Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Swali langu kwako.

Kama aliyeasi alikuwa ni jini siyo malaika, ina maana malaika na majini wote walikuwepo mbinguni na walikuwa wamechangamana pamoja ?
Jibu Ndio na Kwa mujibu wa Quran hapa ndio anafukuzwa humo peponi alipokuwa anaishi Baada ya kupinga amri ya Mungu ya kumsujudia Adam

Qurani 7:18
Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

Quran 7:19
Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu.
 
Nafikiri kutumia akili za mwanadamu kumtafakari Mungu ni kukimbiza upepo.
Akili za Mungu hazichunguziki. Isaya 40:28
 
Na hapohapo unajiuliza kama kweli Mungu anataka watu tumuelewe, kwanini atumie lugha ya mafumbo?
Si ndiyo hapo sasa.

Ma siyo hivo tu, kwanini atugawe katika makundi (dini mbali mbali) alafu atupe vitabu vyenye stori tofauti kumuhusu.

Mfano : Stori zilizoko kwenye Biblia hazifanani sana na zilizoko kwenye Qur'an, unakuta kisa kile kile kimoja kinaelezewa tofauti na upande mwingine.

Mfano: Sababu ya Lucifer kuasi, kwenye biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Sababu ya Kaini kumuua Habili kwenye biblia ni tofauti kabisa na ya kwenye Qur'an.

Mahali ilipokuwa Bustani ya Eden kwa mujibu wa Biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Aliyetaka kuchinjwa na Ibrahim kama Sadaka, aliyeatajwa kwenye biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Sasa kama lengo la Mungu ni sisi tumjue kiusahahi, kwanini sasa kutugawanya dini tofauti, vitabu tofauti ?
 
Nafikiri kutumia akili za mwanadamu kumtafakari Mungu ni kukimbiza upepo.
Akili za Mungu hazichunguziki. Isaya 40:28
Hapo ndipo unapojifungia uwezo wa kufikiri.

Ingelikuwa hivo basi hata wazo la kuwa yupo ingelikuwa la kipuuzi, maana haonekani kwa macho kwa nini nifikiri kuwa yupo
 
Jibu Ndio na Kwa mujibu wa Quran hapa ndio anafukuzwa humo peponi alipokuwa anaishi Baada ya kupinga amri ya Mungu ya kumsujudia Adam

Qurani 7:18
Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.

Quran 7:19
Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu.
Duuh...

I think you have something to adress the World
 
Swali zuri

Kama sisi Ni wa thamani mbona shetani ?

Ni kweli sisi ni wathamani lakini tu wa thamani na wenye nguvu katika yeye (tukifuata matakwa yake) nje ya hapo were useless rejea hadithi za nuhu na gomola. Aliteketeza kwa sababu hawakua na thamani tena

Pili shetani yupo ili kutu challenge kama kama Mungu alivyoamua mwenyewe kuwa tupitishwe kwenya majaribio makali na watakao shinda ndio wakwake.

Tatu rejea mfano wa baba na watoto wanne katika challenge ya kujificha.

Ndio anawapenda sana ila kaamua kuwapa challenge yeye kama baba.

Hiki kitu tunafanya hata kwenye familia zetu Kuna na wapa hard condition wanangu ili wawe bora zaidi na ngangari japo nawapenda

Karibu
Duuh...

Kwa mujibu wako, nitarudi kule kule kuwa Mungu wako ni mwonevu sana.

Japo yeye ndiye anajua kwanini anatuonea, ila cha msingi ni kwamba yeye ni mwonevu
 
Lakini nguvu inayotenda kazi ni moja tu kwa imani yoyote. Ni Mungu muumba.

Umaweza ukawa na imani yako leo na ukapokea nguvu ya Mungu yuleyule muumba.

Ni somo refu na pana lakini ukweli ndip huo. Hata mchawi anaenda kwa nguvu ileile ya Muumba. Ndio maana kwa mawazo maovu ya wanadamu kuna maarifa Mungu amewafungia wanadamu.

Ova
Kwa hiyo unataka kunambia kuwa, Mababu zetu walikuwa wakiiomba miungu alafu miungu nayo inaomba kwa Mungu mkuu (muumbaji) ndiyo maombi yao yanajibiwa au ?
 
Yes Roman empire ilielezwa kwenye kitabu Cha Danieli.
Ila Marekani na Anguko lake Kwa tafsiri yangu binafsi, naona Ufunuo 17&18....
Marekani itaanguka na kuwa nchi ya kawaida although sijajua lini .
We subiri tu aanguke, mwenzako anaachana na Imani potofu na kujiendeleza kisayansi na kitechnolojia na waafrika tukibaki na huu uwoga wetu wa kifikra tutaishia tu kuwekewa satellite na kutengenezewa chanjo.
 
