Urais ni taasisi. Rais ni mkuu wa taasisi hiyo. Kiutendaji,Rais hutenda au kuamua baada ya kushauriwa au kushauriana na Washauri wake. Wapo Washauri wa kila sekta imhusuyo Rais.
Wapo Washauri wa kisheria,kiuchumi,kisiasa na hata kiutamaduni. Taasisi ya Urais imekamilika kila idara. Tangu kuanza utumbuaji,imekuwa ikijitokeza hali ya Washauri wa Rais kuwa 'wachonganishi' badala ya 'washauri'.
Mara baada ya utumbuaji,hudhihirika kuwa sababu zinazoelezwa na Rais katika kutumbua huwa ni tofauti na zile halisi. Nataja mifano ya utumbuaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,Maafisa kadhaa wa TAKUKURU na hata Bodi ya TRA.
Je,Rais hujazwa hasira badala ya kushauriwa katika kuelekea kutumbua? Je,Rais wetu mpendwa amezungukwa na 'Washauri' au 'Wachonganishi'? Tatizo hasa ni nini?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam