Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Ila kwenye story ya Job shetani alikuwa mbinguni na Mungu wakibet
 
Exactly,our mind is limited.
It's not limited..

Ni hofu za watu kuogopa kuongea kwa uwazi na hadharani kwamba Mungu hayupo. ila Akilini mwao na kwenye vichwa vyao huji uliza sana kama kweli huyu Mungu yupo...

Watu wana "fear of unknown" kwamba kuna moto wa milele utawachoma wakisema kwamba huyo Mungu hayupo
 
Mwili wa Binadamu na nature ya viumbe hai Inaelezeka na evolution and origin of species. Hii mada ishamalizwaga. Ndo maana huwezi ona mtu wa dini anaongelea mwili watu wanaongelea uumbaji wa ulimwengu. Soma kitabu Cha Darwin utaelewa hizo system zote Ni mechanisms za nature.
 
Upumbavu wa mwanadamu ni pale anapofika mahali akaamini kitu ambacho hata dhamiri yake inamshuhudia kuwa alichoamini ni upumbavu!! Yaani mtu anaamini kuwa mifumo yote ya uhai uliyoiorodhesha na ambayo hujaiorodhesha ilitokea tu kama matokeo ya ajali nzuri ( a good chaotic interactions without any designer). Ni sawa na mtu kuamini kuwa inawezekana mtu akachanganya kalamu nyingi na karatasi nyingi kisha ikatokea barua inayosomeka na kukupa taarifa kuwa mkeo uliyemwacha ni akiwa na mimba amejifungua mtoto wa kike jana saa sita kamili ya usiku!!


Cc, mbingunikwetu 👏🏼
 
Na watu wa dini wameutengeneza huu Moto ili kuwatishia watu. Ndo maana katika agano la kale hamna Moto Kuna mbinguni tu. Ila wakaona haikoshi kushawishi watu wakaamua kuleta Moto ili kulazimisha watu waogope vitu vya kufikirika. Zeus mwenyewe ana Moto wake, kwa Nini humwamini yeye, na hivi vitu mnafundishwa mkiwa na akili Changa ndo maana unaamini kirahisi. Mtu mzima mwenye akili zake Kama hajawahi kujua dini akisoma story za Biblia anaweza akaona Kama hadithi za watoto
 
Hi inaitwa black and white fallacy kwenye logic. Unanipa option mbili wakati zipo nyingi. Kwani lazma iwe ajali au Mungu. Inaweza kuwa process zingine sio hizo mbili tu.
 
Mkuu ninavyojua mimi ni kwamba: Mwongozo wa Ukristo ni Biblia, na humo ndani ya Ukristi kuna madhehebu mengi, na katika Ukristo kugawanyika kwa madhehebu mengi, kila dhehebu limekuwa na tofauti flani ya mafundisho na dhehebu lingine.

Lakini Biblia inayotumika kwa madhehebu mengi huwa ni ile ile moja.

Na nafikiri kazalishwa kwa madhehebu mengine kulitokana na kuona dhehebu mama l(roman catholic) kama linaenda kinyume na maandiko.

Hivyo basi mpaka leo humo humo kwenye baadhi ya madhehebu ya kikristo hayaamini katika utatu mtakatifu, japo mimi utatu mtakatifu nitakuelewesha badae nanavyoelewa mimi.

Na kinachofanya labda kuwa na mafundisho tofauti nadni ya Biblia moja ni tatizo la ufasiri labda maana Biblia iko katika mafumbo sana.

Lakini swali la msingi kwako ni : Je, inakuwaje Mungu aache watu wake wapotoke kutoka kwenye maandiko sahihi na kuruhu kuingia kwa maandiko ya kupotosha (kama ambavyo unasema labda kuna watu walipotosha biblia kwa maslahi yao binafsi) ?

Yaani kMungu kama lengo lake ni sisi kumwabudu katika haki na kweli, na katupa mwongozo wa kitabu chake, kwanini aruhusu kitabu kiwe zaidi ya kimoja alafu stori tofauti, na kwanini aruhusu hilo litokee lipotoshe watu wakati lengo ni sisi tumjue katika hali ya ukweli.
 
Anhaaa, kwahiyo wewe unaamini theory za Darwin ndiyo zimeelezea asili ya mtu ametokeaje si ndiyo?!


Okay, tuelimishe kwa mujibu wa Darwin, Asili ya Mtu ni Nini!?


 
Creator lazima kiwe kitu kimoja?

Naona unalazimisha kwamba designer wa vyote awe mmoja.

Si lazima designer awe mmoja wanaweza wakawa wengi zaidi ya mmoja.
 
Nimemaanisha sheria za asili.
 
Hi inaitwa black and white fallacy kwenye logic. Unanipa option mbili wakati zipo nyingi. Kwani lazma iwe ajali au Mungu. Inaweza kuwa process zingine sio hizo mbili tu.
Ngoja nikushauri kitu kuwa open minded.... Kisha itumie akili yako vizuri bila kutumia kitabu chochote wala theory za kina Darwin,

Jiulize maswali kuhusu hii Dunia, na Kwa kuanzia anza kutafuta asili ya mtu ni Nini?, kwa kudadisi akili yako bila kushikiwa akili na kitabu au Theory ya mtu yoyote yule.
 
SimbaMpole123 .......je we unaamini Kuna designer?
 
Pamoja na kuwa umewaza vyema sana kwamba Mungu yupo, umepotea huko kwa akina Eva, Adam nk. We jitahidi tu kuona mambo yalivyo na yakupe mwanga kwamba Mungu yupo ila ukiona unawaza ya akina Eva na Adam wake basi ujue kuwaza kwako hakuko sahihi bado
 
Asili ya mtu Mimi sijui na wewe haujui..lakini hayo masystem uliyotaka asili take Ni evolutionary mechanism.
Unaweza kuthibitisha hiyo Evolutionary mechanism ilitokeaje mpaka tukapata hizo system?

Let's trace back our Generation 🧬...... Mfano tu, rudisha kizazi chako kuanzia Mama yako, Mama yake na Mama yako na Bibi yake bibi yako..... Na kuendelea mpaka tunampata Mama wa watu wote!


Jiulize sasa, Je kwa mujibu wa Evolutionary mechanism huyo Mama wa kwanza alitokea wapi?


Ukitoa majibu yanayoingia akilini nakua atheist sasa hivi.
 
Pamoja na kuwa umewaza vyema sana kwamba Mungu yupo, umepotea huko kwa akina Eva, Adam nk. We jitahidi tu kuona mambo yalivyo na yakupe mwanga kwamba Mungu yupo ila ukiona unawaza ya akina Eva na Adam wake basi ujue kuwaza kwako hakuko sahihi bado
Weka sahihi huko kwa Lucifer na Eva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…