Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Story ya Yesu

Mathayo anataja vizazi 26 Kati ya Yesu na Daudi, Luka hutaja vizazi 41. Mathayo anaanza kwa mtoto wa Daudi Solomon, wakati Luka anaanza kwa mtoto wa Daudi Nathan. Mathayo anasema Babu yake Yesu anaitwa Yakobo wakati Luka anasema babu yake Yesu Ni Heli. Cha kushangaza zaidi wamefuatilia vizazi vya Yosefu wakati Hana uhusiano na Yesu Kama kweli kazaliwa kwa bikira Mariam.

Mathayo 2:13-15 inasema Yesu alipelekwa Misri baada ya kuzaliwa. Luka 2:22-40 inasema walibaki Bethlehem, wakaenda Jerusalem na kurudi Nazareth, bila kutaja kwenda Misri.

Kifo Cha Yuda kinasemwa na Mathayo 27:5 kuwa alijinyonga Ila Matendo ya Mitume 1:18 inasema alianguka shambani na akafa.

Yohana 19:17 inatuambia alibeba msalaba wake, Marko 15:21-23 inasema Simoni alimbebea msalaba.
Kila kitabu Cha injili kinasema maneno ya Yesu ya mwisho tofauti Kila injili inachanganya tukio la kufufuka kwa Yesu. Marko 16:2 inasema ilikuwa asubuhi, Yohana 20:1 inasema ilikuwa usiku.

Mathayo 28:2 inasema alionekana malaika mmoja, Yohana 20:11-12 inasema malaika wawili. Marko 16:5 inasema mwanaume mmoja Luka 24:4 inasema wanaume wawili.

Hitimisho: Story ya Yesu inasemekana imeibiwa kutoka dini za kihindi, kipersia, kimisri, kigiriki na kirumi. Miungu yao mingi ilizaliwa December 25, ilizaliwa kutoka kwa Bikira, ilifanya miujiza, ilikufa na kufufuka.

Ina maanisha story ya Yesu sio original na iliundwa na watu tofauti tofauti ndo maana hata vitabu vya dini kuhusu yeye vinajichanganya kuhusu maisha yake yalivyokuwa. Kama ukristo mzima unategemea story hii na Ina makosa kihivi, je Biblia litakuwa neno halisi kutoka kwa Mungu au utunzi wa Binadamu?
 
Kitu kimoja ambacho nimejifunza kupitia hii maada ni kwamba : Kuna ulimwengu wa aina mbili ndani ya mmoja (yaani two in one).

Kuna spiritual world hapa hapa ndani ya dunia na kuna physical world ambayo hii kila mtu anaiona.

Hizo ulimwengu mbili inaonekana zote zinaamini katika destiny tofauti πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Duuh...aisee mkuu uko na NONDO (reference)
 
Spiritual world ndo ipi bana ..hamna hii kitu .kitu ambacho hakiwezekani kuonekana, kunuswa, kusikiwa, kuguswa au kuonjwa...kina tofauti gani na kitu ambacho hakipo. Hizi Ni propaganda tu. Ndo Kama Mimi niseme Nina dragon nyumbani kwangu asiyeonekana. Huwezi kubisha coz utajuaje hayupo ..ndo Mambo spiritual haya..kutishiana tu amani...look the world is very beautiful without this bullshit. Kama unabisha uliza nchi zilizoendelea wakuambia. Hawana mida ya kuondoana mapepo sijui waganga. Wanapata tatizo wanafanya kazi wanasolve..ndo maana wanaendelea.
 
Na mimi naomba kuuliza ni kundi lipi linaabudu Mungu wa kweli kati ya wakristo na waslamu ama pia wachina,wahindu etc kwani kwa namna jinsi hizi dini zilivyo,historia zake,ibada zake na misingi yake haziabudu mungu mmoja kwa lugha rahisi Allah na Mungu wa wakristo ni wawili tofauti?!!

Kwanini iwe hivi?!!
 
Simba
Lakini mkuu tuende mbele turudi nyuma.

Hata hapo kale sana kabla hata Yesu hajazaliwa, kipindi ambacho ulimwengu ulitawaliwa na ustaraabu wa kigiriki.

Kulikuwa na wasomi wa kigiriki ambao ulimwengu bado unawaheshimu mpaka leo.

Mfano kina Socrates,kina Aristotle na kina pilato.

Hawa jamaa kuna wapo walioamini kwenye MATERIALISM (kama hii yako) na kuna wapo walioamini kwenye IDEALISM (kama kina hateeb10 ).

Walioamini kwenye IDEALISM walikuwa wanasema THE SOURCE OF ALL KNOWLEDGE IS FROM GOD (hapa ndipo dini imejikita zaidi nadhani)

Na wale walioamini kwenye MATERIALISM walisema KITU CHOCHOTE AMBACHO HUWEZI KUKIONA,KUKIGUSA,KUKIHISI,KUKIONJA BASI HICHO KITU HAKIPO NA HAKIJAWAHI KUWEPO.

