Searching for the truth
JF-Expert Member
- Mar 22, 2022
- 903
- 1,851
- Thread starter
- #181
Kwa hiyo turudi kule kule kwenye sayansi kuwa "In every action there is equal and opposite reaction" 🥱Nijaribu kukujibu. Kabla sijafanya hivyo nitoe angalizo kwamba maswali juu ya Mungu hayana empirical answers, isipokuwa logical answers. Ukilazimisha logical iwe empirical na kinyume chake basi ni vyema ukaacha kuamini uwapo wa Mungu na nguvu zake.
Swali lako juu ya shetani na nguvu zake: Uwapo wa shetani ndio unaodhihirisha uwapo wa Mungu, bila usiku mchana haupo, bila kulia kushoto hakutakuwapo. Bila adhabu zawadi haina maana. Kadhalika Mungu aliumba hao malaika, na moja akasaliti Mungu akamfanya awe adhabu ya milele itakayotofautisha walio wake na wasio wake. Ni kwa nguvu zake Mungu alimfanya Lucifer awe shetani, yaani nguvu kinzani. Na mara nyingi Mungu ameonyesha ushindi dhidi ya shetani. Ungeuliza pia kwanini Mungu anayesamehe kila Jambo hakumsamehe shetani, jibu ni hilo hapo juu: lazima kuwe na usiku ili tuujue mchana. Lazima kuwe na wovu tuujuwe wema. The two are separable but interdependent.
Swali kwamba Mungu alimpa Adam msaidizi dhahifu hadi akashawishiwa na nyoka kula tunda katazwa.
Ndugu, kwani aliyekuambia kwamba Adamu hakuwa dhahifu Nani? Unadhani Adamu alisamehewa dhambi kwasababu alipewa tu lile tunda? Wote walikuwa dhahifu na Mungu alijuwa hilo ndio maana akawaonya wasile tunda walilokatazwa. Yaani binadamu wote ni dhaifu tangu kuumbwa, kumbuka Mungu hakuumba binadamu kama malaika. Hata Yesu aliyeshuka kwa baba akavaa ubinadamu naye alikuwa dhahifu na akakili udhahifu wake mbele ya mitume wake.
Lakini mkuu kama Mungu ndiye alimfanya Lucifer kuwa shetani kwa nguvu zake mwenyewe basi kazi yake itakuwa haina maana.
Kwa sababu kwa muktadha wako wewe even now Mungu ndiye anae ku-control
Utende dhambi ama usitende,uende mbinguni ama jehanam, yaani kana kwamba sisi hatuna free will tena isipokuwa Mungu ndiye anakifsnyia wewe maamuzi kwa free will zake mwenyewe.
Kama nitakuwa nimekuelewa vizuri lakini.