Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Waarabu, wazungu, Wayahudi na wabantu wote Mungu wao ni mmoja ndio aliyewaumba

Shida ni kwamba Kuna watu miongoni mwa hao hawamjui Mungu wao aliyewaumba
Mungu yupi sasa ?????Mbona wana dini tofauti na kila dini ina mungi mwenye utaratibu wa tofauti na mwingine???
 
Ukamilifu ambao mimi nilikuwa nauungumzia ni wa Mungu.

Mungu kaumba viumbe ambao badae walikuja kumuasi, that means kulikuwa na kasoeo
Kwa muktadha wa Biblia ni kana kwamba "Mungu alimuumba mwanadamu na kumpa ufahamu wa kujua mema tu" ila shetani ndiye akamwonesha mwanadamu ubaya mwa kumshawishi ale lile tunda
 
Ingawa Daudi alitimiza mambo mengi, alikuwa mnyenyekevu. Aliimba hivi kumhusu YEHOVA: “Ninapoziona mbingu zako, kazi za vidole vyako, mwezi na nyota ambazo umetayarisha, mwanadamu anayeweza kufa ni nini hivi kwamba umweke akilini, na mwana wa mtu wa udongo hivi kwamba umtunze?” (Zaburi 8:3, 4)
 
Hakuna imani bila dini na hakuna dini bila imani....Lazima ujue definition ya neno imani na definition ya neno dini
Imani ndo huanza.
Kwani Abrahamu alikuwa na dini?
Alikuwa na Imani Wala sio dini, mara ngapi Abraham aliwadanganya Abimeleki na Farao kuwa Sara ni dada yake Ili asiuwawe?
MBONA alimuingilia Hagai bila ya kumuoa?
 
We ni shahidi ?
MAJINA YA MUNGU NA MAANA ZAKE
♢GOD'S NAMES WITH THEIR MEANING

1. ADONAI
=> Mungu Mwenye enzi yote,kimbilio imara Mwa 15:2‐8, Kut 6:2‐3
God of sovereign,strong refuge
2. EL-ELYON
=> Mungu Aliye juu zaidi ‐Mwa14:18, Dan 4:34
Most high God Psa 21:7
3. EL‐GIBBOR
=> Mungu Mwenye Nguvu Isa 9:6, Zab 147:5
(Mighty God )
4.El GMULOT -
=>Mungu alipaye/atoaye ujira
The God of recompense Jer 51:56
5. EL- HAI
-Mungu Aliye Hai/Anaishi ‐Josh 3:10, 1Sam17:26
Living God
6. EL-OHEENU
. =>Bwana Mungu wetu Zab 99:5,8,9
Lord our God Psa 99:5,89
7.EL-OHIM
=> Mungu Muumbaji /Muumbaji wa milele ‐ Mwa33:20, Kol 1:16‐17
8.ELOHIM YISRAEL
=> Mimi ni Bwana Mungu wako
. Iam the lord your God Lev 18:2
9. EL-OLAM
=> Mungu wa Milele ‐ Ufu4:8, Kut 3:14 Mwa 21:23
Everlasting God/Eternal God [ olam means age ]
10. EL-ROI
=> Mungu Aonaye kila kitu ‐Mith 15:3, Zab 32:8
=> BWANA Mchungaji wangu Zab 23:1
The God of sight, The God who keeps watch Gen 16:13
11. EL-SHADDAI
Mungu Mtoshelezi ‐Mdo 17:28, Kumb 8:4
12. JEHOVA EL-ASHIYB
The lord my restorer
Bwana ni mrejeshaji wangu
13.JEHOVAH EL-EMUMAH -
Mungu mwaminifu
Faithful God
14.JEHOVAH EL-GEMU 'AH -
Mungu alipaye/atoaye ujira
The God of recompense Jer 51:56
15.JEHOVAH EL-MAGOWR -
Bwana ni Chemchemi ya maji hair
The fountain of living water Jer 2:13
16. JEHOVAH JIREH/YIR 'EH = (YEHOVA YIRE )
=> Mungu Mtoaji wetu / Bwana atoaye, Mungu wa kweli ‐ Mwa 22: 8, 14
Yahweh provides,true God
17.JEHOVAH MAKEH
=>Bwana huadhibu dhambi Eze 7:9
The lord smites,punishes sin
18. JEHOVAH MEKADDISHEM
=> Bwana Nikutakasaye ‐ Kut 31:13
I the lord sanctity you Ex 31:13
19. JEHOVAH MISGAB
. =>Bwana ni Mwamba wangu na kinara cha wokovu wangu Zab 18:2
Lord is my rock and my tower deliverance Psa 18:2
20. JEHOVAH NISSI = (YEHOVA NISI )
=>Bwana ni Beramu ( Bendera) yetu
=>Mungu Ushindi wetu ‐ Kut 14:13‐14
=> Bwana ni Ishara yetu/ishara ya ushindi wetu
The lord is our banner /essign/sign
21. JEHOVAH RAPHA => (YEHOVA RAFA )
=>Mungu Atuponyaye ‐ Kut 15:26, Mwa 15:26
The lord who heals Ex15:26 Is 53:4
22. JEHOVAH ROHI
=> Bwana ni Mchungaji wangu ‐ Zab 23:1
The lord is my shepherd Psa 23;1
23.JEHOVAH SABAOTH
=> Bwana wa Majeshi (Majeshi ya Malaika )‐ Malaki 3:7 , 1Sam 1:3
The lord of hosts (Angelic armies)
24. JEHOVAH SHALOM =(YEHOVA SHALOM)
=> Mungu ni Amani yetu ‐ Amu 6:22‐24
The lord is our peace - Judges 6Vs22-24
25. JEHOVAH SHAMMA = (YEHOVA SHAMA )
=> Bwana Yupo/Bwana ni Aliyepo Kut 3:14 Eze 48:35
The lord is there/here Eze 48:35
26. JEHOVAH SHAPHAT
=>Bwana ni hukumu yangu Is 22:32
The lord is my judge
27. JEHOVAH TSIDKZEMU
=> Bwana ni Haki yetu ‐ Yer 23:6
The lord is our righteousness Jer 23:6
 
