Ndugu mwambie nduguyo kuwa, usalama wake ni kwa Mungu pekee muumba wa mbingu na nchi
Sharti la Mungu kumpokea yeyote na kumfanya wake tena ukiwemo wewe
nyakubonga huwa ni moja tu na ni rahisi kabisa. Ni kubali tu kuwa ulikosea, umetenda dhambi kwa kuumiza watu wengine. Hii kwa kifupi huitwa TOBA.!
Ndugu
nyakubonga mzigo wa dhambi ni mzito mno, haubebeki isipokuwa kuupeleka kwa anayeweza kukusaidia na ni mmoja tu, YESU KRISTO pekee yake, maana anasema👇🏻👇🏻
Mathayo 11:28-30 SUV
"....Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi..."
Akishindwa kuelewa hilo☝🏻☝🏻☝🏻afahamu moja tu kuwa, mlipiza kisasi (ambaye ni Mungu mwenyewe) yupo kazini na atamtumia yeyote ili mradi kila mtu apokee malipo ya kazi ya mikono yake. Inawezekana hunielewi ila kwenye hili Mungu mwenyewe anasema hivi kwa uwazi kabisa👇🏻👇🏻👇🏻