Sasa wayahudi kumbuka ni watumwa wa hao westerners walitawaliwa na kunyanyaswa kwahyo kwanini wakuzwe. Halafu mzee dunia inajidhihirisha yenyew tunaona wayahudi bado wanafanya maajabu ya kisayansi. Hivi unjua jamaa walikuwa normal sana katika jamii watu kama akina einstein walikuwa hawana kitu ila wanafanya mapinduzi..
Unajua haya mambo bhan yanahitaji fikra pevu kidogo.
Kwanza Inabidi uelewe kwamba unapozungumzia HISTORY OF AFRICA lazima ujikite kama dhana mbili ambazo ni :
1.Afro-centric view na
2.Euro-centric view.
Afro-centric view ndiyo inayosemaga ukweli halisi kuhusu historia ya africa na kwa kiasi kikubwa imeandikwa na wanahistoria weusi (waafrica wenyewe).
Lakini Euro-Centric view hawa ni wapotoshaji kwa kiasi kikubwa, wameandika uzushi na uwongo wa kutupa na kuikandia Africa, na waandishi wake ni wazungu.
Naweza kupa mfano mmoja thabiti : Wanahistoria wa kizungu (Euro-centric) wameandika kuwa sababu kubwa zilizowafanya wao waje kututawala africa (yaani ukoloni) ilikuwa ni kuja kutuletea ustaarabu kwa maana Africa ilikuwa ni kama bara la giza halijui chochote wala kujishughulishi na chochote watu wake wapo wapo tu kama wanyama,eti walikuja kutuletea dini tuachane na uchawi, eti walikuja kukomesha biashara ya utumwa.
Tena kuna mpuuzi mmoja wa kizungu kaenda mbali zaidi katutusi akasema "Africans were an animal men who were living in the Forest".
Lakini ki-uhalisia huo wote ni uwongo tu wa wazungu ku-maintain superiority yao.
Hapo ndipo walipokuja wenye mtazamo wa AFRO-CENTRIC VIEW kuja kusahihisha uwongo na uzushi huo.
Afro-centric wakasema: Africa kabla ya kuja kwa wazungu halikuwa bara la giza (dark continent) lisilojua chochote kama wazungu wanavyosema, bali tulikuwa na maendeleo yetu kwa kiasi chake hata kama ulaya walituzidi ila ilikuwa kidogo tu.
Wakasema sisi waafrica tulikuwa tuna elimu yetu (informal education), tulikuwa tunalima, tunafanya biashara (goods by goods), tulikuwa na mifumo yetu ya kiutawala na kisiasa mfano MKWAWA KINGDOM chini ya CHIEF MKWAWA ambae aliwahi kuwatembezea kichapo wajerumani vizuri tu n.k.
Na pia Afro-centric wakasahihisha kwa kusema kuwa sababu zilizowafanya wazungu kuja Africa siyo kuja kuleta ustaarabu wala dini au kukomesha biashara ya utumwa, bali walikuja kwa ajili ya kutafta malighafi kwa ajili ya viwanda vyao vya ulaya, mahali ambapo wangepata cheap labour, mahali ambao wangepata maeneo kwa ajili ya uzalishaji wao wa ziada (surplus production) na pia maeneo kwa ajili ya wao kuishi maana waliona kama ulaya wameanza kubanana (kuwa wengi).
HIvyo basi sitaki kukubishia kuwa "Ma-piramidi ya Egpty hayajajengwa na wayahudi" ila nataka nikusanue kuwa, kuwa makini na wasomi wa kimagharibi, mara nyingi huwa hawasemi ukweli kuhusu Africa kwa sababu ya wao kutaka kujiona ni superio muda wote, hawataki kabisa kuona kama waafrica tuliwahi kuwazidi kwa chochote.
Na ndiyo maana wanasema hayo mapiramidi yamejengwa na wayahudi waliokuwa utumwani misri au viumbe Aliens, lakini wamisri wanasema hiyo ni kazi yao wenyewe.
NB: Soma kitabu kinaitwa "HOW EUROPE UNDER DEVELOPED AFEICA" kimeandikwa na Walter Roodney mwaka 1973.
Humo ndani kawavua nguo wazungu balaa hadi ikabidi wamuue (assination).