Naanza kutilia shaka uwezo wa Rais Samia kuongoza Taifa

Naanza kutilia shaka uwezo wa Rais Samia kuongoza Taifa

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo.

Pamoja na mapungufu yake Magufuli alikuwa na watu wake (inner circle) aliowaamini waliokuwa wanampatia taarifa sahihi hasa za ndani, SSH hana anategemea watu wa system ambao wengi wao wana ajenda zao binafsi ikiwemo ya kumpata mrithi baada yake.

Kwamba Marekani wakimaliza uchaguzi hakuna mikutano ya hadhara wala maandamano, it’s wrong, hadi leo Trump anafanya mikutano, Marekani maandamano ni kila siku tumeona wakati wa ‘Black Lives Matters’ nk nk.

Kwamba yeye (Samia) hawezi kuingilia kesi iliyo mahakamani wakati huo huo anazungumzia maendeleo ya kesi iliyopo mahakamani, kuwa, wanaoshitakiwa kwa ugaidi pamoja na Mbowe kesi zao zimeshasikilizwa na wanatumikia vifungo kabaki Mbowe, hii ni kama keshamhukumu Mbowe anawajenga watu kisaikolojia kuwa kama wenzake wamehukumiwa lazima Mbowe naye atumikie kifungo, hii sio sahihi.

Kwamba, Mbowe alikimbilia Kenya akaanza kupanga ugaidi, kidiplomasia hili halina afya linaweza kusababisha mgogoro kuwa Kenya inahifadhi watuhumiwa wa kigaidi.

Kama Rais mwenyewe anaitangazia dunia kuwa kuna watu Tanzania wamehukumiwa kwa ugaidi anategemea investor gani ata invest kwenye nchi ya magaidi, it’s just a common sense kulitambua hilo.

Haya ni machache kati ya mengi niliyoyaona kuhusiana na uwezo wa Rais kuchambua mambo kwa hadhi ya urais. Kama ni wasaidizi wake wanampotosha ama yeye kwa makusudi anaamua kupotosha, basi yampasa awe na uwezo wa kugundua na kujua madhara yake.

Leo kuna watu wameanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa Samia (kiuongozi).

Ndio maana nikasema naanza kuwaelewa watu hasa ‘Sukuma Gang’ kina Gwajima, Polepole, Bashiru wanaoonyesha wazi kutofautiana na Mwenyekiti wao, pamoja na sababu kutosemwa lakini wana send message kuhusiana na uwezo wa rais.
 
Twende mbele turudi nyuma upinzani lazima ujitafakari why mnakimbilia kumsapoti mtu bila kujiridhisha?? Kuna agenda nyingi za kusimamia ambazo zingewaboost suala la tozo,chanjo then mnakuja kwny katiba sasa nyie mnajua kabisa watanzania wengi Wana mashaka na chanjo nyie kutwa kuwahimiza suala la tozo kimya
 
Kama umeanza kuwa na wasiwasi naye leo basi nakupa pole mkuu, mwenziyo tangu atuambie kuwa tutaomboleza siku 14 badala ya 21 tukajua tayari fwamba.
Kweli hata Mimi Siku ile nilishangaa 14/21.Anajua katiba ila hana uelewa wa Katiba.

Ameulizwa na BBC ulijiandaa kuwa Rais?

Amesema kwa kweli hakujiandaa kwa kifo cha Rais kufa akiwa madarakani ndio ilikuwa Mara ya kwanza.Hivyo hakujua kikatiba nini tafsiri ya VP.

Muda aliotumia na BBC ameharibu zaidi kuliko muda huo angetumia kukutana na vyama vilivyochambukachambuka ili kuleta umoja
 
Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo...
Kama ulihitaji miezi yote hiyo kuling'amua hili then ww pia huenda huko sawa mkuu.
 
Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo...
Ametangaza kuwa mtu anayetuhumiwa kwa ugaidi ameshtakiwa!! Hili sio kizuizi kwenye uwekezaji
 
⏰💯 ni mweupe na mwepesi mno. Katiba imetupiga hapa kutuletea huyu mtu.

Tumepigwa mbaya sana si kdg. Hii nchi sijui ilimkosea nn Mungu mpk anaiadhabu kiasi kikubwa kama hiki. Hakuna aliyehukumiwa kwenye kesi ya akina Mbowe. Watuhumiwa so far ni wa4 na hakuna aliyekuhumiwa. Kwanini Rais anasema wameshahukumiwa?

Eti Mbowe amefanya vurugu na kuitisha maaandamano, ina maana Rais hana taarifa kwamba maandamano ni haki ya kikatiba? Rais anasema wapinzani wanafanya maandamano na kuchoma magari, ni lini hayo yametokea?

Huenda wasaidizi wa Rais hawafanyi kazi yao sawa hii si sawa kbs.
 
Tulipo tunahitaji nguvu ya ziada ili walau tupige hatua, Watanzania tunatia huruma mno, wengi wetu hatujui tunaamini nini na kwa wakati gani ndiyo maana tunakosa hata nguvu ya kufanya maamuzi sahihi juu ya tunachokitaka.
 
Back
Top Bottom