Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Mkuu una kitu, utafika Mbali sana
 
Malaika hajawahi kupinga amri ya Mungu na aliwaumba hivyo wanafanya wanachomrishwa na Mungu

Aliyepinga kumsujudia Adam ni Jini na Majini wamepewa Freewill kama alivyo Kwa binaadam na Kwa sababu binaadam na Majini wamepewa Freewill ndio maana wamewekewa moto na pepo

Quran 15:26
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.

15:27
Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.

Na sababu ya Ibilisi kukataa kumsujudia Adam ni majivuni yake tu anasema yeye ni Bora Kwa kuwa yeye ameumbwa Kwa moto

Quran 7:12
Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo


Kuhusu Adam na hawa kula tunda waliikazwa pia ni sababu Wana freewill Yani Wana uwezo wa kufanya chocho hata kile ambacho wamekatazwa na Mungu

Binaadam ameumbwa Kwa udongo ana Nafsi na matamanio

Jini ameumbwa Kwa moto ana Nafsi na matamanio

Malaika wameumbwa Kwa Nuru Nafsi wanayo lakini hawana matamanio
 
Swali zuri

Kama sisi Ni wa thamani mbona shetani ?

Ni kweli sisi ni wathamani lakini tu wa thamani na wenye nguvu katika yeye (tukifuata matakwa yake) nje ya hapo were useless rejea hadithi za nuhu na gomola. Aliteketeza kwa sababu hawakua na thamani tena

Pili shetani yupo ili kutu challenge kama kama Mungu alivyoamua mwenyewe kuwa tupitishwe kwenya majaribio makali na watakao shinda ndio wakwake.

Tatu rejea mfano wa baba na watoto wanne katika challenge ya kujificha.

Ndio anawapenda sana ila kaamua kuwapa challenge yeye kama baba.


Hiki kitu tunafanya hata kwenye familia zetu Kuna na wapa hard condition wanangu ili wawe bora zaidi na ngangari japo nawapenda

Karibu
 
So na wewe unaamini dunia nzima ilijaa maji? Kwa elimu yako ya historia na jiografia? Geological records zinaonyesha hii story Ni ya uwongo. Pia wamisri walikuwa wameshaendelea na hamna kipindi ambacho maendeleo Yao yalikatizwa na mafuriko ya dunia nzima. Story hii Ina makosa mengi nikianza kuongelea siwezi Maliza.
 
So na wewe unaamini Kuna majini?
 
Geological records ndo Nini?
 
Geological records ndo Nini?
Utafiti wa kijiolojia. Kuelewa Hali ya kihistoria ya udongo na mawe duniani. Wanaweza jua kwa kutafiti Kama sehemu fulani mda fulani kulitokea kitu fulani Kama Ni mafuriko tetemeko au mmomonyoko. In short hamna evidence ya dunia nzima kujaa maji na hiki kitu hakiwezekani kifizikia na kibiolojia
 
Ngoja kwanza wapi huko pamesema malaika hana utashi.

Kabla sijaendelea
 
Utafiti huo ni timilifu kwa asilmia ngap?
 
Utafiti huo ni timilifu kwa asilmia ngap?
Fatilia wewe Sasa.. kwa akili za mtu mzima ipi rahisi kuaminika dunia nzima kujaa maji au hizo tafiti. Haya wanyama wote wameeneaje kwenye lile boat. Na dunia kujaa maji kufunika milima inamaanisha watakuwa katika high altitude wanyama na watu wote wangekufa kwa baridi na pressure. Mwisho wa siku hii story ipo kwa wahindi na wamesapotamia na zimeandikwa zamani Sana inamaanisha imeibiwa. So inaonyesha iliandikwa na watu ambao hawana ujuzi wa dunia ndo maana Ina makosa mengi. Kasome the Epic of Gilgamesh (moja wapo wa hizi story za mafuriko..karibia kila dini inayo yake)
 
Maswali kama sisi (binadamu) ni kina nani
Kwa kawaida wengi hudhani ni huo mwili lakini sio kweli. Kwa wakristo ukisoma mwanadamu alivyoumbwa utajua wewe ni nani. Soma kitabu cha Mwanzo kwenye uumbaji



tumetoka wapi asili yetu,
Asili yetu ni Mungu mwenyewe na ni kama ilivyo asili ya kila unachokiona. Ila mwanadamu akapendelewa kwa kuwa na mfano wa asili yake yaani Mungu.

kwanini tupo (dhumuni la kuishi),
Dhumuni ni kuwakilisha uwepo wa Mungu duniani na kuitawala dunia na vyote viijazavyo. Lakini tumesahau dunia inatawala wanadamu. Ukielewa maana ya utawala utatawala kila eneo la maisha yako.
mwisho wetu ama hatima yetu ni nini,
Ni kutawala pamoja na Mungu milele. Mungu alishatukomboa tulikojichuuza. Kwa vile tuna utashi huru ni jukumu la mateka kuondoka utumwani au kubakia ikiwa umezoea utumwa. Mlango uko wazi yaani Neema.
Ulimwengu wa vitu je kama sayari, nyota, galaxies zimekuwepo vipi na nini hasa mwisho wake.
Ni kwa namna ile ile ulimwengu wetu umepatikana.
.
 
Tunapo ongelea Mungu maana yake tunazungumzia muweza wa yote.

Kama aliweza kufufua wafu anashidwaje kuwafanya viumbe waishi kwenye anga za juu

Japo haikusemwa Ni futi ngapi above

Pia Mimi siamini 100% wataalamu walioshindwa hata kutabili mvua kiusahihi


Karibu
 
Mi nilidhani unataka kuuliza kwanini kuna watu wanaishi maisha yaliyonyooka na wengine tunataabika
Ni uchaguzi. Hicho ulichonacho ndicho uliomba kwa Mungu.

Kumbuka kuomba sio kupayuka na kukesha makanisani ukisali.
 
Lakini kabla hiyo imani ya Mungu mpya kuletwa, historia inaonesha kuwa Mababu zetu (Waafrica Weusi) walikuwa na imani zao kabla hata hizo za Mungu mpya kuletwa.
Lakini nguvu inayotenda kazi ni moja tu kwa imani yoyote. Ni Mungu muumba.

Umaweza ukawa na imani yako leo na ukapokea nguvu ya Mungu yuleyule muumba.

Ni somo refu na pana lakini ukweli ndip huo. Hata mchawi anaenda kwa nguvu ileile ya Muumba. Ndio maana kwa mawazo maovu ya wanadamu kuna maarifa Mungu amewafungia wanadamu.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…