Hakuna kufutwa uzi , acha watu watolewe gizani hili suala Lina hoja na dalili za waziMjadala ufungwe au uzi ufutwe kama kuna upotoshaji wa neno la Mungu
😹😹😹 Mi sio Mod Ila ukicomment matusi watakushughulikia mods..!!kuna kitu nataka kucomment ila nasikia za chinichini eti we ni Mod? ni kweli 🙂
Hao mitume na manabii wanajijua wanayofanya ndio maana wanaropoka lengo Lao zaidi ni mshiko na jamaa mtaji kashaupata anatafuta maisha mengine kiaina nje ya udanganyifu wake.Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Nabii Mkuu na maarufu Afrika Mashariki na Kati, Nabii GeoDavie, kwa mara ya kwanza ameipinga biblia hadharani kama unavyoweza kumsikiliza kwenye video ifuatayo. Nabii Mkuu ametanabahisha hilo baada ya kukerwa na watu wanaomuandama kila kukicha kuwa hatumii maandiko yaliyomo kwenye biblia katika mahubiri yake. Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa mkuu.
View attachment 3279501
MAONI YANGU
Kwa muda mrefu nimekuwa siyaamini mahubiri ya Nabii GeoDavie lakini kwa hili la biblia ni kama vile namuelewa kwa mbaaali! Nasimama na Nabii kwani hata mimi kuna baadhi ya maandiko katika biblia yananipa shida kuamini kama kweli yaliandikwa na Mungu au ni maneno tu ya wanadamu.
Baadhi ya maandiko tata yaliyomo kwenye biblia na ambayo yanawashangaza wengi ni kuhusu kuumbwa kwa mwanadamu pale bustanini Eden na kisha mwanadamu akadanganywa na nyoka na kujikuta akiadhibiwa na Mungu. Adhabu ambazo mwanadamu aliadhibiwa na Mungu zinasimama hadi leo.
Kwanza, huyo nyoka aliyemdanganya Eva akala tunda la ujuzi wa mema na mabaya alitoka wapi mbona uumbaji wa nyoka haukutajwa kwenye hadithi ya uumbaji? Au kuna mpinzani wa Mungu aliyemuumba huyo nyoka ili kuharibu mipango ya Mungu?
Pili, Mungu alikuwa na malengo gani kumuumba mwanadamu mwenye akili pungufu ukilinganisha na akili za nyoka huku akijua kuwa nyoka angemdanganya kwa urahisi na kumlisha matunda kutoka mti uliokatazwa na Mungu?
Tatu, kwanini Mungu aliumba huo mti wa matunda huko Eden huku akijua kuwa matunda yale yangetumiwa na nyoka kumlisha mwanadamu aliyemuumba? Inawezekana Mungu alifanya makusudi ili mwanadamu ale matunda kisha amuadhibu adhabu ya milele?
Utata mwingine ni kuhusu kuoa kwa Cain na Abel. Adam na Hawa walifanikiwa kuzaa watoto wawili tu wa kiume, ambao ni Cain na Abel. Lakini ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 4:17, imeandikwa kwamba Cain alimjua mke wake, na akapata mimba na kumzaa Enoch. Huu mstari unazua utata kuhusu ni wapi mke wa Cain alipatikana ikichukuliwa kuwa Adam na Eva walikuwa ndio viumbe pekee waliokuwepo duniani wakati huo. Hata jina la huyo mke wa Cain halijatajwa mahali popote pale kwenye biblia.
Kwa mifano hii ya utata (contradictions), na mingine mingi iliyojaa kwenye biblia, kuna uwezekano mkubwa kuwa biblia ni mradi wa wanadamu, hasa wazungu, iliyotungwa kwa manufaa yao binafsi, hasa maslahi ya kikoloni.
Nawasilisha.
watu watolewe gizani au wanaingizwa gizani? Kuna upotoshaji, nabii wa uongo anatimiza unabii wa biblia kuwa watatokea manabii wa uongo na ye ndio miongoni mwa manabii wa uongoHakuna kufutwa uzi , acha watu watolewe gizani hili suala Lina hoja na dalili za wazi
Huyo ni Nabii wa uongo asilimia mia ila kuhusu Bible hapo kasema ukweli na kapiga kwenye mshono.watu watolewe gizani au wanaingizwa gizani? Kuna upotoshaji, nabii wa uongo anatimiza unabii wa biblia kuwa watatokea manabii wa uongo na ye ndio miongoni mwa manabii wa uongo
Nimecheka na funga yangu aliposema vitu vengine vinaeleweka wasijitoae ufahamuHuu ndiyo ukweli msiotaka kusikia wengi
hapa najua tu unashabikia kwa kuwa we ni kobazi, unadhani hata upande wenu mko sahihi?Huyo ni Nabii wa uongo asilimia mia ila kuhusu Bible hapo kasema ukweli na kapiga kwenye mshono.
Tuko sahihi 💯 fil 💯 , na hilo swala kusuhu bible liko wazi kabisa hata ukisoma historia yake utagundua kuwa Kuna mikono ya watu imefanya Yao.hapa najua tu unashabikia kwa kuwa we ni kobazi, unadhani hata upande wenu mko sahihi?
Uzi aufutwi hapa mpaka uelimikeMjadala ufungwe au uzi ufutwe kama kuna upotoshaji wa neno la Mungu
AtheistKwanini Jamiiforum hawajaweka Emoji ya Kupiga makofi kwenye Reaction 👏👏👏👏👏
Ukisona kwa utulivu falsafa za wagiriki... Socrates, Plato, Aristotle, n.k.... na ukiambiwa kwamba biblia ya kale ilikuwa katika maandishi ya kigiriki.... Huoni taabu kupinga kwamba Biblia ni neno la Mungu, ISIPOKUWA ni hekima ya binadamuAtheist wamepata hoja toka kwa nabii mkuu. Yule ni mpuuzi fulani anayejua kucheza na akili za nyumbu. Sasa akisema biblia ni maneno ya watu atuambie maneno ya Mungu ni yapi?
PRO MAXGeoDavie ni mhuni kama wahuni wengine.
Malaya kwa kiwango cha lami.
Mngese yule mtu alichukua mke wa rafiki yangu aliyekuwa miongoni mwa walinzi wake.PRO MAX
Aisee Mimi sio Atheist na Sijawahi Kuwa Atheist..Atheist
Hawa manabii wakiwabana vizuri watawaambiwa ukweli tuHayo maswali ukiwauliza wafia dini humu wanaanza kukulaani, ukweli ni kwamba upeo wao ni mdogo wanapelekwa km nyumbu..!!