hateeb10
JF-Expert Member
- Dec 8, 2022
- 2,920
- 1,223
Unataka ushahidi wa Nini kati ya haya :-,Nipe ushahidi tusibishane kwa hisia
1. Mungu yupo/hayupo?
2. Mungu ni Mmoja/ Ni wengi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka ushahidi wa Nini kati ya haya :-,Nipe ushahidi tusibishane kwa hisia
Ila kwenye story ya Job shetani alikuwa mbinguni na Mungu wakibetMstari
Mstari
Hujanielewa vizuri kama ulivyohisi kwenye mstari wako wa mwisho. Soma swali la mtoa mada Kisha soma jibu langu. Kiufupi shetani hayuko na malaika mbinguni, huko alishafukuzwa na hana nguvu mbele ya Mungu kama mtoa mada anavyodhani. Nguvu ya shetani iko duniani anakojaribu kushawishi watu, nguvu yake ndio mtihani wa binadamu katika kumtukuza na kumjuwa Mungu. God doesn't control everything but He is capable of and can do that at His own will and convenience. Sasa nilitoa disclaimer kwamba we can't discuss God empirically but logically.
It's not limited..Exactly,our mind is limited.
Mwili wa Binadamu na nature ya viumbe hai Inaelezeka na evolution and origin of species. Hii mada ishamalizwaga. Ndo maana huwezi ona mtu wa dini anaongelea mwili watu wanaongelea uumbaji wa ulimwengu. Soma kitabu Cha Darwin utaelewa hizo system zote Ni mechanisms za nature.View attachment 2603766
Iwafikie wale wote wanaopinga uwepo wa THE BEST DESIGNER/THE BEST CREATOR!.,
Human being is a work of art& engineering.... Yani Mtu alivyo tu inaonyesha kuna ufundi ambao umefanya mpaka ukaona mifumo yote kwenye mwili wa binadamu kuanzia:-
1. Respiratory system
2. Digestive system,
3. Circulatory System
4. Nervous System
5. Endocrine system
6. Muscular system
7. Skeletal system
8. Immune system
9. Urinary system
10. Reproductive system.
Yani, Ingetosha kabisa kuangalia mwili wako na jinsi unavyofanya kazi kujua kwamba kuna DESIGNER aliyeweka mifumo yote hiyo., Au kama unahisi mwili wa binadamu na jinsi unavyofanya kazi umejitokeza tu from nowhere, let's conclude that hata robots tunazoziona zimejitokeza tu from nowhere..... Does it make sense?
Upumbavu wa mwanadamu ni pale anapofika mahali akaamini kitu ambacho hata dhamiri yake inamshuhudia kuwa alichoamini ni upumbavu!! Yaani mtu anaamini kuwa mifumo yote ya uhai uliyoiorodhesha na ambayo hujaiorodhesha ilitokea tu kama matokeo ya ajali nzuri ( a good chaotic interactions without any designer). Ni sawa na mtu kuamini kuwa inawezekana mtu akachanganya kalamu nyingi na karatasi nyingi kisha ikatokea barua inayosomeka na kukupa taarifa kuwa mkeo uliyemwacha ni akiwa na mimba amejifungua mtoto wa kike jana saa sita kamili ya usiku!!It's not limited..
Ni hofu za watu kuogopa kuongea kwa uwazi na hadharani kwamba Mungu hayupo. ila Akilini mwao na kwenye vichwa vyao huji uliza sana kama kweli huyu Mungu yupo...
Watu wana "fear of unknown" kwamba kuna moto wa milele utawachoma wakisema kwamba huyo Mungu hayupo
Na watu wa dini wameutengeneza huu Moto ili kuwatishia watu. Ndo maana katika agano la kale hamna Moto Kuna mbinguni tu. Ila wakaona haikoshi kushawishi watu wakaamua kuleta Moto ili kulazimisha watu waogope vitu vya kufikirika. Zeus mwenyewe ana Moto wake, kwa Nini humwamini yeye, na hivi vitu mnafundishwa mkiwa na akili Changa ndo maana unaamini kirahisi. Mtu mzima mwenye akili zake Kama hajawahi kujua dini akisoma story za Biblia anaweza akaona Kama hadithi za watotoIt's not limited..
Ni hofu za watu kuogopa kuongea kwa uwazi na hadharani kwamba Mungu hayupo. ila Akilini mwao na kwenye vichwa vyao huji uliza sana kama kweli huyu Mungu yupo...
