Naanza kuamini Bundi kulia usiku Mahali palipo na mgonjwa ni ishara mbaya

Mtu akianza kufa, huwa anaanza kufa taratibu.

Sehemu baadhi hutangulia kufa kabla ya ubongo.

Bundi anauwezo wa kunusa mwili ambao umeshaanza kufa hata akiwa mbali!!
 
Hii ni kweli ila iko kisayansi, bundi anauwezo wa kuhisi harufu ya dead cells za kiumbe hai. Mwanadamu ambaye ni mgonjwa Huwa anakufa kiungo kimoja baada ya kingine kabla moyo haujasimama.
 
Sio bundi tu hata mbwa, Mbwa wa mtaa mzima.!!

Kuna mlio flani ivi wanalia tofauti na ule wa kubweka, wakitoa huo mlio zaidi ya siku 3 ujue tayari.
 
Sio bundi tu hata mbwa, Mbwa wa mtaa mzima.!!

Kuna mlio flani ivi wanalia tofauti na ule wa kubweka, wakitoa huo mlio zaidi ya siku 3 ujue tayari.
Ukute ni wale mbwa wanakula hadi mapera sasa choo hakitoki halafu sisi tunadhani wanatabiri kifo.
 
Bundi ana uwezo wa kunusa harufu ya kifo siku 14 kabla ya kifo kutokea na huwa hachezi mbali na eneo la tukio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bundi Wala hahusiani na mambo ya kichawi ila ana uwezo mkubwa wa kuhisi Kifo. Hii ni kulingana na mapokeo ya wazee wetu not confirmed scientifically.
 
Mtu akianza kufa, huwa anaanza kufa taratibu.

Sehemu baadhi hutangulia kufa kabla ya ubongo.

Bundi anauwezo wa kunusa mwili ambao umeshaanza kufa hata akiwa mbali!!
UONGO UONGO UONGO UONGO
 
Kwa mila za kwetu ukisikia sauti ya mbinu na mbweha kwa kweli hapo hata kama hakuna mgonjwa lakini familia inakuwa na mawazo sana, lazima juhudi za mazingara zifanyike kuwaondoa kwenye dimbwi la mikosi na nia mbaya
 
Ni bundi na siyo mbinu
 
Bundi ana uwezo wa kunusa harufu ya kifo siku 14 kabla ya kifo kutokea na huwa hachezi mbali na eneo la tukio

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijawahi sikia kuna watu wamefukiwa na kifusi bundi wakaja eneo hilo na kuanza kulia.

Mahospitalini wanapokufa watu daily yupo?

Vipi kwenye maeneo yenye vita na majanga ya asili yanaoua watu huko duniani?

Au ni bundi wa hapa kwetu tu ndo wamejaaliwa huo unusaji?
 
Nakumbuka nikiwa Form 3 mwaka 1987 niliumwa Pneumonia kali na nikaandikiwa Xpen za masaa....usiku wake hali ilikuwa mbaya vichomi kila sehemu kifuani....sikuweza kulala na usiku wa manane nilistukia bundi katua kwenye fensi nje ya dirisha langu anaangalia kwangu na baadae mbwa wa mtaani walianza kulia sana....nikajua sasa naondoka.....usiku ule ulikuwa mrefu na mgumu na hofu ya kufa ilinijaa kwani nilikuwa naamini mambo hayo ya bundi na vilio vya mbwa ni uchuro..........ila namshukuru Mungu nilifika asubuhi na nilipona na nipo mpaka sasa.....Mungu ni mkubwa.
 
Upo sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…