Swali langu kwako, ina maana hao wasomi wakigiriki wa kale ambao waliamini kwenye IDEALISM hizo stori nako kuna mahali walizitoa ? Maana ni kale sana kabla hata ya hivi vitabu vya dini kuwepo wala yesu hajaja duniani bado
 
Coz kila utamaduni umetengeneza njia zake za kuabudu na kujibu maswali ambayo wanashindwa kujibu. Ila with time Sayansi na technology imekuwa to the point that nchi nyingi zilizoendelea hazibishani kuhusu Mungu wa kweli ni yupi coz wanajua wote ni zao la fikra za binadamu wa kale waliokosa maarifa juu ya ulimwengu unavyofanya kazi ndo maana zote Zina makosa ya kihistoria, kimaadili na kisayansi hapa na pale. So wameamua kufocus na vitu tulivyonavo Sasa na kujitahidi kuboresha maisha ya binadamu
 
Kwanini uamini Solar System ni kigezo cha uwepo wa Mungu mkuu?!!

Kwmba hakuna namna nyngne Mungu anaweza kujidhihirisha kiwa yupo?!

What if mimi nikisema iyo nguvu ni shetani sababu nae shetani km anavyotajwa kiwa ndp chanzo cha maovu anaonekana yuko na uwezo mkubwa pia na kashindikana
 
Huyo Mungu mwenyewe huwezi kuthibitisha yupo.

Katika kuamini huyo Mungu yupo umekuwa sawa na hao waamini dini.

Unarudi kule kule unakokukataa.
 
Nimelitolea mfano tu ila viko vingi.

Na mimi sijasema Mungu bali nimesema designer, huyu designer kama ndo itamwita Mungu mimi sijui
 
Na pia labda umesema sababu hufatilii ila kuna objects zina igonga dunia na jua kila siku huko,ko km Mungu ndo anasimamia utaalamu wa solar system bas basi hakuuwekea ukamilifu wa asilimia 100
 
Hii umeiweka vizuri sana,ila ninaomba ufafanuzi hapo uliposema hapo uliposema Majini waliumbwa katika ardhi hii...
 
Huyo jamaa mifano yake ya kitoto sana kwani hakuna mifano ya michezo yenye washindani mmoja mfano tennis
 
Hapa umeunganisha logical non sequitur na argument from incredulity. Both are logical fallacies.

Yani unaona jambo ambalo hulielewi linafanyaje kazi, una conclude lazima itakuwa ni kazi ya Mungu.

Kama huelewi sayari na nyota zinazungukaje, hilo linamaanisha huelewi sayari na nyota zinazungukaje.

Hilo halimaanishi zinazungushwa na Mungu.

Kama huelewi, jifunze uelewe. Usiweke jibu la mkato kwamba hii ni kazi ya Mungu.
 
Hata mimi sijasema zinazungushwa na Mungu bali nimesema zinakuwa controled na DESIGNER huyo designer mimi jina simjui ila yupo katika dhana tu
 
Skia nikwambie
Unaongelea karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa kristo. Jiulize technology Yao ilikuwa level gani, sheria zao zilikuwaje, na hivyo. Kingine mambo ya miungu haijaanza kwenye ukristo sijui uhindi. Umeanza miaka ya kale wakati binadamu ni wawindaji maporini. Issue Ni kwamba mtu anakuwa ana maswali mengi kuhusu ulimwengu ambayo kwa kipindi kile angefikiria Sana na kupoteza mda kuliko kuwaza Mambo ya msingi Kama kusurvive kutoliwa na wanyama wakali na kupata chakula. Hivyo bac..waliaminisha watoto miungu ipo kwenye mapango ambao wazee tu wanaingia ..baadae vijana wakavamia mapango na wakaona ni uwongo tu..wakaja wagiriki wakaweka miungu yao juu ya mlima Olympus lakini watu washapanda milima yote na hamna miungu kule. Waviking wakasema miungu yao ipo sayari jirani ya Asgard. Watu wametembea sayari zote solar system bila kuniona hiyo miungu. Wayahudi wakaja na Yahweh mawinguni..nae wazungu wametengeneza ndege tunavuka mawingu kila siku hatuoni Mungu. Hivyo wakaamua kumficha kabisa na kusema hayupo ulimwenguni. Jiulize why wanamficha, wanamficha ili kuweza kuweka sheria zozote na kusema ni za Mungu coz nani atabisha Sasa, afu wanakupromise zawadi na adhabu baada ya kufa coz wanajua hamna mtu anarudigi kwa hiyo inabidi tu uamini coz unaogopa kitachokukuta usipoamini na hivyo wanaendelea kukucontrol unakuwa mtumwa wa dini Yao. Lakini now nchi zilizoendelea zimegundua huu upuuzi na Sasa zinaishi maisha kuboresha binadamu anavyoishi na sio kushika maadili ya mababu wa jamii fulani huko mbali ambao hawakujua hata Kama dunia ndo inazunguka jua.
In short no spirituality sijui idealism. Sayansi imeshatuonyesha everything ni kwenye ubongo. Ubongo wako ukiharibika huwezi waza huwezi fanya chochote. Hamna Cha roho ni ubongo..na ukifa unaoza.
 
Bro finally humu mtu anaelewa logical fallacies. Coz religions ndo zinatumia Sana hizi..kitu hukielewi Mungu kafanya ukija kuelewa kazi ya Mungu inapungua mpaka mwishowe inaisha. Ndo Mambo ya god of the Gaps...haya watu hawaoni kwamba gaps zimepungua na watu wanazidi kujua why vitu vipo jinsi vilivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…