Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Naamini Mungu yupo ila nashindwa kuuelewa ukamilifu wake, labda muendelee kunifunza

Roman empire ipo wapi...Paulo ni mtu wa wapi.. hebu kuwa na data bac wayahudi ni Old testament mpaka gospels bac. Baada ya hapo ni Paul preaching all over Europe na Asia. Na John of Patmos ambae ni Greek.
Hivi hujui kuwa wayahudi walitawanyika mataifa mbali mbali na ndo maan siku ya pentecoste walinena kwa lugha za kigeni wale waliokuwa Yerusalem na Yesu. Paul ni myahudi aliezaliwa Roma haimfanyi kutokuwa myahudi.
 
Trump alivokuwa madarakani alisema mwaka 2020 atawarudisha wamarekani mwezini, lakini mpaka ametoka madarakani hakufanya.

NASA wenyewe wakaja wakasema wamesogeza mbele from 2020 to 2022 kwa sababu mambo flani flani ya kiufundi hayajaenda sawa lakini bado 2022 hawakufanya tena.

Wakaja wakasogeza tena hadi 2024, ndo tunasubiri wakifanya kweli basi tutaamini 1969 walienda siyo maigizo.

Ila wasipofanya, tutaanza kuamini huko nyuma walikuwa wanafanya HOLY WOOD.
Sure mkuu ile story ina ukakasi sana details nyingi haziko clear ngoj tuone kama itatokea hyo 2024 hawa jmaa wanadanganya ulimwengu kwa malengo mabaya sana watu hawajui tu.
 
Pyramidi walijenga wayahudi kipindi cha kutawaliwa au unabisha kuwa wayahudi hawajatawaliwa na misri tuanzie hapo
Nnavyojua mimi, dhana ya Ma-piramidi ya misri kujengwa na wayahudi kipindi cha utumwa wao wa miaka 430, hiyo dhana huwa wanayo zaidi ma-westerners kwa sababu huwa hawataki kabisa kukubali kuhusu civilization yoyote kuwepo Africa before colonial Era.

Na wazungu wengine wakaenda mbali zaidi wakasema yale ma-piramidi yalijengwa na ALLIENS na siyo watu (ELON MUSK ni miongoni mwa wanaoamini katika dhana hiyo).

Lakini wamisri wenyewe kwa historia yao wanasema hayo mapiramidi waliyajenga wenyewe kwa technolojia yao wenyewe hakuna cha Wayahudi wala ALIENS.

Ila ulimwengu wa mgharibi hukataa hilo kujengwa na wamisri wenyewe kwa sababu hawataki Africa kuonekane kulikuwa na civilization kabla yao .
 
Sure mkuu ile story ina ukakasi sana details nyingi haziko clear ngoj tuone kama itatokea hyo 2024 hawa jmaa wanadanganya ulimwengu kwa malengo mabaya sana watu hawajui tu.
Yeah, na ukizingatia hayo mambo yalifanyika kipindi cha vita baridi, ambako mambo mengi sana yalikuwa yanaghushiwa kuliko uhalisia wenyewe ili tu upande mmoja uonekane uko mbele ya mwenzake.
 
Nnavyojua mimi, dhana ya Ma-piramidi ya misri kujengwa na wayahudi kipindi cha utumwa wao wa miaka 430, hiyo dhana huwa wanayo zaidi ma-westerners kwa sababu huwa hawataki kabisa kukubali kuhusu civilization yoyote kuwepo Africa before colonial Era.

Na wazungu wengine wakaenda mbali zaidi wakasema yale ma-piramidi yalijengwa na ALLIENS na siyo watu (ELON MUSK ni miongoni mwa wanaoamini katika dhana hiyo).

Lakini wamisri wenyewe kwa historia yao wanasema hayo mapiramidi waliyajenga wenyewe kwa technolojia yao wenyewe hakuna cha Wayahudi wala ALIENS.

Ila ulimwengu wa mgharibi hukataa hilo kujengwa na wamisri wenyewe kwa sababu hawataki Africa kuonekane kulikuwa na civilization kabla yao .
Sasa wayahudi kumbuka ni watumwa wa hao westerners walitawaliwa na kunyanyaswa kwahyo kwanini wakuzwe. Halafu mzee dunia inajidhihirisha yenyew tunaona wayahudi bado wanafanya maajabu ya kisayansi. Hivi unjua jamaa walikuwa normal sana katika jamii watu kama akina einstein walikuwa hawana kitu ila wanafanya mapinduzi.
 
