Any way acha iwe mwenye bidhaa zake ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho.
Lakini Je, vipi kuhusu sisi kumjua yeye.
Tunamjua yeye kupitia vitabu vyake vya dini (mfano Biblia na Qur'an).
Swali ni Je, kwanini sasa vitabu vya dini vituambie stori tofauti kwenye kitu kile kile kimoja ?
It means kuna kitabu kitakuwa kimepotosha ?
Hivyo vitabu mnavyosoma wajanja wenu akina Paulo wamevichakachua Kwa makusudi Ili kukupotezeni msifuate dini ya Mungu ila mfuate dini yao
Hi yapa the same story Mungu alimuhadithia nabii Musa baadae akaja kumuhadithia mtume Muhammad kuhusu wale malaika walioenda Kwa nabii Ibrahim kumbashiria mtoto Isihaka
Mwanzo 18:2
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
Mwanzo 18:3
akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Mwanzo 18:4
Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
Mwanzo 18:5
Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
Mwanzo 18:6
Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
Mwanzo 18:7
Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.
Mwanzo 18:8
Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
Mwanzo 18:9
Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
Mwanzo 18:10
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
Quran 51:24
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
25
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni.
26
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
27
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
28
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu.
29
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
30
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua.
Bibilia inasema wale wageni Ibrahim alipowaandalia chakula walikula
Quran inasema walipoandaliwa chakula hawajakula na hapo ndipo Ibrahim alipojua kuwa wale ni malaika
Ukweli ni kwamba Malaika hawali chakula so hiyo story katika bibilia imechakachuliwa