Naanza kutilia shaka uwezo wa Rais Samia kuongoza Taifa

Naanza kutilia shaka uwezo wa Rais Samia kuongoza Taifa

Nimeisikia sana hiyo kauli "a man is a political animal" kujustify nguvu kubwa ya raslimali watu na raslimali fedha inayotumika kwenye siasa, tena za ushindani.

Nchi hii maskini wanasiasa wanalipwa marupurupu kibao utadhani ni maCEO wa billion dollar companies.

Kuna hadi ruzuku za vyama vya siasa kila mwezi katika chi ambayo kila sehemu unapopita hata mijini ni makorongo, wanafunzi wanasomea chini ya miti.

Unawezaje kuwekeza nguvu kubwa kwenye siasa za tom and jerry wakati real issues zimelala?

Leo hii kijana anamaliza chuo hata hajafanya lolote la maana kwenye jamii yake anataka kazi yake ya kwanza aende bungeni. Kisa? Kwa sababu tumejenga linchi linalothamini wapiga domo wa majukwaani kuliko watu wanaofanya mambo halisi on the ground.

Awkward!

You earn my vote 🙂
 
Nope. Criticism yako kuhusu Rais Samia ni kwa sababu maslahi yako ya kisiasa yameguswa basi.

Mlimsema hivyo Rais Magufuli mkamwita dikteta uchwara. Leo hii anaonekana afadhali kwa sababu hayupo hai?

Rais pekee atakayeonekana imara kwenu ni yule tu atakayefanya yale mnayoyataka. Pale atakapopishana nanyi mara moja ataonekana hafai.

Kwa sisi wengine kufeli au kufaulu kwa Samia hakutegemei mambo yenu ya siasa.
Poor them, kila asiyeyasikiliza yao kwao atapewa jina...Wamekosa malengo wamebaki kusubiria mkono kudondoka kama yule mnyama scavenger...I pity these people!
 
Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo.

Pamoja na mapungufu yake Magufuli alikuwa na watu wake (inner circle) aliowaamini waliokuwa wanampatia taarifa sahihi hasa za ndani, SSH hana anategemea watu wa system ambao wengi wao wana ajenda zao binafsi ikiwemo ya kumpata mrithi baada yake.

Kwamba Marekani wakimaliza uchaguzi hakuna mikutano ya hadhara wala maandamano, it’s wrong, hadi leo Trump anafanya mikutano, Marekani maandamano ni kila siku tumeona wakati wa ‘Black Lives Matters’ nk nk.

Kwamba yeye (Samia) hawezi kuingilia kesi iliyo mahakamani wakati huo huo anazungumzia maendeleo ya kesi iliyopo mahakamani, kuwa, wanaoshitakiwa kwa ugaidi pamoja na Mbowe kesi zao zimeshasikilizwa na wanatumikia vifungo kabaki Mbowe, hii ni kama keshamhukumu Mbowe anawajenga watu kisaikolojia kuwa kama wenzake wamehukumiwa lazima Mbowe naye atumikie kifungo, hii sio sahihi.

Kwamba, Mbowe alikimbilia Kenya akaanza kupanga ugaidi, kidiplomasia hili halina afya linaweza kusababisha mgogoro kuwa Kenya inahifadhi watuhumiwa wa kigaidi.

Kama Rais mwenyewe anaitangazia dunia kuwa kuna watu Tanzania wamehukumiwa kwa ugaidi anategemea investor gani ata invest kwenye nchi ya magaidi, it’s just a common sense kulitambua hilo.

Haya ni machache kati ya mengi niliyoyaona kuhusiana na uwezo wa Rais kuchambua mambo kwa hadhi ya urais. Kama ni wasaidizi wake wanampotosha ama yeye kwa makusudi anaamua kupotosha, basi yampasa awe na uwezo wa kugundua na kujua madhara yake.

Leo kuna watu wameanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa Samia (kiuongozi).

Ndio maana nikasema naanza kuwaelewa watu hasa ‘Sukuma Gang’ kina Gwajima, Polepole, Bashiru wanaoonyesha wazi kutofautiana na Mwenyekiti wao, pamoja na sababu kutosemwa lakini wana send message kuhusiana na uwezo wa rais.
I cant add or minus anything on this article, you have said it all!
 
mama na mimi anaanza kuniudhi, hivi kulikuwa na haja gani ya kuongea na vyombo vya habari kwanza?!! angekausha tu na kuwaachia wenyewe wanayotaka kuyaongea bila kuhusisha sauti yake. ukweli ni kuwa hivi vyombo vya habari lengo kuu haswa ni kutafuta madhaifu ya mtu tu na si kutangaza habari njema zake........ilipaswa alitambue hilo. hapo ameshajikoroga, hayo maneno yake mawili matatu aliyoyaongea yatachambuliwa kwa kila namna kwa muda mrefu hata wa miaka mitatu, na zile point zake muhimu zote hautozisikia zikizungumzwa hata chembe........watakomaaa kwenye tafsiri zao tu na maoni yao. kipindi ambacho hata ndani kuna wasiokutakia mema kama kina pole pole na mwenzake gwajima (sababu ya ukabila, dini na ukanda), ni kipindi cha kuchunga mno ulimi.