Sasa wayahudi kumbuka ni watumwa wa hao westerners walitawaliwa na kunyanyaswa kwahyo kwanini wakuzwe. Halafu mzee dunia inajidhihirisha yenyew tunaona wayahudi bado wanafanya maajabu ya kisayansi. Hivi unjua jamaa walikuwa normal sana katika jamii watu kama akina einstein walikuwa hawana kitu ila wanafanya mapinduzi..
Unajua haya mambo bhan yanahitaji fikra pevu kidogo.

Kwanza Inabidi uelewe kwamba unapozungumzia HISTORY OF AFRICA lazima ujikite kama dhana mbili ambazo ni :

1.Afro-centric view na

2.Euro-centric view.

Afro-centric view ndiyo inayosemaga ukweli halisi kuhusu historia ya africa na kwa kiasi kikubwa imeandikwa na wanahistoria weusi (waafrica wenyewe).

Lakini Euro-Centric view hawa ni wapotoshaji kwa kiasi kikubwa, wameandika uzushi na uwongo wa kutupa na kuikandia Africa, na waandishi wake ni wazungu.

Naweza kupa mfano mmoja thabiti : Wanahistoria wa kizungu (Euro-centric) wameandika kuwa sababu kubwa zilizowafanya wao waje kututawala africa (yaani ukoloni) ilikuwa ni kuja kutuletea ustaarabu kwa maana Africa ilikuwa ni kama bara la giza halijui chochote wala kujishughulishi na chochote watu wake wapo wapo tu kama wanyama,eti walikuja kutuletea dini tuachane na uchawi, eti walikuja kukomesha biashara ya utumwa.

Tena kuna mpuuzi mmoja wa kizungu kaenda mbali zaidi katutusi akasema "Africans were an animal men who were living in the Forest".

Lakini ki-uhalisia huo wote ni uwongo tu wa wazungu ku-maintain superiority yao.

Hapo ndipo walipokuja wenye mtazamo wa AFRO-CENTRIC VIEW kuja kusahihisha uwongo na uzushi huo.

Afro-centric wakasema: Africa kabla ya kuja kwa wazungu halikuwa bara la giza (dark continent) lisilojua chochote kama wazungu wanavyosema, bali tulikuwa na maendeleo yetu kwa kiasi chake hata kama ulaya walituzidi ila ilikuwa kidogo tu.

Wakasema sisi waafrica tulikuwa tuna elimu yetu (informal education), tulikuwa tunalima, tunafanya biashara (goods by goods), tulikuwa na mifumo yetu ya kiutawala na kisiasa mfano MKWAWA KINGDOM chini ya CHIEF MKWAWA ambae aliwahi kuwatembezea kichapo wajerumani vizuri tu n.k.

Na pia Afro-centric wakasahihisha kwa kusema kuwa sababu zilizowafanya wazungu kuja Africa siyo kuja kuleta ustaarabu wala dini au kukomesha biashara ya utumwa, bali walikuja kwa ajili ya kutafta malighafi kwa ajili ya viwanda vyao vya ulaya, mahali ambapo wangepata cheap labour, mahali ambao wangepata maeneo kwa ajili ya uzalishaji wao wa ziada (surplus production) na pia maeneo kwa ajili ya wao kuishi maana waliona kama ulaya wameanza kubanana (kuwa wengi).

HIvyo basi sitaki kukubishia kuwa "Ma-piramidi ya Egpty hayajajengwa na wayahudi" ila nataka nikusanue kuwa, kuwa makini na wasomi wa kimagharibi, mara nyingi huwa hawasemi ukweli kuhusu Africa kwa sababu ya wao kutaka kujiona ni superio muda wote, hawataki kabisa kuona kama waafrica tuliwahi kuwazidi kwa chochote.

Na ndiyo maana wanasema hayo mapiramidi yamejengwa na wayahudi waliokuwa utumwani misri au viumbe Aliens, lakini wamisri wanasema hiyo ni kazi yao wenyewe.

