Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Ushahidi unaonesha kuwa KORANI imekopi kila kitu kutoka kwenye BIBLIA kama inavyosomeka kwenye screenshot hii hapa. Kwa hiyo ndugu zangu, masimulizi ya hizi dini mbili kumbe yanaashiria kuwa ni masimulizi ya wanadamu na wala sio neno la Mungu wala Allah. Tumepigwa!
View attachment 3283684
.huyu ni mfanyabiashara/mwekezaji wa kuchuma toka kwa idiots evangelical christians
 
Wakristo na waislam wa kiafrika wote ni mbwa wasijua bwana wao si quruan au biblia iliyo juu ya Mwafrika.

Ni kutojitambua tu,kwanini vitabu hivyo vishushwe kwa warabu na wazungu tu na kusiwe na vitabu hivyohivyo au vingine vilivyoshushwa india,china,kenya,usa,nk?
 
Great thinking.
 
Bila shaka hiyo ilikuwa katika kitabu cha Kumbukumbu la torati......hiki kitabu ni riwaya kama riwaya nyingine mkuu......katika riwaya mwandishi amepewa mamlaka ya ku impersonate viumbe visivyokuwa binadamu.
Bibilia ni kitabu tu unasoma km nongwa zingine.
Nilisoma bibilia km kitabu na nikamaliza koote nikaweka mukichwa..
Biblia ni maandishi tu.
Fwata unachoona kiko sawa vingine tupilia mbali.
Kama zambi ya kwanza ni kwenda chooni kila muda.
Hiyo dhambi no 1.
Hata Trump na Netanyau na m7 nanani sijui.
Dakika ya mwisho wanataga kule chooni.
 
Sasa kwanini wachawi wanakiogopa kitabu cha biblia? Ukishika kitabu cha biblia ukapita maaneo waliopo wachawi wanatamani kukufukuza. Na kwanini ukichukua spika ukaanza kuhubiri kitabu cha biblia karibu na nyumba za wachawi wanaogopa wanafanya kila wawezavyo kukuzuia usiendelee kuhubiri maaneo yao?
Tunaomba majibu.
 
Huyo anajulikana ni wa nani...Mwongo kama baba yake ibilisi
 
Naomba niwape siri:
Biblia ni neno la Mungu:

1. Neno la Mungu ni Upanga wa Roho - Linatumika kupigana vita vya kiroho dhidi ya shetani na majeshi yake. Ndio maana ukitaja neno la Mungu karibu na wachawi wanatoroka au wanatamani wakufukuze uondoke. (Waefeso 6:17)

2. Neno la Mungu ni Moto wa kiroho – Linachoma kila uchafu, udanganyifu, na nguvu za giza. Ukianza kusoma au kutamka neno la Mungu mahali pa uchawi, hata watu wa giza wanakosa amani na kuanza kutetemeka. (Yeremia 23:29)

3. Neno la Mungu ni Nyundo – Linavunja kila kizuizi cha kiroho na kifungo cha shetani. Ukikutana na vizuizi vya maisha, unapotamka neno la Mungu kwa imani, mambo yaliyokuwa yamefungwa yanafunguliwa ghafla. (Yeremia 23:29)

4. Neno la Mungu ni Taa ya miguu yetu – Linaongoza njia ya maisha ili tusipotee. Wakati hujui cha kufanya au umechanganyikiwa, neno la Mungu linakupa mwanga wa kuchukua hatua sahihi. (Zaburi 119:105)

5. Neno la Mungu ni Ngome ya kweli – Hutoa ulinzi dhidi ya hofu, mashaka, na mashambulizi ya adui. Mtu akijua neno la Mungu moyoni, hata akikumbwa na hatari, anakaa mtulivu na salama.

6. Neno la Mungu ni Mbegu ya kiroho – Linapopandwa ndani ya moyo huzaa matunda ya ushindi na wokovu. Wakati mwingine unaweza kufundisha mtoto au rafiki neno la Mungu leo, akalielewa na kulikubali baada ya miaka kadhaa. (Luka 8:11)

7. Neno la Mungu ni Dawa ya uponyaji – Linaponya roho, nafsi, na hata mwili. Kuna watu walikosa amani kwa magonjwa ya ndani, lakini baada ya kushika neno la Mungu wakaona uponyaji wa ajabu. (Mithali 4:22)

8. Neno la Mungu ni Nguvu ya Mungu kwa wokovu – Huokoa na kuleta maisha mapya. Watu wengi waliokuwa wamedhoofika au wamekosa tumaini, walipolisikia neno la Mungu wakapata nguvu mpya na kubadilika kabisa. (Warumi 1:16)

9. Neno la Mungu ni Nuru ya maisha – Linatoa mwanga katika giza la ulimwengu. Unapokuwa kwenye giza la matatizo au huzuni, neno la Mungu linakuonyesha njia ya matumaini na faraja. (Zaburi 119:130)

10. Neno la Mungu ni Chakula cha roho – Linatulisha na kututia nguvu ya kiroho. Ukiacha kusoma neno la Mungu, unajikuta huna nguvu za kiroho na unakuwa dhaifu rohoni. (Mathayo 4:4)

11. Neno la Mungu ni Kioo – Linatuonesha hali yetu halisi na kutusaidia kubadilika. Unaposoma neno la Mungu, linakuonyesha makosa yako na maeneo yanayohitaji kurekebishwa. (Yakobo 1:23)

12. Neno la Mungu ni Msumeno wa kiroho – Huchambua roho na nafsi, mawazo na nia. Kuna mambo mengi tuliyoficha ndani, lakini tukisoma neno la Mungu, linafunua na kutusaidia kutubu. (Waebrania 4:12)

13. Neno la Mungu ni Ushuhuda wa kweli – Linasimama dhidi ya uongo na udanganyifu wa adui. Hata kama watu wanazusha habari zisizo sahihi, neno la Mungu linaendelea kuthibitisha ukweli.

