Naandika nikijua hasa nini kinaendelea. Makonda fanya haya usidhurike

Noma sana!
 
Makonda bado hajajifunza ukisoma alichokiandika ni kama bado anaamini yeye ni untouchable na bado ananguvu sana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kijana ameshachelewa, alikosa washauri na bado hana washauri.... Aliamini baada ya kifo cha mzee ndugu zake kutoka nyumbani wangeshika usukani, wakafeli na usukani ukaangukia kwa wenyewe...

Wakajaribu kumtisha mama awaogope na kuwasikiliza wakiamini atakuwa anawaogopa kwa uongo wa kumtishia kiti chake na influence ya ukanda, Mama chini ya Wasaigon na Chalinze akawa strong akilindwa na wenyewe...

Vijana wa mjini wameachiwa wamkung'utishe kimyakimya kimtaamtaa kama yeye alivyokuwa akideal nao gizani, nao sasa wanamalizana naye gizani.....kwa sasa yupo kizuizini Dar es salaam.

Kosa la ndugu zetu wa kanda ile, walijioverestimate na kushindwa kufanya proper calculation ya mifumo na mizizi yake....wenzao wanastrong hold maeneo nyeti na influence kubwa maeneo hayo, lakini ndugu zetu walivimbiwa na kuchokonoa kila mahala kiasi cha kufanya sasa isemwe, "No trust to them again"
 
Kwamb aende ukweniiiii Haka nako ni kakipengele
 
Huyu ni vema akamatwe mapema, ajibu tuhuma dhidi yake, awataje watu wake aliokuwa akiwatumia kuendesha uharamia. Mmoja tunaambiwa yupo mahabusu kule Kusini mwa nchi kwa kosa la kumpora fedha mfanyabiashara na kisha kumwua.
Kwanini serikali inapata kigugumizi kumkamata?! Hii kauli ya kina kirefu cha maji yaliyotulia inaashiria nini!

Who is behind him!
 
Kumbe baadhi nchi anaweza kwenda lakini hao jamaa hawezi kuwakimbia hata nje wapo ni familia
 
Kama anaweza kutoka hapa nchini na atoke kwa kweli, ule utetezi wake jana kwenye hauingii akilini kabisa, yaweza kua alikua kweli na nia njema katika kuwaletea watu haki na ustawi mwema lakini ndini yake alikua na roho mbaya kwa wengine, ni kusema alizidisha harakati zake mpaka kuguswa maisha na maslahi ya watu na pasipo yeye kuangalia usalama wake kesho ambayo ndio leo yake.
Alipo kua na wakati mzuri kwake alisahau kua nyakati hazidumu.
 
Wanaweza wakafanikiwa wakamshtaki au hata kumuua lakini kesho ataokea mwingine naye atataka kulipiza kisasi kwasababu anazo zijua mchezo wa visasi hauna mwisho ndiyo maana watu Aina ya Mandela ni adimu Sana lakini wanatoa fundisho kubwa Duniani.
 
Atoke hadharani aombe radhi kwa aliyofanya ya hovyo kwa umma na watu binafsi, hayaondoki hayo milele bila hiyo namna, ushamba, sifa za kijinga na uroho wa mali ukauzunisha hata kupoteza wengi.
 
Mfano ungelikua wewe ndo Makonda kwa aliyoyafanya yngekimbilia nchi gani?

Maana hata US ambaye ndo kiranja kampiga Pini huyo mtu
 
Unamshauri huyo mpuuzi wanini,acha aliwe kichwa mbuzi yule!
 
Hama Nchi Kwa Muda watu uliowatesa ni wengi ila kwakuwa tumeambiwa samehe 7 mara 70 tumeshasamehe ila Kwa Usalama wako zaidi hamia Kwa Mkeo ukweni Rwanda Au Nenda Ulaya Kasome hata Miaka minne utarudi Tanzania hasira za wengi zikiwa zimetulia,
Bro uovu wa huyu jambawazi ulikuwa mkubwa mno, asilalamike kwani ni 'shoka kwa shoka', 'sururu kwa sururu' 'damu kwa damu'
'ukatili kwa ukatili'
 
Makonda ametoa funzo kwa Vijana tukipewa madaraka tuwe na mipaka na umakini mkubwa kwenye kudeal na mambo.. tutende haki na sio kunyang'anya haki, tuache tamaa za mali bali tujikite kwenye utumishi na maadili yake..
Ali Hapi alikua nae anaelekea huko nadhani Kuna wakubwa walimng'ata sikio akatulia.
 
Huyu ni WA kufa mapema maana ndio alikuwa msimamizi mkuu was genge la wasiojulikana.

Pia ndiye aliyesimamia kupigwa risasi Tundu Lissu.

Hawezi kupona atamfuata shetani mwenzie kule kuzimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…