Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nimekuambia Kuwa Ilikuwa Ni metaphor na wala Sio kuongea Kwa Kuongea Hili swala Nimelijibu Ila Ulipohoji Ndo nimekupa Maswali..
Ila Ilikuwa Ni metaphor na Sio Kitu halisia
Sawa ilikuwa metaphor .sasa nakukumbusha jina la kitabu kinaitwa SENSA .hiyo metaphor inatosha hapo .😁
Hao sio wahusika wa biblia hayo ni matukio yaliyotukia duniani zama mbalimbali na Allah ndio alikuwa anatusimulia.
Sawa .ili nikuamini naomba takwimu za kizazi cha Ishmael.najua Allah alikwisha kusimulia😸😸😸😸
 
Hili bandiko ni refu sana. Kama ni mtu unaependa summary wala usilisome.

Huyu jamaa anajichanganya. Biblia ina sehemu kuu mbili, Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale lilitokana na Torati ya Wayahudi. Wayahudi ni kabila na dini. Yesu na wafuasi wake wa mwanzo walikuwa wayahudi kwa hiyo alilelewa katika tamaduni hiyo. Wakati Yesu anaishi, Uyahudi ulikuwa sehemu ya himaya ya warumi.

Baada ya kifo cha Yesu wafuasi wake wakawa wanakumbushana kuhusu maisha yake. Injili nne zilizomo kwenye Agano Jipya ziliandikwa kati ya miaka 66 na 110 baada ya kifo cha Yesu. Ya kwanza iliandikwa na Marko, ikafuatwa na ya Mathayo na ya Luka. Ya mwisho iliandikwa na John. Haya maagano yaliandikwa kutokana na simulizi na ushuhuda wa wale waliokuwepo wakati wa uhai wa Kristu. Hii si ajabu maana waliokuwa wanajua kuandika wakati ule walikuwa wachache na mafundisho ya Yesu yalipingwa sana na wayahudi ambao waliona ni tishio kwa imani yao.

Mwanzoni ukristu ulichukuliwa kama vile ulikuwa kwa ajili ya wayahudi tu. Ni Paulo, ambae alikuwa mrumi ndie aliyefungua mlango kwa wale ambao sio wayahudi. Hamna mahali panaposema kuwa Biblia iliandikwa na Mungu. Ni binadamu ndio walioandika na ndio maana injili zinatofautiana katika simulizi zake.

Pamoja na yote haya, ni imani yetu wakristu kuwa mitume walioandika Injili waliongozwa na Mungu ndio maana tunasema ni Neno la Mungu ikimaanisha kuwa ni ujumbe wa Mungu. Hata Koran Takatifu iliandikwa kutokana na simulizi za Mohammed S.A.W maana yeye mwenyewe alikuwa hajui kusoma wala kuandika.

Kusema kuwa warumi walificha Biblia ni uongo mtupu maana wakati wakristu wanaandamwa na utawala wa warumi hapakuwa na Biblia. Na ukristu ulipata uhai baada ya kiongozi wa warumi, Constantine wa kwanza kujiunga nao na kuitangaza kuwa dini ya utawala wake katika kikao cha Nicae miaka 300 baada ya kifo cha Kristu. Sasa atasemaje Roman Empire ilificha Biblia wakati baada ya Constantine ilikuwa ndio dini ya taifa?

Kikao cha Rome kilichofanyika 382 AD ndicho kilichoamua vitabu vipi viunde Agano la Kale na Jipya. Kulikuwa na kikao kingine mwaka 393 ambacho kilipitisha muundo wa kitabu cha Biblia tunacho kijua sasa hivi. Palikuwa na vikao vingine baada ya hapo. Cha mwisho kilifanyika 1545 mpaka 1563 na kusema Biblia ya kikatoliki itakuwa na vitabu 46 katika Agano la Kale na 27 katika Agano Jipya. Madhehebu mengine nayo yalikuja na tafsiri zao. Kanisa lake Mashariki nalo lina Biblia na tafsiri yake. Tafsiri zote hizi zina msingi mmoja ila zinatofautiana kidogo kidogo.

Shida ya wengi wetu tunamchukua Mungu kama binadamu mwenye mikono, mdomo na anayeandika kama sisi. Ukweli ni kuwa kwa kiasi kikubwa uelewa wa Mungu ulitokana na context ya wakati ule. Musa alipoandika Kitabu cha Mwanzo aliandika kwa uelewa wake wa wakati ule. Kwake yeye dunia ilikuwa uyahudi kwa hiyo mifano na simulizi zake zilitokana na experience yake. Hakujua kuna Afrika, kuna Marekani au sehemu iliyotanda barafu.

Watu kama huyu Nabii hawajui wanalosema. Ila kwa sababu tuna tabia ya kuamini kila tunachoamini basi wanakusanya wafuasi kibao.

Amandla....
 
Huyu ni wakala wa shetani! Nadhani kafikia mwisho wa kazi yake anamalizia. Anawaandaa waumini wake kisaikolojia. Kama wewe unaabudu kwake be prepared!
 
Mkuu una hoja; usikilizwe. Tusubiri wenyewe waje kutupa majawabu.

Wakati tukisubiri wataalamu waje, hebu kula chuma hiki mkuu:
***************************************************************************************
Here's a more detailed explanation:
  • Common Ancestry:
    Scientific evidence, including genetic studies, strongly supports the idea that all humans are descended from a small, ancestral population that lived in Africa.

  • Migration and Adaptation:
    As humans migrated and settled in different parts of the world, they adapted to their local environments through natural selection. This adaptation led to variations in traits like skin color, stature, and susceptibility to certain diseases.