14. Neno la Mungu ni Sauti ya Mungu – Ni njia ambayo Mungu huwasiliana nasi moja kwa moja. Wakati mwingine unapokuwa na maswali moyoni, ukisoma neno la Mungu unakutana na majibu yanayogusa maisha yako moja kwa moja.

15. Neno la Mungu ni Silaha ya kujitetea – Hutumika kujikinga dhidi ya hila za shetani. Wakati wa vita vya kiroho au hofu, ukitumia neno la Mungu unapata ulinzi na ushindi.

16. Neno la Mungu ni Nguvu ya kukomboa – Linaweza kuvunja laana na vifungo vya kizazi. Watu wengi waliokuwa wamefungwa na laana za familia, walipotumia neno la Mungu wakafunguliwa na maisha yao kubadilika.

17. Neno la Mungu ni Chemchemi ya hekima – Linatufundisha maarifa na namna ya kuishi kwa hekima. Ukiwa na changamoto, ukitafuta ushauri kwenye neno la Mungu unapata majibu bora kuliko ya binadamu.

18. Neno la Mungu ni Ahadi ya Mungu – Linatuhakikishia neema, rehema, na ushindi. Wakati wa majaribu makubwa, kukumbuka ahadi za Mungu kunaleta faraja na nguvu mpya.

19. Neno la Mungu ni Ushindi katika majaribu – Linatufundisha kushinda majaribu kama Yesu alivyoshinda. Kila wakati unaposhawishika au kukabiliwa na vishawishi, neno la Mungu linakupa ujasiri wa kushinda. (Mathayo 4)

20. Neno la Mungu ni Msingi usioyumba – Hutujenga imani yetu na kutufanya tusiyumbishwe na pepo za mafundisho. Ukijenga maisha yako juu ya neno la Mungu, hata upepo wa dunia ukivuma, hautaanguka kirahisi.
 
Sasa kwanini wachawi wanakiogopa kitabu cha biblia? Ukishika kitabu cha biblia ukapita maaneo waliopo wachawi wanatamani kukufukuza. Na kwanini ukichukua spika ukaanza kuhubiri kitabu cha biblia karibu na nyumba za wachawi wanaogopa wanafanya kila wawezavyo kukuzuia usiendelee kuhubiri maaneo yao?
Tunaomba majibu.
hata mapepo yanaondoka Kwa jina la Yesu ni kweli baadhi ya mambo yaliondolewa lkn msingi wake bado upo, huyo tapeli hajielewi kama walivyo wafuasi wake,kama no maneno ya watu yeye anawafundisha Nini wafuasi wake?
 
mbona wachawi wakubwa ni mapadre, wachungaji, na wanojiita mitume, manabii n.k they are some witches in church, wanatumia biblia
 
hata mapepo yanaondoka Kwa jina la Yesu ni kweli baadhi ya mambo yaliondolewa lkn msingi wake bado upo, huyo tapeli hajielewi kama walivyo wafuasi wake,kama no maneno ya watu yeye anawafundisha Nini wafuasi wake?
Lakini pamoja na utapeli wake, huyu nabii ana hoja. Nashauri asikilizwe.
 
Lakini pamoja na utapeli wake, huyu nabii ana hoja. Nashauri asikilizwe.
Hoja gani? Anadhani hatujasoma bible history na church history?
Huyo nabii wa uongo anadhani hatujui kuhusu Talmud, Septuagint, Vulgate na kwa nini Roman Catholic church wana 72 books na Evangelicals wana 66 books?
Kwa tuliosoma doctrine of Cults and Occults huyo nabii ana sifa zote za wana wa Ibilisi
 
Naona umenisaidia kujijibu wewe mwenyewe mkuu. Kama biblia ni neno la Mungu kwanini idadi ya vitabu inatofautiana?
 
Naona umenisaidia kujijibu wewe mwenyewe mkuu. Kama biblia ni neno la Mungu kwanini idadi ya vitabu inatofautiana?
Mkuu naomba kwa unyenyekevu mkubwa nikujibu from spiritual perspective.
Ili Bible iwe neno la Mungu ni lazima hayo maandiko yawe inspired (2Peter 1:20-21 na 2Timothy 3:16). Naomba nikuulize katika vile vitabu 6 vya apokrifa ambavyo viliongezwa na maaskofu wa kanisa la Roman Catholic mwaka 1546 ukivisoma unaona kuna inspiration yoyote? Na je, unajua ni hoja zipi zilizotumika kuviexclude katika Biblia ya vitabu 66?Kwangu mimi hivyo vitabu huwa navisoma kama vitabu vingine vya historia though vina sababisha contradiction na vitabu vingine katika vile 66 na wala sivitumii katika mafundusho ya msingi yahusuyo imani
 
Basi kwa mukdatha huu, nakubaliana nawe kuwa biblia ni maneno ya wanadamu kwa kuwa wanaweza kuyaongeza na hata kuyapunguza maneno kwenye biblia. So, nabii GeoDavie yupo sahihi 💯 %. Naona sasa tunaongea lugha moja mkuu.
 
Back
Top Bottom