NB: Soma kitabu kinaitwa "HOW EUROPE UNDER DEVELOPED AFEICA" kimeandikwa na Walter Roodney mwaka 1973.

Humo ndani kawavua nguo wazungu balaa hadi ikabidi wamuue (assination).
 
Sasa wayahudi kumbuka ni watumwa wa hao westerners walitawaliwa na kunyanyaswa kwahyo kwanini wakuzwe. Halafu mzee dunia inajidhihirisha yenyew tunaona wayahudi bado wanafanya maajabu ya kisayansi. Hivi unjua jamaa walikuwa normal sana katika jamii watu kama akina einstein walikuwa hawana kitu ila wanafanya mapinduzi.
Alafu kitu kingine, mimi sikatai kuwa wayahudi ni wabunifu.

Ila nikupe mtihani mmoja, alafu huo mtihani nijibu bila kuingiza mambo ya dini humu.

Mtihani wenyewe ni huu : Ikiwa wayahudi ni wabunifu toka enzi za zamani, llikuwaje walishindwa kutumia ubunifu wao kuilinda nchi yao mpaka wakawa wanatekwa hovyo na kuchukuliwa watumwa ?

Tangu zamani JEWISH KINGDOM ambako ndiko ilikuwa nyumbani kwa wayahudi, taifa lao lilipitia vipindi mbali mbali vya kutekwa.

Ilianza Babilon Kingdom (Iraq ya leo ) ikaipiga Jewish Kingdom na kuiteka kwa miaka, badae ikaja Pursian(Iran ya leo) ikawateka na kuwatawala vya kutosha,badae ikaja Dola ya Uyunani (Ugiriki) chini mwamba Alexender THE GREAT akawaburuta vya kutosha pia, ikaja ROMAN EMPIRE pia ikawaburuza kwa mamia ya miaka mpaka kipindi cha Yesu, badae wakaja kumalizia OTTO MAN EMPIRE (Uturuki ya leo) nao wakawatawala na kuwatawanywa vya kutosha.

So,.can you tell me ubunifu wao wakati wote ulikuwa wapi washindwe kuutumia kuilinda nchi yao dhidi ya maadui kama wanavyofanya laeo.

Nijibu please bila kutumia muktadha wa dini, maana ukitumia muktadha wa dini utanambia ilikuwa ni mpango wa Mungu wao kuteseka na kupelekwa utumwani
 
Sasa wayahudi kumbuka ni watumwa wa hao westerners walitawaliwa na kunyanyaswa kwahyo kwanini wakuzwe. Halafu mzee dunia inajidhihirisha yenyew tunaona wayahudi bado wanafanya maajabu ya kisayansi. Hivi unjua jamaa walikuwa normal sana katika jamii watu kama akina einstein walikuwa hawana kitu ila wanafanya mapinduzi.
Alafu kitu kingine, mimi sikatai kuwa wayahudi ni wabunifu.

Ila nikupe mfano mtihani mmoja, alafu huo mtihani nijibu bila kuingiza mambo ya dini humu.

Mtihani wenyewe ni huu : Ikiwa wayahudi ni wabunifu toka enzi za zamani, llikuwaje walishindwa kutumia ubunifu wao kuilinda nchi yao mpaka wakawa wanatekwa hovyo na kuchukuliwa watumwa ?

Tangu zamani JEWISH KINGDOM ambako ndiko ilikuwa nyumbani kwa wayahudi, taifa lao lilipitia vipindi mbali mbali vya kutekwa.

Ilianza Babilon Kingdom (Iraq ya leo ) ikaipiga Jewish Kingdom na kuiteka kwa miaka, badae ikaja Pursian(Iran ya leo) ikawateka na kuwatawala vya kutosha,badae ikaja Dola ya Uyunani (Ugiriki) chini mwamba Alexender THE GREAT akawaburuta vya kutosha pia, ikaja ROMAN EMPIRE pia ikawaburuza kwa mamia ya miaka mpaka kipindi cha Yesu, badae wakaja kumalizia OTTO MAN EMPIRE (Uturuki ya leo) nao wakawatawala na kuwatawanywa vya kutosha.

So,.can you tell me ubunifu wao wakati wote ulikuwa wapi washindwe kuutumia kuilinda nchi yao dhidi ya maadui kama wanavyofanya laeo.