Watu wana "fear of unknown" kwamba kuna moto wa milele utawachoma wakisema kwamba huyo Mungu hayupo
Hi inaitwa black and white fallacy kwenye logic. Unanipa option mbili wakati zipo nyingi. Kwani lazma iwe ajali au Mungu. Inaweza kuwa process zingine sio hizo mbili tu.Upumbavu wa mwanadamu ni pale anapofika mahali akaamini kitu ambacho hata dhamiri yake inamshuhudia kuwa alichoamini ni upumbavu!! Yaani mtu anaamini kuwa mifumo yote ya uhai uliyoiorodhesha na ambayo hujaiorodhesha ilitokea tu kama matokeo ya ajali nzuri ( a good chaotic interactions without any designer). Ni sawa na mtu kuamini kuwa inawezekana mtu akachanganya kalamu nyingi na karatasi nyingi kisha ikatokea barua inayosomeka na kukupa taarifa kuwa mkeo uliyemwacha ni akiwa na mimba amejifungua mtoto wa kike jana saa sita kamili ya usiku!!
Cc, mbingunikwetu 👏🏼
Mkuu ninavyojua mimi ni kwamba: Mwongozo wa Ukristo ni Biblia, na humo ndani ya Ukristi kuna madhehebu mengi, na katika Ukristo kugawanyika kwa madhehebu mengi, kila dhehebu limekuwa na tofauti flani ya mafundisho na dhehebu lingine.Kipimo cha kutumia Ili kujua kitabu gani kimesema kweli ni akili yako tu., Yani ukivisoma vitabu hivyo viwili utagundua kipi kimesema kweli na kipi kimeongea uongo na kwenye hivyo vitabu viwili ukiona kitu hakiingii akiilini mfano concept ya utatu ukiona haiingii akilini basi ujue ni Uongo huo.
Injili(Biblia) ilianza kabla ya Qur'an na Qur'an yenyewe inatambua na kuheshimu hilo,..lakini hiyo hiyo Qur'an inasema kwamba Kuna baadhi ya watu waliamua kuuza Maneno ya Mungu kwa thamani ndogo ya maslahi yao kwenye Dunia, wakabadilisha baadhi ya mambo kwenye Hivyo vitabu vya mwanzo(Biblia) kabla ya Qur'an .... Mfano jiulize tu, Je concept ya Utatu mtakatifu imetoka kwa Mungu au watu wamejitungia?
Anhaaa, kwahiyo wewe unaamini theory za Darwin ndiyo zimeelezea asili ya mtu ametokeaje si ndiyo?!Mwili wa Binadamu na nature ya viumbe hai Inaelezeka na evolution and origin of species. Hii mada ishamalizwaga. Ndo maana huwezi ona mtu wa dini anaongelea mwili watu wanaongelea uumbaji wa ulimwengu. Soma kitabu Cha Darwin utaelewa hizo system zote Ni mechanisms za nature.
VyoteUnataka ushahidi wa Nini kati ya haya :-,
1. Mungu yupo/hayupo?
2. Mungu ni Mmoja/ Ni wengi?
Asili ya mtu Mimi sijui na wewe haujui..lakini hayo masystem uliyotaka asili take Ni evolutionary mechanism.Anhaaa, kwahiyo wewe unaamini theory za Darwin ndiyo zimeelezea asili ya mtu ametokeaje si ndiyo?!
Okay, tuelimishe kwa mujibu wa Darwin, Asili ya Mtu ni Nini!?
View attachment 2603768
Creator lazima kiwe kitu kimoja?Upumbavu wa mwanadamu ni pale anapofika mahali akaamini kitu ambacho hata dhamiri yake inamshuhudia kuwa alichoamini ni upumbavu!! Yaani mtu anaamini kuwa mifumo yote ya uhai uliyoiorodhesha na ambayo hujaiorodhesha ilitokea tu kama matokeo ya ajali nzuri ( a good chaotic interactions without any designer). Ni sawa na mtu kuamini kuwa inawezekana mtu akachanganya kalamu nyingi na karatasi nyingi kisha ikatokea barua inayosomeka na kukupa taarifa kuwa mkeo uliyemwacha ni akiwa na mimba amejifungua mtoto wa kike jana saa sita kamili ya usiku!!
