Nachukizwa na wanaomuita mwanangu Zuchu

Nachukizwa na wanaomuita mwanangu Zuchu

Habari za wakati huu waungwana..

Mitaani kumekuwa na tabia ya kuwaita watoto wa kike jina la ZUCHU, hasa kwa wale ambao majina yao yanaanzia na herufi 'Zu'

Mwanangu anaitwa Zulfa, sasa wanamuita ZUCHU kitu ambacho mimi kama mzazi sipendi kwani sio jina nililompa mwanangu.

Wakati mwingine nawaza kubadili jina na kutafuta jingine lakini siwezi kwani Zulfa ni jina ninalo lipenda.

Ujumbe wangu ni kwamba, sio vizuri kutunga na kuwapa majina watoto wa watu ambao wana majina yao halisi, hasa kuwapa majina ambayo hayana picha nzuri upande wa maudhui na maadili.


#BM
Hilo ni tatizo la majina ya kubandikwa.

Usipokaa kimya ukaanza kukemea, watunzi ndiyo wanapata upele wa kukuna na wanalipitisha kweli.

Na ukiitwa ukawa mkali wa kurusha mawe, ndiyo kabisaa hilo linakuwa ni jina lako la ubatizo.
 
Hilo ni tatizo la majina ya kubandikwa.

Usipokaa kimya ukaanza kukemea, watunzi ndiyo wanapata upele wa kukuna na wanalipitisha kweli.

Na ukiitwa ukawa mkali wa kurusha mawe, ndiyo kabisaa hilo linakuwa ni jina lako la ubatizo.
Huwa nakemea sana na wanajua sipendi, ila kwa sasa naona wameanza kunielewa maana nilikuwa mkali sana kuhusu hilo
 
Baba mke baba zuchu

hutaki m-bandike tangazo lakatazo kutoitwa zuchu
Hakuna haja ya tangazo, ila this time nikisikia mtu anamuitwa hivyo, nitamkemea kwa maneno makali mpaka akiniona tena abadilishe njia
 
Mwanao kalikubali ndio maana umelijua,anza kuzungumza na mwanao.
Au mwanao anamkubali sana zuchu mwenyewe
 
Back
Top Bottom