASA ALIWEKA HIZI SHERIA??????? MAANA KILA MUNGU WA KILA DINI ANA SHERIA ZAKE MKUU...
 
Ndo sio Sasa sheria za mtu. Haya Mimi Nina miaka 22 na demu wangu ana miaka 20. Tunafanya Mapenzi bila kucheat na tunatumia uzazi wa mpango. Haya kosa langu hapo Mimi Ni Nini.
 
Then why the stori is different in the same thing 😎
Biblia na Qur'an zimeandikwa na watu tofauti na zama tofauti na desturi tofauti.
Nikupe mfano mzuri
Torati ya Musa yenye vitabu vitano vya mwanzo pale Kuna kitabu Cha Walawi sura ya 11 imekatazwa WAEBRANIA wasile wanyama akiwemo ng'amia, kambale.
Na Wayahudi wameishika mpaka Leo
Ukija kwenye Taurati ya Qur'an nguruwe haruhusiwi kula ila ng'amia na kambale wanamla.
Huoni tofauti apo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…