Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Ni kweli, kila dini ina mungu wake kabisa
 
hahahahah! Ukisema zinabadilika unamuondolea mungu hiyo sifa ya kujua kila kitu. Au hauamini kama kweli anajua kila kitu?
Kwani wewe ukitaka kwenda posta kupitia Morogoro road baadae ukajua kumbe Ali Hassan Mwinyi road hakuna foleni ukaamua kupitia huko, inakuondolea kupajua posta? au kuijua Morogoro road

Samahani kama sio mwenyeji dar kwa huu mfano, utambia niikupe mwingine kama hujaelewa
 
Hapendi mabaya sio wanaofanya mabaya ndio maana tukitubu tunaamini tunasamehewa angekua hatupendi asingetusamehe na asingepatikana asiye na mabaya sababu hatuna ukamilifu ndio maana tumepewa nafasi ya kujutia mabaya na kutubu.
Hayo mabaya kama hayapendi yeye si Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje Kuto kuumba Dunia isiyo na mabaya??

Mabaya ambayo humsababisha mwanadamu ayafanye...
 
mimi nipo mwanza but i've got your point. Mkuu naongelea hatima ya mtu either jehanamu au peponi na kwa mfano wako umeongelea kupajua tu kwa majina na sio kufika au kupapitia


Kumbuka mungu ndio muumba sio tupo under him kabla hajakuumba anajua wewe ni wa jehanamu tu so huwezi change na ikitokea yeye alijua kuwa ni wa jehanamu ila ulipozaliwa ukatumia maombi kama ulivyodai ukaenda peponi hapo tunaiterm kama alikuwa hajui maana yeye kabla haujazaliwa alijua wewe ni wa jehanamu but umebadilisha ukawa wa peponi kwa maamuzi yako but something that's impossible


Hauwezi kuchange hatima anayoijua mungu since he is your designer you can never go beyond his expectations buddy!
 
Okay, swali langu ni hili.... Mtu pamoja na designed systems zote zilizopo kwenye mwili wake kwa ufahamu wako, zina Designer au hazina?
Kwanza unajuaje kwamba uliumbwa?

Kwa nini unadhani uliumbwa na kitu usicho kifahamu na hukijui?

Ukisema designer aliye kuumba wewe yupo ina maana unamjua ulishawahi kumuona.

Lakini hujui kama kweli yupo ila ni imani za watu tu, kwamba yupo.Pia hata kusema hayupo ni sahihi kwa vile ukitaka kudhibitisha ali kuumba huwezi unabaki kukisia.
 
Lakini hamna kitu ambacho binadamu atafanya kinachostahili kuungua milele. Hii adhabu imewekwa na dini ili kuendesha watu. Hazikuwepo katika agano la kale. Ndo maana wanajua kwa hii adhabu wote mtakubali kuendeshwa na wanaosema dini imewafata wao
 
Ndo maana ninakuambia husomi Biblia. Soma story ya Nuhu afu utaona hivi vitu. Wakristo wengi wanakubali dini Yao ya ukweli wakati hawajawahi soma Biblia kiundani. Ni sawa na kusaini mkataba bila kuusoma.
 
Bro. Hii paradox inaitwa paradox of omniscient na freewill. Huwezi sema Mungu anajua kila kitu afu at the same time ukasema binadamu wanamaamuzi.
 
Lakini hamna kitu ambacho binadamu atafanya kinachostahili kuungua milele. Hii adhabu imewekwa na dini ili kuendesha watu. Hazikuwepo katika agano la kale. Ndo maana wanajua kwa hii adhabu wote mtakubali kuendeshwa na wanaosema dini imewafata wao
siamini pia kama kweli kuna huo moto wa milele
 
Bro. Hii paradox inaitwa paradox of omniscient na freewill. Huwezi sema Mungu anajua kila kitu afu at the same time ukasema binadamu wanamaamuzi.
sijasema kuwa binadamu wana maamuzi binadamu hatuna maamuzi ila ni kwa maelezo ya jamaa anayedai kuwa mtu anaweza kuichange kwa kuomba

ila point yangu ni kuwa hatma ambayo mungu anaijua juu ya mtu ni hiyo hiyo mwanadamu hawezi kuichange
 
Designer yupi sasa mkuu?????? Mbona sheria za dini hazifanani.Sheria za Allah ni tofauti na sheria za Yehova na ni tofauti na sheria za Mbakaso
 
Binafisi siamini katika habari za moto wa milele kwamba kuna sehemu roho za binadamu zitachomwa milele.

Hizi habari za mbinguni na motoni ni aina ya reward and punishment system iliyowekwa ili kuleta hofu na kuweza kutawala watu kwa njia nyepesi. Kwamba ukifanya kama tunavyotaka utazawadiwa na ukifanya kinyume basi utaadhibiwa.

Na ili kukamata watu zaidi wakamtengeneza mungu wa kufikirika na kusema yeye ndio mwazilishi wa hayo yote, na kulazisha watu wamuani huyo mungu na kumuacha Mungu wa kweli.

Kwa kifupi Mungu hayupo kama wanavyo muelezea kwenye vitabu vingi vya kiimani.

Kuna mtu aliwahi kuniambia njia nzuri ya kujifunza mambo ya kiimani ni through experience, achana na mambo ya kusoma rundo la vitabu ambavyo vimeyumbishwa na wanadamu kwa maslai binafsi.
 
MUNGU YUPI SASA??????MUNGU WA WAARABU AU MUNGU WA WAYAHUDI AU MUNGU WA WABANTU????????NA VITABU VIPI SASA??????VITABU VYA WAARABU AU WAYAHUDI AU WAHINDU AU WABUDHA????
 
umenena vyema brother!

These stories were just created in the mindsets of ancient people but in real situation they do not exist.
 
Nafikiri kuna baadhi ya biblia za lugha zingine zina vitabu zaidi ya 66,

Tunarudi palepale wewe na adam ni mfano kwa nini unataka ukamilifu usio wako... utashi wako ndio ukamilifu wako... kutenda makosa na kulazishwa kukili na kuomba msamaha kwa maelekezo ya aliyekuumba, kudhibitiwa ukikaidi au kumiminiwa baraka ikimpendeza aliyekuumba ndio ukamilifu wako.. unadai ukamilifu upi ili iweje kwa manufaa ya nani? Anaekumiliki anataka uwe hivyo we unakuja na tuakili twako twa kibinadamu kumpangia almight? Kweli?

Ukijifanya janja janja unakula burn, we mwenyewe Mello akiamua kwa utaratibu wake anakupa ban ya kipindi atakacho na hauna la kumfanya zaidi ya kulalama... unampangia Modurator utaweza kweli? Ukiona unaonewa sana ungana na wasio mwamini Almight uwe na amani moyoni hahahaha. Wapo wakina kilanga and alike.
 
MUNGU YUPI SASA??????MUNGU WA WAARABU AU MUNGU WA WAYAHUDI AU MUNGU WA WABANTU????????NA VITABU VIPI SASA??????VITABU VYA WAARABU AU WAYAHUDI AU WAHINDU AU WABUDHA????
Waarabu, wazungu, Wayahudi na wabantu wote Mungu wao ni mmoja ndio aliyewaumba

Shida ni kwamba Kuna watu miongoni mwa hao hawamjui Mungu wao aliyewaumba
 
Ni maoni yako
Kwasababu ni miungu tofauti, mmoja wapo ndo wa ukweli, .
Kila mwamba ngoma huvutia kwake
 
I bore down and worship my GOD - JEHOVA... kila sekunde na kila saa.. Matendo yake ni ya Ajaabu....
1. Kila mwenye Pumzi na Amsifu BWANA ( Zaburi 150:6)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…