Nijibu please bila kutumia muktadha wa dini, maana ukitumia muktadha wa dini utanambia ilikuwa ni mpango wa Mungu wao kuteseka na kupekwa utumwani
 
Wewe muafrica kwann kabla ya kuja hyo dini usiwe na technlogy yako. Halafu hizo story za mwezini mbona nyingi tu ni za kutunga. Halafu alokwambia mbingu ipo hapo unapohisi wewe ni nani? Mungu anaishi nje ya upeo wa wanadamu. Wewe mwafrica sayansi nd kifo chako cha kwanza umepew smartphone ya kubishana jamii forums.
Kwahio mwezi haupo? Au mwezi upoje... em elezea umachomaanisha ukisema kua story za mwezini ni za kutunga
 
Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    14.1 KB · Views: 7
Trump alivokuwa madarakani alisema mwaka 2020 atawarudisha wamarekani mwezini, lakini mpaka ametoka madarakani hakufanya.

NASA wenyewe wakaja wakasema wamesogeza mbele from 2020 to 2022 kwa sababu mambo flani flani ya kiufundi hayajaenda sawa lakini bado 2022 hawakufanya tena.

Wakaja wakasogeza tena hadi 2024, ndo tunasubiri wakifanya kweli basi tutaamini 1969 walienda siyo maigizo.

Ila wasipofanya, tutaanza kuamini huko nyuma walikuwa wanafanya HOLY WOOD.
Hapana asee... NASA haijasema kua wanampango wa kurudisha watu mwezini. Ninachokumbuka ni kua walisema kua hawana mpango wa kurudisha watu mwezini kwa sababu ya gharama. Inagharimu pesa nyingi sana na hakuna umuhimu wa kupeleka binadamu mwezini na ni risk kubwa. Kama ni utafiti unaweza kutuma vifaa vikatafiti vizuri tu bila kupeleka binadamu. Unajua China ndio ilikua nchi ya kwanza kupeleka vifaa kwenye far side ya mwezini?

Kama hujui, kuna billionea (Jeff Bezos nafkir) alikua na mpango wa kupeleka watu mwezini kama watalii.. unalipia, unapewa tiket afu unapelekwa mwezini.
 
Data za 2004... [emoji2365]
Ila still, Japan ni mostly atheist nation na ndio miongoni mwa nchi zenye amani zaidi. Hii pamoja na nchi zingine zenye majority ya atheists ndio proof kua hauhitaji mungu/miungu kua na amani. Pia 'shit hole' countries nyingi ukiangalia ni nchi zenye dini sana.
 
Mkuu wewe unaishi lini ?

Unaishi juzi,jana,leo au kesho ?

Kuwa current, ndiyo maana unasema unakumbuka ila hujui nini kiliendelea baada ya kutokukumbuka.

NASA siyo shirika la kibinafsi bali ni shirika la serikali ya marekani, Rais wa marekani akisema maana yake watekelezaji ni NASA na wala hawana mamlaka ya kusema bajeti ni kubwa maana bajeti wanapewa na serikali.

NASA wanajiandaa kurudi mwezini 2024 na gharama bajeti ya safari hiyo ni dolar bilion 28, na tayari rocket sasahivi inafanyiwa majaribio na Kampuni ya SPACE X ya Elon Musk ndiyo imepewa Zabuni ya kutengeneza rocket hiyo.

Hiyo rocket inaitwa ARTEMIS -1 na juzi tu hapa imetestiwa ikalipuka kwa hiyo bado mambo ya kiufundi hayajakaa sawa kwa asilimia zote, na usishangae walaja kusogeza tena mbele.

Na timu ya wana sayansi wa NASA watakaoenda mwezini kwenye hiyo safari tayari ishatajwa ina wana sayansi kama watano nadhani (mwanamke mmoja) na tayari sasahivi washaanza kupigishwa mazoezi ya kwenda kuwa adapt mazingira
 
Una uhakika ni za 2004 mkuu ?
 
NASA ni shirika la serikali, nalitambua hilo. Na nawafuatilia kwa ukaribu sana. Hivi unajua kua NASA haihusiki na mambo ya space pekee...? Kwa kias kikubwa imefocus ktk aeronautics na sio kwenda mwezini...

