Suala siyo nani anakufa na ugonjwa huo ndo iwe suala msingi kwa jamii yake tu. Watu na jumuiya za kimataifa na nchi zote wanaangalia haya magonjwa kwa mtizamo mtambuka, kuna magonjwa ambayo anapotokea mgonjwa mmoja tu, ni tishio kidunia. Ndo maana nimekwambia soma kwa nini nchi zote wanachama wa WHO wanasimamiwa na International Health Regulations (IHR)?. Utaelewa kwa nini Ebola si tatizo kwa nchi yenye mgonjwa tu.
Hii inatokana na umuhimu uliowekwa kwa magonjwa husika/yenye sifa tajwa). Ni kwa sababu inaweza kutatiza maendeleo ya dunia: kibiashara, uchumi, usalama na usafiri duniani. Na gharama za kuuzuia ugonjwa usisambae na kutibu ni kubwa kuliko kinga. Wewe unaona hii si shida kwa dunia?