Ni maoni yako
Maoni yako wewe yakoje?

Hakuna imani bila dini na hakuna dini bila imani....Lazima ujue definition ya neno imani na definition ya neno dini
Kuna mambo bado huyaelewi.

Imani haitegemei dini. Dini ni mifumo tu iliyoanzishwa wala haina uhusiano wa moja kwa moja na imani. Kuna watu wapo kwenye dini moja lakini imani zao zimeegemea sehemu nyingine.
 
Wanajmii forum. Kwa uhuru tuliopewA na Mwenyezi Mungu... Allah/ JehovA... naomba tumkemee Mwanzisha Uzi.. kwa kujaribu Kumkashifu.. Mwenyezi Mungu anaetupA Uhai..
1. Dr. Janabi.. Director of MUHAS ( cardiologist) kuna kipindi alihojiwa ITV... alisema sisi Wataalam kuna kipindi tunautoa Moyo wote na kuufanyiA operation.... ila tunakua tunamba Mungu Moyo uendelee kudundA.... GOD miracles...
2. Ben Carson- Katika kitabu chake cha Gifted hands..." If we acknowledge our need for God, he will help us.”
ni mtu aliemwamini Sana Mwenyezi MUNGU... ALLAH/ JEHOVA
 
Hapana, lengo langu ni kujifunza siyo kum-kashfu Mungu
 
Hujajibu swali langu Mkuu,. Mimi nimeuliza hivi⤵️
Mtu pamoja na designed systems zote zilizopo kwenye mwili wake kwa ufahamu wako, zina Designer au hazina?
 
Hujajibu swali langu Mkuu,. Mimi nimeuliza hivi⤵️
Mtu pamoja na designed systems zote zilizopo kwenye mwili wake kwa ufahamu wako, zina Designer au hazina?
Akikujibu mo
Jina la Mungu nalolifahamu ni YHWH, hapo umetaja sifa zake.
 
Mungu yupi sasa ?????Mbona wana dini tofauti na kila dini ina mungi mwenye utaratibu wa tofauti na mwingine???
Mungu ni mmoja na dini ni Moja na manabii wote walifunuliwa Mungu ni mmoja na dini ni Moja

Hi ni orodha ya manabii waliotajwa ndani ya Quran kuwa walifunuliwa Mungu ni mmoja na dini ya kweli ni Moja ( Uislam)

1)Adam
2)Idris
3)Nuh
4)Saleh
5)Shuayb
6)Hud
7)Ibrahim
8)Lut
9)Ismail
10)Is-haq
11)Yaqub
12)Yusuph
13)Yunus
14)Mussa
15)Harun
16)Ayyub
17)Daud
18)Sulayman
19)Ilyas
20)Alyasa
21)Dhul-kifl
22)Zakaria
23)Yahya
24)Issa
25)Muhammad
 
Safi umeanza kupevuka kiakili niseme sio watu wengi hujiuliza kwa undani hivi. Mimi nami katika kujibu maswali ya watu huwajibu kulingana na level yao.

Usitetereke kiimani hata mimi naamini uwepo wa Mungu. Lakini yakupasa kujua kuwa Mungu tunayesoma habari zake vitabuni (Biblia, Quran) sio yule Mungu halisi kwani ameelezewa kulingana na jinsi mtu flani alivyoona, ndio kusema ni vigumu kumwelezea Mungu kwa utimilifu wake kwani kuna tatizo kubwa la kumwelewa Mungu (epistemological problem).

Ni kweli yeye ni mkamilifu na mweza wa vyote ameumba vyote na kuvipa uhuru ikiwa ni pamoja na shetani. Shetani au mwanadamu akitumia uhuru wake kufanya ubaya Mungu hawezi kulaumiwa.

Ubaya au uovu ni jinsi unavyoona wewe tu niseme in absolute terms hakuna kitu kama hicho! Kwani simba akila swala ni uovu? Je simba akila mtu ni uovu! Au mtu akila swala ni uovu? Mtu akila ndizi ni uovu? Na je mtu akila mtu ni uovu?

Ni “hatari “ kutaka kumjua sana Mungu na unatakiwa uwe na uelewa flani wa mambo la sivyo utaishia kuwa hovyo. Nitaachia hapo kwani kujua kunaambatana na majukumu makubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…