Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Ushahidi unaonesha kuwa KORANI imekopi kila kitu kutoka kwenye BIBLIA kama inavyosomeka kwenye screenshot hii hapa. Kwa hiyo ndugu zangu, masimulizi ya hizi dini mbili kumbe yanaashiria kuwa ni masimulizi ya wanadamu na wala sio neno la Mungu wala Allah. Tumepigwa!
1000195952.jpg
 
Mimi ni mkristu lakini naamini mengine ni hadithi na mengine ni kumbukumbu ya yaliyotokea.

Amandla...
Kwa mfano, unadhani ni yapi ni hadithi mkuu? Mimi nafikiri hadithi ya uumbaji ni masimulizi na hisia za wanadamu kama ilivyo kwenye hadithi ya organic evolution kwenye vitabu vya biology. Nyingine ni ile hadithi ya Nuhu na safina yake. Ile nayo ni hadithi pure. Hebu wewe ongezea yale ambayo unadhani ni hadithi tu mkuu.
 
Kwa mfano, unadhani ni yapi ni hadithi mkuu? Mimi nafikiri hadithi ya uumbaji ni masimulizi na hisia za wanadamu kama ilivyo kwenye hadithi ya organic evolution kwenye vitabu vya biology. Nyingine ni ile hadithi ya Nuhu na safina yake. Ile nayo ni hadithi pure. Hebu wewe ongezea yale ambayo unadhani ni hadithi tu mkuu.
Ile ya Jonah kuliwa na nyangumi. Koo la nyangumi ni dogo kiasi binadamu hawezi kupita.

Amandla...
 
Biblia Yenye Neno La Mungu Haipo Mkuu!
Ilipotezwa zaman sana..
Neno Biblia au Bible ni Neno linalomaanisha Mkusanyiko wa Vitabu..

So yes Naamini Kuna Bible ilikuwa na neno la Mungu ambayo sasa Hatuna
Neno la Mungu halipotei ndugu yangu, unawezaje kupoteza neno la Mungu kwa mfano?
 
Nabii GeoDavie abarikiwe sana kwa kusema ukweli. Sehemu kubwa ya biblia na korani iliandikwa na wanadamu kama hadithi nyingine tunazosoma kwenye tamthlia na hekaya za Abunwasi.

Kwa mfano, hebu niambie Nuhu aliwezaje kukamata wanyama wote (ke/me) tunaowaona hapa duniani na kuwajaza kwenye safina? Yaani akakamata hadi kupe, konokono, viroboto, chawa, tembo, minyoo, nzi, ndege, nk. Hii ni hadithi tu ndugu zangu.

Kama kweli hilo linawezekana, hiyo safina ilikuwa kubwa kiasi gani kujaza viumbe wote wa dunia hii (ke na me).

Kuna wadudu wengine ukiwaangalia hadi unajiuliza hivi kwa mfano, viroboto alivikamataje?

Hizi ni hadithi tu ndugu zangu, msidanganywe.
 
Biblia sio mtaala WA veta..Maneno yasio na asili ya duniani pia tafsiri yake haiko duniani... Waziri mkuu amewataka vijana WA kitanzania wenye degree kurudi veta kupata ujuzi Zaidi na tpaul mwenye akili ya kasuku namshauri aache hizi adventure zisizo level yake aufuate ushauri WA waziri mkuu...

Kitabu cha mwanzo kimeandikwa na Nabii Musa ambae kijana kasuku kama tpaul hamfikii kielimu,,kiuchumi,, exposure,,,utajiri,,kifamilia,,,kiakili,,kimtazamo wala chochote...Lakini kutokana na ukasuku na kufata mkumbo kijana Kutoka mchafu koge ñae ana hoja eti project ya wazungu...

Wewe project yako ni ipi??? Veta kuna fani ya upishi,,karudie upate maarifa.,.Ukiwa jikoni unapikia hoteli muda WA kumkashifu MUNGU hutoupata..
Mkuu tujikite kwenye hoja. Kuna mambo mengi kwenye biblia ambayo ukiyaangalia kwa uhalisia unaona kabisa kuwa hapa tunapigwa. Hebu niambie kwa mfano kama hadithi ya Nuhu ni tukio la kweli au ni hadithi. Give concrete evidences.
 
Ile ya Jonah kuliwa na nyangumi. Koo la nyangumi ni dogo kiasi binadamu hawezi kupita.

Amandla...
Kws hiyo wewe unakubaliana na maneno ya nabii GeoDavie kwa 💯 % au unakubaliana kwa 50%? Kwanini? Give concrete evidence.
 
Kws hiyo wewe unakubaliana na maneno ya nabii GeoDavie kwa 💯 % au unakubaliana kwa 50%? Kwanini? Give concrete evidence.
Kila mtu aamini anavyotaka Mkuu. Huyu jamaa simjui wala simfuatili kwa hiyo inaniwia ngumu kukujibu. Ila kwa ujumla namuona kama msanii ambae mara anapotosha wanaomfuata.

Amandla...
 
Kila mtu aamini anavyotaka Mkuu. Huyu jamaa simjui wala simfuatili kwa hiyo inaniwia ngumu kukujibu. Ila kwa ujumla namuona kama msanii ambae mara anapotosha wanaomfuata.

Amandla...
Hata kama humfuatilii, hayo maneno aliyosema yana ukweli kiasi gani?
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.

View attachment 3279501

MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.

Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.

Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?

Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?

Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?

Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.

Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.

Nawasilisha.