Si ndiyo hapo sasa.

Ma siyo hivo tu, kwanini atugawe katika makundi (dini mbali mbali) alafu atupe vitabu vyenye stori tofauti kumuhusu.

Mfano : Stori zilizoko kwenye Biblia hazifanani sana na zilizoko kwenye Qur'an, unakuta kisa kile kile kimoja kinaelezewa tofauti na upande mwingine.

Mfano: Sababu ya Lucifer kuasi, kwenye biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Sababu ya Kaini kumuua Habili kwenye biblia ni tofauti kabisa na ya kwenye Qur'an.

Mahali ilipokuwa Bustani ya Eden kwa mujibu wa Biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Aliyetaka kuchinjwa na Ibrahim kama Sadaka, aliyeatajwa kwenye biblia ni tofauti kabisa na kwenye Qur'an.

Sasa kama lengo la Mungu ni sisi tumjue kiusahahihi, kwanini sasa kutugawanya dini tofauti, vitabu tofauti ?
Hii ndo inaonyeshwa kwamba haya sio maneno ya Mungu Bali Ni story za binadamu.
 
kuna watu hawamjui Mungu na ni matajiri
kuomba sio kupata
Lazima kuna namnaa ama sivyo basi binadamu wote sio sawa
Hii inaonyesha hamna tofauti ya kuomba na kutokuomba kwa sababu kitu kinaweza tokea au kisitokee Ni juhudi tu ndo zinaleta maendeleo. Ndo maana wazungu wanajenga viwanda wakati waafrica wanajenga makanisa.
 
kuna watu hawamjui Mungu na ni matajiri
kuomba sio kupata
Lazima kuna namnaa ama sivyo basi binadamu wote sio sawa
Ndio maana nikasema KUMBUKA kuomba sio kukesha na kupayuka makanisa.

Halafu wengi mnadhani kusema unamjua Mungu ni kutamka jina lake na kuingia majengo ya ibada.

Huyo unasema hamjui Mungu ndio anamjua zaidi ya wewe ukeshae majengo ya ibada.
 
Utafiti wa kijiolojia. Kuelewa Hali ya kihistoria ya udongo na mawe duniani. Wanaweza jua kwa kutafiti Kama sehemu fulani mda fulani kulitokea kitu fulani Kama Ni mafuriko tetemeko au mmomonyoko. In short hamna evidence ya dunia nzima kujaa maji na hiki kitu hakiwezekani kifizikia na kibioloji

Kuna makala nillisoma mwaka jana, ngoja nimenyee kidogo.

Kwanza, kumbuka kuwa asilimia kama 75 % au 78% (Robo tatu ya Dunia) ni maji mpaka sasa.

That means, sehemu ya nchi kavu duniani huwa ni ndogo sana (only 23% to 25 %).

Hiyo makala niliyosoma mwaka jana ilikuwa ni ya mambo ya Geology na ulikuwa ni utafti mpya kabisa.

Na utafti huo ulikuwa una-suggest kwamba : "INDIA ndiyo nchi ya kwanza duniani kujitokeza kama ardhi juu ya dunia". That means dunia nzima hapo mwanzo ilikuwa ni maji tupu.
 
Kwa hiyo unataka kunambia kuwa, Mababu zetu walikuwa wakiiomba miungu alafu miungu nayo inaomba kwa Mungu mkuu (muumbaji) ndiyo maombi yao yanajibiwa au ?
Kwa ufupi chief Mangungo atakuwa na afadhali kuliko uelewa ulonao katika hili.

Nakuombea Mungu azidi kukufundisha ila achilia kwanza kilichofunga moyo wako.
 
Kwako ni uongo kulingana na ulichonacho yaani unachofahamu.

Kwangu ni ukweli 100% utake ama usitake. Ova
Mimi kunambia kuwa watu wanaoishi maisha mazuri au ya shida ni maamuzi yao, hapa nakataa.

Sometimes mifumo inaweza ku-determine maisha ya watu, ku-faver wengine na kuwaumiza wengine.

Unless unambie wewe ni freemason/illuminati, maana nyie naskiaga mnaujua ulimwengu kuliko mtu yeyote yule 😁😁😁
 
Hii inaonyesha hamna tofauti ya kuomba na kutokuomba kwa sababu kitu kinaweza tokea au kisitokee Ni juhudi tu ndo zinaleta maendeleo. Ndo maana wazungu wanajenga viwanda wakati waafrica wanajenga makanisa.
Mi naamini sio juhudi tu kuna jambo tu lipo ndio maana Asia wanaamini sana kuhusu Fate/Destiny yani haya maisha ni kama yamepangwa nahisi ndio mana kuna watu wanafanya unabii wa yajayo
 
Back
Top Bottom