Pre GE2025 Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuwaombee ili waendelee kusomesha watoto wao expensive schools in kenya kama Aghakhan academy mombasa sio
 
Tuwaombee ili waendelee kusomesha watoto wao expensive schools in kenya kama Aghakhan academy mombasa sio
Tuwaombee Ili kugombana kwao kusiumize raia wasio na hatia,

Wakabidhi chama kingine Kwa Amani kabisa.
 
mkinga kawa nabii? dah. hongera zake.
 
Labda mungu na sio Mungu
Sasa Unadhani CCM inaingiza bila Mungu kuruhusu?

Sasa ni muhimu kuomba Ili kugombana kwao, kusifanyike lango la kuvuruga Amani ya nchi yetu.
 
Ukiokoka unabadilishiwa kabila, unakuwa Myahudi pure, raia wa Mbinguni, Si Mjinga tena!!
ni kweli. shida ni kama huyo nabii kaokoka au ni hawa tuliowazoea wakiuza maji, mafuta, unga na chumvi.
 
Msigwa na msaidizi wa Mdee wamechomekwa na CDM humo CCM kimkakati bila wenyewe kujijua wakipumbazwa na usanii wanaotumia kuwashambulia CDM.

CDM mnashauriwa kutowajibu wote waliotimkia CCM ila mjibidishe kitaalamu zaidi kupata taarifa zote nyeti kutoka kwa wasuka mipango na kuifanyia kazi bila kuitangaza kwenye majukwaa ya kisiasa......you will outsmart the devil out-rightly....period!!
 
Hawa waganga wa kienyeji wanojiita.manabii wanatafuta hela

Wanawatisha maCcm huku wanasikilizia wanajua maccm Wana mihela ya arabuni watawatafuta ili wawasaidie kurekebisha visivyorekebishika
 
Jambo hili halina ushahidi,

Ni tetesi tu.
 
hakuna umuhimu wowote kwa chadema kuichunguza ccm, kwasababu hakuna kitu chadema wasichokijua kwa ccm, na hata kujua kwao hakuna madhara yeyote kwa ccm. ukweli uliopo ni kwamba msigwa na yeyote anayeondoka wamechoka na umwinyi wa mbowe na soon hata Lisu ataondoka ama la, atakuwa kimyaaa harakati zote ataziacha. why? baada ya kulamba asali.
 

Ni sawa na mimi sasa hivi kusema, kesho itakuwa jumanne, tuiombee sana nchi yetu.

Hapo hakuna unabii, mwambieni huyo mtu afanye kazi za uzalishaji mali aache ujanja ujanja na kutafuta umaarufu.
mzee yahaya ndiye alifanya nikaamini na bado nasubiri moja ya tabiri zake itimie ili ujenzi wa sanamu lake ufanyike bila hiyana.
 
CCM wakifarakana itakuwa ni ahueni kwa Taifa. Hii CCM ya nyakati hizi ni shetani anayewatesa sana Watanzania.

Tuombe wafarekani bila ya kuleta madhara kwa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…