Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Sawa...

Amesema, kuna kipindi Roman Empire iliificha Biblia (ni kweli tena wengine waliuawa).

Swali langu kwako mleta mada ni kwanini Roma iliificha Biblia?

Unamskia anasema ukioneshwa "mistari original", reference yake ni ipi?

Nina maswali mengi ya kukuliza tafadhali uanze kunijibu hilo kwanza...
Sasa kama walificha kwa Zaidi ya Miongo kadhaa baadae wakaruhusu Una Uhakika gani kama Hawakubadili baadhi ya Aya?
 
Sasa kama walificha kwa Zaidi ya Miongo kadhaa baadae wakaruhusu Una Uhakika gani kama Hawakubadili baadhi ya Aya?
Kwa hivyo mpaka hapa inaonesha unaamini Biblia ni neno la Mungu ila huelewi ile ilofichwa na ilotolewa baada ya kufichwa ipi ni sahihi?

Au huamini tu Biblia yoyote ile huamini kuwa ni Neno la Mungu!?
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.

View attachment 3279501
MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.

Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.

Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?

Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?

Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?

Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.

Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.

Nawasilisha.

​


Ukweli ni kwamba, katika nyakati hizi, hakuna nabii wala mtume. Ukimsikia mhubiri yeyote anajiita nabii au mtume, tambue kuwa huyo ni tapeli.
 
Sawa...

Amesema, kuna kipindi Roman Empire iliificha Biblia (ni kweli tena wengine waliuawa).

Swali langu kwako mleta mada ni kwanini Roma iliificha Biblia?

Unamskia anasema ukioneshwa "mistari original", reference yake ni ipi?

Nina maswali mengi ya kukuliza tafadhali uanze kunijibu hilo kwanza...
Ndugu mkuu, ninachofahamu mimi ni kuwa Roman Empire walificha biblia ili wawatawale watu kirahisi. Na mistari original sio rahisi kupatikana kwa saabu hao washenzy walipoficha biblia kwa miaka yote hiyo 600, possibly mistari pia ilipotea.

Anyway, tusubiri wengine nao waje tusikie wanasemaje mkuu.
 
Kwa hivyo mpaka hapa inaonesha unaamini Biblia ni neno la Mungu ila huelewi ile ilofichwa na ilotolewa baada ya kufichwa ipi ni sahihi?

Au huamini tu Biblia yoyote ile huamini kuwa ni Neno la Mungu!?
Biblia Yenye Neno La Mungu Haipo Mkuu!
Ilipotezwa zaman sana..
Neno Biblia au Bible ni Neno linalomaanisha Mkusanyiko wa Vitabu..

So yes Naamini Kuna Bible ilikuwa na neno la Mungu ambayo sasa Hatuna
 
Back
Top Bottom