Cc, mbingunikwetu [emoji1376]
Nimemaanisha sheria za asili.Acha uwongo Sheria hazifanani. Wengine wanakula nguruwe wengine hawali, wengine wake wanne wengine mmoja, wengine wavae magunia wengine wasivae. Hizi Ni sheria za watu. We unaweza ukakuta mchwa kwenye kichuguu ukawaambia wakuabudu na wafuate sheria zako au utawaunguza. Jua jinsi ulimwengu ulivyokuwa mkubwa sisi Ni Kama bacteria katika ulimwengu... Huyo muumbaji kwani ajali kuhusu bacteria wanajamianaje au wanavaaje.. Ina msaidia Nini yeye
Ngoja nikushauri kitu kuwa open minded.... Kisha itumie akili yako vizuri bila kutumia kitabu chochote wala theory za kina Darwin,Hi inaitwa black and white fallacy kwenye logic. Unanipa option mbili wakati zipo nyingi. Kwani lazma iwe ajali au Mungu. Inaweza kuwa process zingine sio hizo mbili tu.
SimbaMpole123 .......je we unaamini Kuna designer?View attachment 2603766
Iwafikie wale wote wanaopinga uwepo wa THE BEST DESIGNER/THE BEST CREATOR!.,
Human being is a work of art& engineering.... Yani Mtu alivyo tu inaonyesha kuna ufundi ambao umefanya mpaka ukaona mifumo yote kwenye mwili wa binadamu kuanzia:-
1. Respiratory system
2. Digestive system,
3. Circulatory System
4. Nervous System
5. Endocrine system
6. Muscular system
7. Skeletal system
8. Immune system
9. Urinary system
10. Reproductive system.
Yani, Ingetosha kabisa kuangalia mwili wako na jinsi unavyofanya kazi kujua kwamba kuna DESIGNER aliyeweka mifumo yote hiyo., Au kama unahisi mwili wa binadamu na jinsi unavyofanya kazi umejitokeza tu from nowhere, let's conclude that hata robots tunazoziona zimejitokeza tu from nowhere..... Does it make sense?
Pamoja na kuwa umewaza vyema sana kwamba Mungu yupo, umepotea huko kwa akina Eva, Adam nk. We jitahidi tu kuona mambo yalivyo na yakupe mwanga kwamba Mungu yupo ila ukiona unawaza ya akina Eva na Adam wake basi ujue kuwaza kwako hakuko sahihi badoWakuu poleni kwa upambanaji.
Binafsi mimi kuna mda huwa nikitulizaga kichwa changu huwa naanza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu mimi (binadamu) na ulimwengu kiujumla (Universe).
Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani,tumetoka wapi asili yetu, kwanini tupo (dhumuni la kuishi), mwisho wetu ama hatima yetu ni nini, Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.
Hapo juu ni baadhi tu ya maswali ambayo huwa naiuliza sana akili yangu ikiwaga katika hali ya utulivu.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba, katika maswali yote hayo ambayo huwa najiuliza, sijawahi kupata jibu la uhakika kuniridhisha kuhusu hayo maswali yangu.
Nimekuwa nikifanya bidii kubwa sana kupata majibu ya maswali yangu kupitia usomaji wa majarida au vitabu vihusuvyo historia,sayansi, dini na Falsafa lakini kote bado sijapata majibu ya kuniridhisha tofauti na kuambulia majibu ya kinadharia tu ambayo yana strength kiasi chake lakini pia yana weakness sehemu nyingi tu.
Na nikiri wazi tu kuwa katika usomaji wangu wa nadharia hizo zote (historia, sayansi, dini, falsafa) sehemu ambayo nimeanza kuiamini kunipa majibu ya maswali yangu ni kwenye DINI.
Nikiwa na maana nimeanza kuamini kwamba uwepo na sisi tuliohai na visivyo hai hapa ulimwenguni ni matokea ya Uumbaji ya nguvu kubwa sana inayoitwa MUNGU/ALLAH kama ambavyo dini nyingi zinaelezea nguvu hiyo.
Na leo maswali yangu yanajikita huko kwenye hiyo nguvu (Mungu) maana nimeanza kuiamini lakini pia kila nisomapo BIBLIA (mimi mkristo) inanipa maswali chungu nzima.
Sasa leo swali langu limejikita kwenye UKAMILIFU wa MUNGU.
Naombeni wasomaji mnielewe kuwa sina maana ya kukufuru (maana mara nyingi niulizapo maswali kuhusu MUNGU huwa naambiwa nakufuru) bali mimi nataka kujifunza zaidi kumuhusu huyu Mungu.
