Du! kiama kimekaribia ngoja niende bar nikagide za mwisho mwishoMahakama ya hakimu mkazi jijini Arusha leo imevunja rasmi ndoa ya bibi Pamela na mumewe baada ya kuthibitika pasi na shaka kuwa alikuwa na mahusiano nje ya ndoa na nabii Jodevi wa ngurumo za upako wa jijini Arusha.
Mtoto wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka 15 ndiye aliyetoa ushadihi wote ukiwemo wa nabii kufika nyumbani na kupelekewa juice kwenye gari yake yenye vioo vyeusi na kukaa humo kwa muda mrefu na mamaake pia nabii kufika nyumbani usiku baba akiwa hayupo na kuambiwa akalale huku nabii akibaki na mama sebuleni muda mrefu akifanyiwa maombi maalum
Vile vile ushahidi na msg za simu na kwenye laptop na mambo mengine mengi yamethibitisha pasi na shaka mahusiano ya wawili hao na hatimaye mahakama kuamua kuvunja ndoa hiyo takatifu
Chanzo: Wapo radio