​
mkuu, nadhani uendelee kuusoma vizuri huo mradi wa wazungu., huenda ukapata kuuelewa vizuri. na kuhusu huyo bwana, Geodavie...biala shaka ilikuwa unamuelewa hapo zamani lakini sasa ndo umeshindwa kumuelewa baada ya hilo tamko lake.

unaweza jiuliza anahubiri nini basi? neno la nani? au na yeye ana mradi wake anao hubiri?

NB; Kama nakuona hivi miaka kadhaa ukaja kuwa mhubiri mkubwa ukihubiri na kufundisha kilicho andikwa ktk Bibilia (mradi wa wazungu). Endelea kutafakari mkuu😎😎😎
 
Tatizo lako unauangalia Ukristo kwa jicho la Uislam.
Hakuna kitu kuangalia Ukristo kwa jicho la Uislamu. Hicho kitu kwamba haliwezekani.

Tunaupima Ukristo kwa jicho uhalisia, au unataka kutuambia uhalisia haupo ?
Unataka yale wanayofanya/itikadi Waislam na Wakristu wayafuate.
Wala sijawahi kutaka hilo, sababu najua UISLAMU umekamilika na haulinganishwi na dini nyingine yoyote.

Nyinyi kama mna hoja, jibuni kwa macho yenu. Cha msingi uhalisia upo.
Unashindwa kukubali wao Wakristu Mungu wanayemuabudu siyo Mungu anayeabudiwa na Waislam. Ukikubali hilo wala hautapata shida na mambo ya Wakristu.

Hili si kweli kwa namna wanavyo muelezea Mungu katika maandiko yao, ndio yule yule ambaye sisi Waislamu tuna muabudu. Shida namna mnavyomuelezea na kumuabudu kunaenda kinyume na uhalisia.

Kwahiyo sisi hatupati tabu, bali tunawashangaa inakuwaje mnapingana na Uhalisia ?
Jiulize kwa nini hautaki kuuangali Ubudha kama unavyouangalia Ukristu? Jibu ni moja tu. Uislam uko obsessed sana na Ukristu, unajihisi haukamiliki bila Ukristu., na hilo ni tatizo lako siyo la Wakristu.
Vyote tunaviangalia kutokana na haja. Sasa Leo hii mabudha hawajitangazi au hasako wengi katika maeneo yetu kuzidi nyinyi Wakristo.

Lakini sehemu ambayo Mabudha wengi wanaongelewa sana na vitabu vimendikwa, bali hata Mimi Nina kitabu kina volume mbili, kimeelezea dini nyingi ikiwemo ubudha.
 
Hata mungu ana chanzo mkuu? Alitoka wapi?
Mungu hayupo.

Hakuna Mungu.

Waamini Mungu (Theists) wanaodai Mungu yupo, ndio wenye jukumu la kueleza na kuthibitisha chanzo cha huyo Mungu wanayedai yupo.
 
Imeandikwa katika 2 Timotheo 3:16;Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,.
 
Unataka nini majina ya watoto wa Kaini au watoto wengine wa Adam?
Watoto wengine wa Adam na Eva mbali na Kaini na Abeli. Waliitwaje na wametajwa kwenye kifungu gani cha biblia?
 
Okay, Sasa yule shetani aliyekua anapiga story na Mungu kwenye kisa cha Ayubu ni nani?

Na yule aliyefungiwa kuzimu na Yesu ni yupi?

Km viumbe vyote viliumbwa na Mungu kwahiyo Mungu anaumba vitu ambavyo anajua fika vitamsumbua??

Basi Mungu kazidiwa akili na binadamu, maana binadamu anaweza kutengeneza bomu na akajua jinsi ya kulitegua lakini Mungu anashindwa kumdhibiti shetani aliyemuumba!!!

Hii ajabu sana!! 😹😹
Mkuu umemaliza kila kitu. Hii hoja yako ipigiliwe msumari iwe bango kila mtu akaisome.
 
Mwanzo 2:21
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
Mwanzo 2:22
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
Mbona mwanaume hana mbavu pungufu? Je, ule ubavu alioung'oa Mungu ulichipua tena?
 
Mkuu tujikite kwenye hoja. Kuna mambo mengi kwenye biblia ambayo ukiyaangalia kwa uhalisia unaona kabisa kuwa hapa tunapigwa. Hebu niambie kwa mfano kama hadithi ya Nuhu ni tukio la kweli au ni hadithi. Give concrete evidences.
Nilikwambia Wewe ni kasuku Kwa hio kama unaweza nenda kasali Kwa geo davi alioshindwa kumsaidia mwanae aliekuwa na msongo WA mawazo (depression) kama Wewe.Ila Anglia usije kuishia kujichora tattoo.
 
Wenzio wasio muamini MUNGU hawana hata mda WA kuhoji vifungu/mistari ya biblia..Lakini Wewe tpaul Kwa sababu akili yako haina TOFAUTI na akili ya mbuni huna cha kufanya zaidi ya kujihusisha na dini usioijua,,usioipenda na usioiamini..Kama hujioni kwamba una tatizo la afya ya akili nakushauri ukapime minyoo uone unayo kiasi gani,,,pili ukachunguze minyoo imekula kiasi gani cha portion ya ubongo wako...Ukafanye kutulia upate recovery...Tatizo la afya ya akili ulilo nalo ni kubwa sana...
 
N
Yule ni mtumishi wa ibilisi, mafundisho yake ni utata mtupu. Kule tu kujiita nabii mkuu ni uongo mtupu hakuna nabii wa kweli wa namna ile. Nyumbu tu ndio anaowadanganya na kujaza sinagogi lake.
Nabii wa kweli ni yupi?
 
Back
Top Bottom