  • Genetic Variation:
    While humans share a vast majority of their DNA, there are differences that have accumulated over time due to random mutations and genetic drift.

  • "Races" are a Social Construct:
    The concept of "race" is a social construct, not a biological reality. There is more genetic variation within so-called "racial" groups than between them.

  • Interbreeding:
    Humans have interbred across geographic regions, further blurring the lines of "racial" distinctions.

  • Not Separate Origins:
    The idea that different "races" evolved from separate origins is a misconception.

  • Evolutionary Processes:
    The differences we see in human populations are the result of evolutionary processes, not separate origins.
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo chake, Hata chanzo cha kila kitu lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo chanzo, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje ku exist chenyewe tu bila chanzo.

Hata huyo binadamu wa kwanza, Haiwezekani atokee tu, from nowhere. Na yeye lazima awe na chanzo chake.

Na chanzo cha huyo binadamu wa kwanza kiwe na chanzo chake, Hivyo hivyo pasipo kukoma.

Kwa maana hiyo, Kutakuwa na vyanzo vingi visivyo na mwisho, pasipo kukoma endless.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mwanzo, Hata binadamu hawana binadamu wa kwanza.
 
Hahaha Very Impressive Mimi nahisi Ni kama Wewe Sema Mimi Nilivuka more Way further maana Baada ya Kutoka kwenye Uislmu nilikuwa Myahudi 😀😀
Unajua kuna thin line ya intelligence na uchizi,nikisoma mapito yako ya kiimani na elimu,najua wewe ni very intelligent darasani,wale intelligent wenye element za uchizi,yaani ulitoka ukristu,ukaenda uislam, ukaenda uyahudi,halafu ukaacha kuamini juu ya Mungu
 
Biblia siyo maneno ya Mungu bali ya watu,mbona uko wazi
Mimi nafahamu kilichopo nyuma yake. Huyu ni mfuasi wa shetani ni freemasonry aliyejificha kwa mlango wa biblia baada ya kuona muda wake wa kazi kwisha sasa anaanza kutapatapa. Na bado yapo mengi atasema. Biblia ni neno la Mungu! Na ni neno lilihai!
 
Sawa ilikuwa metaphor .sasa nakukumbusha jina la kitabu kinaitwa SENSA .hiyo metaphor inatosha hapo .😁

Sawa .ili nikuamini naomba takwimu za kizazi cha Ishmael.najua Allah alikwisha kusimulia😸😸😸😸
Kivipi yani
 
Hayo maswali ukiwauliza wafia dini humu wanaanza kukulaani, ukweli ni kwamba upeo wao ni mdogo wanapelekwa km nyumbu..!!
Uzuri ni kwamba kwenye Mungu amewavuta kila watu wa kila nyazifa na elimu tofauti kama mtu atasema dini ni kwa wajinga basi utaoneshwa wasomi haswa ambao ni maprofesa na Wacha Mungu
 
DNA inabadilika kulingana na Mazingira na Sababu nyingi na kupelekea kuzalisha offspring ambayo ni tofauti na ancestors.

Swala la DNA ni haliwezi kulinda point yako. Inawezekana kabisa mtu mmoja akazaa albino, mtu huyohuyo akadhaa mweusi na watoto wake huwenda wakazaa Wazungu.
Yes. DNA inabadilika kutokana na mutations pamoja na genetic drift.
 
Kufikirika na kusadikika maana yake ni kutokuwepo?
Unaweza kufikiri na kusadiki chochote.

Unaweza kufikiri na kusadiki hata kitu cha uongo ambacho hakipo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa hicho unacho kifikiri na kukisadiki, ni kwamba hakipo.

Na kufikiri kwako ni uongo tu.

Mimi nakwambia specifically Mungu hayupo.
 
Kama palikua na nyoka na miti maana yake vilikuwepo kabla ya Adam,na adam na mkewe kurubuniwa haimaanishi Mungu kuzidiwa akili bali udhaifu wa binadam, wangapi wanatapeliwa/danganywa hata leo!?..hilo ni umbile la binadam,free will
Sasa Mungu kwann aliumba binadamu dhaifu wakati alijua kuna nyoka ambaye atamdanganya? Na kwa maelezo ya biblia shetani alivaa Umbo la nyoka, je shetani naye aliumbwa siku gani? Au yeye na Mungu walitokea wapi?
 
Sio. Biblia tu vitabu vyote vya kiimani
Kwa Quran hapana, tazama muundo wa Quran, mtume anasema nimeshushiwa wahyi,kwa kuwa hajui kuandika anawaambia waandishi wake,wanajiandaa kuandika (Quran 25:4-5),aya za Quran..'wanakuuliza kuhusu zakkat,sema uwaambie,sema Mungu ni mmoja,hakuzaa wala kuzaliwa nk..kama ushawahi soma Quran utakua umeelewa, sasa bible ni tofauti,ni kama elvis musiba anamuelezea willy gamba
 
Sasa Mungu kwann aliumba binadamu dhaifu wakati alijua kuna nyoka ambaye atamdanganya? Na kwa maelezo ya biblia shetani alivaa Umbo la nyoka, je shetani naye aliumbwa siku gani? Au yeye na Mungu walitokea wapi?
Shetani si kiumbe bali sifa, shetani yule alikua ibilisi ambaye kiumbile ni jini,na hata leo,umbo la nyoka ndiyo majini hupendelea kujibadilisha wajapo kwa binaadam,ukiacha njiwa,majini kama malaika,yaliumbwa kabla ya binadam
 
Back
Top Bottom