Ila anyway, tamko la recent kutoka NASA hawaja confirm kua watapeleka binadamu mwezini. Sababu kubwa ni gharama. Inagharimu pesa nyingi kupeleka watu mwezini wakat unaweza kupeleka vifaa tu na vikafanya kazi kubwa kuliko binadamu anavoweza kufanya, ni low cost na safer. Kwa ufupi hakuna umuhimu wa kupeleka binadamu mwezini!
 
Nijaribu kukujibu. Kabla sijafanya hivyo nitoe angalizo kwamba maswali juu ya Mungu hayana empirical answers, isipokuwa logical answers. Ukilazimisha logical iwe empirical na kinyume chake basi ni vyema ukaacha kuamini uwapo wa Mungu na nguvu zake.

Swali lako juu ya shetani na nguvu zake: Uwapo wa shetani ndio unaodhihirisha uwapo wa Mungu, bila usiku mchana haupo, bila kulia kushoto hakutakuwapo. Bila adhabu zawadi haina maana. Kadhalika Mungu aliumba hao malaika, na moja akasaliti Mungu akamfanya awe adhabu ya milele itakayotofautisha walio wake na wasio wake. Ni kwa nguvu zake Mungu alimfanya Lucifer awe shetani, yaani nguvu kinzani. Na mara nyingi Mungu ameonyesha ushindi dhidi ya shetani. Ungeuliza pia kwanini Mungu anayesamehe kila Jambo hakumsamehe shetani, jibu ni hilo hapo juu: lazima kuwe na usiku ili tuujue mchana. Lazima kuwe na wovu tuujuwe wema. The two are separable but interdependent.

Swali kwamba Mungu alimpa Adam msaidizi dhahifu hadi akashawishiwa na nyoka kula tunda katazwa.

Ndugu, kwani aliyekuambia kwamba Adamu hakuwa dhahifu Nani? Unadhani Adamu alisamehewa dhambi kwasababu alipewa tu lile tunda? Wote walikuwa dhahifu na Mungu alijuwa hilo ndio maana akawaonya wasile tunda walilokatazwa. Yaani binadamu wote ni dhaifu tangu kuumbwa, kumbuka Mungu hakuumba binadamu kama malaika. Hata Yesu aliyeshuka kwa baba akavaa ubinadamu naye alikuwa dhahifu na akakili udhahifu wake mbele ya mitume wake.
Haya sio majibu ya Logic, hakuna logic bila reasoning na endapo uta reason tu mambo ya Imani utagundua kuwa huwezi kutoa majibu ya maana

Ni kwenye issue moja tu ndio binadamu wote waga wanafanana Akili haijarishi wana level gani ya Elimu, wametokea wapi,wamekulia wapi ni kwenye issue za DINI

Uongee na ambae hajasoma kabisa formal education,awe ameishia st 7,awe ni form four,awe ni Advance awe ni chuo kikuu wote awe professor wote wanakuwa katika level moja ya uelewa

Uwezo wa Ku reason unakuwa sawa kwa sababu muda huo kinachowaendesha ni hisia za uoga na Tamaa ya ku satisfy Desire walizonazo katika Maisha

Kwa lugha nyepesi vile Mungu anatuona Sisi ni kama vile tuwaonavyo watoto wadogo ambao bado hawana utambuzi, mtoto ambae popote alipo kuna 80% akafanya kitu ambacho hatakiwi kufanya

Kwa maana hiyo Mungu alijua fika kuwa Adamu atakula tunda alilowakataza, ila akaacha tu wale kwakuwa aliwaambia wasile, Alafu ili iweje?

Yani mfano una mtoto mdogo sehemu anayocheza kuna Bomu la kuzikwa Ardhini, wewe kama mzazi unapaswa kumwambia usicheze hapo kuna mabomu yalizikwa yanaweza kukulipukia au unapswa kuondoa Bomu kabisa hapo ili uhakikishe mtoto anakuwa sehemu salama?

Ukiamucha aendelee kucheza sehemu ya hatari na Bomu likamlipukia, ukaja kuulizwa ilikuaje ukamuacha hapo utajibu kuwa nilimpa options either aendelee kucheza hapo au aondoke ila yeye akaamua kuendelea kucheza hapo, hilo ni jibu la Logic au utaonekana Akili haziko sawa?
 
Back
Top Bottom