by the way, mazungumzo yao sijayasikiliza naishia kuona mashambulizi tu humu mtandaoni (jambo ambalo si jipya kwa wafuasi wa chama fulani hivi kwani wao kuna wanayotaka kuyasikia sasa mtu asipoyaongea tu hayo basi matusi, kejeli, vijembe n.k ndo malipo yake); ninajua athari za vyombo vya habari.hii ni fursa nzuri ya kuanzia mama, afanye mambo ya maendeleo wakati mitandao inapokuwa against nae halafu muda si mrefu utaona watapiga kelele wenyewe za kukupongeza. ilikuwa hivyo kwa magufuli, alikuwa anapondwa mno lakini akaziba masikio na kuendelea na mishe zake, mwisho wa siku leo kila mtu anampongeza. ukiona watu fulani hivi wanakusifia sifia ujue kuna mahali hapapo sawa......wamepata mwanya wa kukuchezea.

Aiseee!!! Umelia sana hadi huku Chattle kaburi la Chuma limetikisika likisema ^Hivi mmeanza kunikumbuka mapema hii, eeeh!???^ 🙂 🙂 🙂
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Mkuu wa nchi kabisaaa anaji ng'atang'ata ivo duuu Mungu tunusuru na haya mapito
 
Najua mtanikumbuka,nlakini hamtanikumbuka kwa mabaya!

R.I.P! niko safarini naelekea Dodoma kwenye vikao vyetu maalumu, tumeaibika kwakweli!
 
Oooh! anajua kiingereza, oooh! huyu ni muungwana, Oooh! angalau watu wana nyuso za furaha! Yaani tuna mijitu mijinga ktk nchi hadi inatia shaka. JF yenyewe imejaa mijitu ya hovyo hovyo hadi unashangaa mitandaoni inafanya nini! Tena watu wako ktk ajira za serikali wanatamani rais mzembe!
Inaboa kuliko maelezo mkuu.......
 
Baada ya kusikiliza interview ya Rais Samia Suluhu na Salimu Kikeke, nimegundua mambo matatu kwenye uongozi wa Samia Suluhu, aidha Rais hayuko well informed au anadanganywa/potoshwa au uwezo wake wa kutambua mambo ni mdogo.

Pamoja na mapungufu yake Magufuli alikuwa na watu wake (inner circle) aliowaamini waliokuwa wanampatia taarifa sahihi hasa za ndani, SSH hana anategemea watu wa system ambao wengi wao wana ajenda zao binafsi ikiwemo ya kumpata mrithi baada yake.

Kwamba Marekani wakimaliza uchaguzi hakuna mikutano ya hadhara wala maandamano, it’s wrong, hadi leo Trump anafanya mikutano, Marekani maandamano ni kila siku tumeona wakati wa ‘Black Lives Matters’ nk nk.

Kwamba yeye (Samia) hawezi kuingilia kesi iliyo mahakamani wakati huo huo anazungumzia maendeleo ya kesi iliyopo mahakamani, kuwa, wanaoshitakiwa kwa ugaidi pamoja na Mbowe kesi zao zimeshasikilizwa na wanatumikia vifungo kabaki Mbowe, hii ni kama keshamhukumu Mbowe anawajenga watu kisaikolojia kuwa kama wenzake wamehukumiwa lazima Mbowe naye atumikie kifungo, hii sio sahihi.

Kwamba, Mbowe alikimbilia Kenya akaanza kupanga ugaidi, kidiplomasia hili halina afya linaweza kusababisha mgogoro kuwa Kenya inahifadhi watuhumiwa wa kigaidi.

Kama Rais mwenyewe anaitangazia dunia kuwa kuna watu Tanzania wamehukumiwa kwa ugaidi anategemea investor gani ata invest kwenye nchi ya magaidi, it’s just a common sense kulitambua hilo.

Haya ni machache kati ya mengi niliyoyaona kuhusiana na uwezo wa Rais kuchambua mambo kwa hadhi ya urais. Kama ni wasaidizi wake wanampotosha ama yeye kwa makusudi anaamua kupotosha, basi yampasa awe na uwezo wa kugundua na kujua madhara yake.

Leo kuna watu wameanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa Samia (kiuongozi).

Ndio maana nikasema naanza kuwaelewa watu hasa ‘Sukuma Gang’ kina Gwajima, Polepole, Bashiru wanaoonyesha wazi kutofautiana na Mwenyekiti wao, pamoja na sababu kutosemwa lakini wana send message kuhusiana na uwezo wa rais.
Ni lini uliona ana uwezo wewe nyumbu wa makengeza mbowe 🤣🤣🤣

Naona mnajitekenya na kucheka wenyewe kama ngiri
 
Back
Top Bottom