Dini nyingi (hasa Ukristo na uislamu) zimekuwa zikimwelezea Mungu kuwa ni Mkamilifu sana,mwenye nguvu nyingi sana, uwezo na akili zake hazichunguziki, hashindwi na chochote n.k.
Je hilo lina ukweli ? kupitia Biblia mimi nimeanza kudhani kwamba huenda kweli Mungu ana nguvu nyingi sana ila siyo zote, ana uwezo mkubwa sana ila siyo uwezo wote,ana maarifa mengi sana ila siyo maarifa yote, ana ukamilifu mwingi sana ila siyo ukamilifu wote n.k
Nasema haya ni kutokana na maswali yafuatayo :
1. Kama Mungu ana ukamilifu wote, kwanini sasa alimuumba malaika (Lucifer/shetani) alafu badae akaja kumuasi?
Kama Shetani/Lucifer aliasi maana yake ni kwamba Mungu alimuumba huyu kiumbe akiwa na madhaifu kadhaa na ndiyo maana alishindwa kuitii amri/mamlaka ya muumbaji wake.
Kama Mungu angelikuwa na ukamilifu wote, basi malaika wote wangelikuwa wameumbwa katika namna ya utii pekee, uasi usingetokea na huo uasi unadhihirisha kwamba Mungu aliwaumba hawa malaika wakiwa na udhaifu flani, hawakuwa na uimara wote.
2. Uumbaji wa Eva (Hawa) unaonesha kulikuwa na madhaifu pia.
Katika Biblia takatifu kwenye kitabu cha mwanzo, kuna mistari inaeleza kuwa "Mungu alimpa usingizi mzito Adam, alafu akabandua sehemu ya ubavu wake na kumfanya/kumuumba mwanamke (Hawa/Eva)".
Alafu Mungu akamwambia Adam kuwa huyu mwanamke atakuwa msaidizi wako
Lakini ni huyo huyo mwanamke ambae shetani (kwenye umbo la nyoka) alienda kumdanganya akachukua matunda ya mti walioambiwa asile yeye akala na akampelekea na mumewe (Adam) pia akala.
Lakini Mungu alivyomuuliza Adam kwanini umekula matunda ya mti ambao nilikwambia usile, Adam alijibu kuwa "Ni huyo mwanamke uliyenipa ndiye aliyeniletea nikala".
Tukio hili linadhihirisha kuwa Mungu alimpa Adam msaidizi (Hawa) ambae ni dhaifu sana na ndiyo maana alisababisha dhambi ikaenda hadi kwa Adam.
Na huenda kama Mungu angelikuwa amempa Adam msaidizi imara asiye na madhaifu basi ile dhambi ya kula tunda ingeepukika.
Uko wapi sasa ukamilifu wote wa Mungu ikiwa aliweza kuwaumba malaika dhaifu (ambao walikuja kumuasi) na pia bado akampa Adam msaidizi dhaifu kabisa ambaye alisababisha dhambi imwendee hadi Adam?
Kwa leo naombeni comment zenu zinifunze kuhusu hilo tu (La ukamilifu wa Mungu) alafu mengine nitauliza siku nyingine, na mengine nitakuwa nauliza humo humo kwenye comments zenu.
NB: Naamini Mungu yupo, kutokana na baadhi ya vitu ninavyoviona ulimwenguni (hasa uumbaji/creation) ambapo kuna baadhi ya vitu hasa sayansi inakosa majibu ya kuridhisha, ila shida yangu kubwa ni sifa za Mungu ambazo anapewa na wanadamu naona kama zinashindwa kujidhihirisha kwenye baadhi ya mambo.
Karibuni mnifunze.
Unaweza kuthibitisha hiyo Evolutionary mechanism ilitokeaje mpaka tukapata hizo system?Asili ya mtu Mimi sijui na wewe haujui..lakini hayo masystem uliyotaka asili take Ni evolutionary mechanism.
Zitaje hizi sheria za asili?Nimemaanisha sheria za asili.
Weka sahihi huko kwa Lucifer na EvaPamoja na kuwa umewaza vyema sana kwamba Mungu yupo, umepotea huko kwa akina Eva, Adam nk. We jitahidi tu kuona mambo yalivyo na yakupe mwanga kwamba Mungu yupo ila ukiona unawaza ya akina Eva na Adam wake basi ujue kuwaza kwako hakuko sahihi bado