Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!.

Paskali
Asante kwa kuleta hili hapa, binafsi huwa naogopa sana kujadili mambo yawahusuyo watumishi wa Mungu au wapakwa mafuta wa Bwana.
Tuanze na Corona...this is real na haitakiwi kufanyiwa mzaha wa kinabii. Sayansi haina unabii zaidi ya kufanya sanaa.
Pia naomba kudeclare kuwa mimi niko Mwanza ambako nabii Malisa kaanzia. Sitaki kujiingiza kuhusu ni Mungu gani anamtumikia hilo anajua yeye na Mungu wake. Naomba nijikite tu kwenye huo unabii anaouleta, nabii huonyeshwa yajayo sio yaliyopo...alitakiwa aje na unabii kabla Corona haijaanza na apewe suluhisho. Unabii gani huu hapa ni mtu anaangalia tu alama za nyakati kuwa hata ikienda sana haiwezi kulast long, lakini kusema huo ni unabii...labda Mungu wake anajua. Na kuhusu watu waliopiga simu na kupewa unabii on the spot,nikukumbushe tu miezi sio mingi South Africa mtumishi wa Mungu alimfufua mfu na matokeo yake tunayajua kwa hiyo hiyo ya watu kupiga simu is not a big deal. Japo sikatai manabii wapo but this is too cheap to be bought.
Corona is real nirudie tena,tukisikiliza hasa manabii tutaishaa...kwa nini haiendi walikolazwa wagonjwa akapige maombi ya kuzuia vifo?
Na je,kanisani kwake wamewela ndoo za maji na sanitizer? Kama wameweka ni kwa ajili ya nini wakati Mungu kamwambia hakuna kufa tena?
Watanzania tufuateni maelekezo ya watalaamu wa afya na wasemaji wenye dhamana ya kusemea gonjwa hili.
Hivi kwa hiyo airtime aliyopewa na kutizamwa na watanzania mamia kwa maelfu,akiaminiwa tutapata athari kiasi gani? Maana watu wataamini hakuna vifo na corona mwisho April,si wataachana na tahadhari zozote?
Serikali imuite na arudishwe WasafiTv akanushe kama yule anaitwa Mashimo aliedai anadawa kwa kuitangaza youtube na baadar kukanusha yeye mwenyewe...
Hii ni sanaa...watumishi wanashauri kusikiliza wataalamu huku wakimwomba Mungu kuliepusha hili balaa na si hii sanaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo anayejiita nabii malisa sio mkweli!

Mimi sijaongea nae Wala sijampa maono katika njozi.

Kuweni makini na hao manabii wa nyakati hizi huko duniani, nawapenda Sana wanadamu.
 
Kwa vile unazungumzia mungu na yesu, ni kweli hawawezi kitu, lakini ingekuwa ni Mungu na Yesu, Wanaweza kila kitu!.
P
 
Kwa vile unazungumzia mungu na yesu, ni kweli hawawezi kitu, lakini ingekuwa ni Mungu na Yesu, Wanaweza.
P
Mkuu Pascal, herufi kubwa au ndogo ni utaratibu tu wa kiuandishi ila hauhusiani kabisa na nguvu au mamlaka ya kitu. Kwamba ukiandika Mungu/Yesu hapo ndio utukufu wake na nduvu wake zinakuja ila ukiandika mungu/yesu basi umebadilisha maana?😂😂. Na je ukiandika MUNGU/YESU wanakua na mamlaka na nguvu mara 2 zaidi?

Na wewe pia umevutika kudanganyika kwenye kuhusisha mamlaka ya kitu na uandishi wa herufi. Okay, tuseme iko hivyo, je nikitamka pia itatofautisha?

Tuendelee kuomba haka kagonjwa kapite.
 
Ha
Haya maneno uliyoandika yamekwisha andikwa.
 
Najitahidi kuishi imani ambayo inanisukuma 'to do everything as if God does not exist, but in the background I know that he exists'. Hivyo, almost always namwomba Mungu anijalie kile anachoona yeye kinafaa kwangu na siyo ninachoona kinafaa na pia anijalie muda na wakati anaoona unafaa na siyo ninaoona unafaa. Haya maombi mengine na unabii wa kupiga ramli huu 'mimi simo'.
 
Namuonaga kwenye tv huyu jamaa,namuona fresh japo kuna maneno wanamnenea mabaya
Na wapo wanaomuongelea vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You can't be serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huona na yeye huyo nabii Tapeli anapotosha umma? Je yule mke na mume waliitelemshwa kwenye daladala wakapelekwa polisi na kutangazwa na Mambosasa kwa mbwembwe, ni wakati wa kuwafutia mashitaka yao na kuachiwa huru,au kwa sababu wao ni WANYONGE?
 
TB joshua mwenzake alisema march 27 hakutakua na corona, tarehe moja mwezi wa nne ilipofika visa vya maambukizi viliongezeka pamoja na kifo cha mtu mmoja

Atuambie ni may ya mwaka gani?

It's Scars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…