Duuh...
Swali la Mungu alikuwa aliishi wapi kabla ya kuiumba MBINGU ambayo ni makao yake ni swali la msingi sana, na inabidi wataalamu wa haya mambo mje mjibu huku (ila kwa reference siyo kwenye fikra zenu).
Lakini mimi nikujibu hilo la heavenly bodies kugongana, probably inawezekana zamani viliwahi kugongana na hata wanasayansi wanasema hivo.
Na hata wana sayansi wa leo (modern scientists) wanatuambia kuwa miaka bilioni kadhaa ijayo hii galaxy yetu (milky way) itakuja kugongana na galaxy ya jiran (Adromeda galaxy) na bado ya mgongano huo itazaliwa galaxy mpya kwa jina lingine,lakini hakuna proof maana haijatokea bado.
Lakini pia, can you imagine kwenye galaxy yetu pekee (milky way) kuna kana kadiriwa kuwa na nyota kati ya bilion 300 mpaka bilion 500, pamoja na sayari zisizopungua bilion 100.
Sasa, hii galaxy yetu ni mojawapo ya galaxy ndogo sana, alafu fukiria idadi ya nyota zilizopo kwenye hiyo galaxy, fananisha na galaxy zingine kubwa zaidi ya yetu zitakuwa na nyota ngapi na sayari ngapi.
Alafu kumbuka galaxy zenyewe zipo nyingi sana, na kila galaxy ina ina mabilioni ya nyota na sayari.
Alafu imagine the whole observabale universe inakadiriwa kuwa na nyota siyo chini ya trilion 12.
Alafu wanasayansi wanakadiria kuwa "The number of stars in the universe is much bigger than all the grains of sand in the beaches on planet earth"
Na hivyo vyote viko kwenye motion, waweza nambia kama hivi vitu havina anayevidhibiti huoni kuwa vingekuwa vinagongana kila sekunde ?
Au hujaskia matukio ya Austronomy, wakisema kuwa "kuna jiwe kubwa la angani linakuja uelekeo wa dunia kuja kuiogonga la likiigonga dunia ndiyo maisha kwa heri" .
Lakini mara unashangaa wanatoa repoti tena kuwa hilo jiwe lililokuwa linakuja uelekeo wa dunia sasahivi limeshabadili mwelekeo siyo hatari tena kwa dunia.
We unadhani huo mwelekeo linabadilisha tu lenyewe bila mdhibiti ?
Kuna designer wa huu ulimwengu broo hata kama hatumwoni kwa macho.