DOKEZO Nadai fidia kutoka Mgodi wa Barrick North Mara toka 2023 bila mafanikio, naomba msaada nipate haki yangu

DOKEZO Nadai fidia kutoka Mgodi wa Barrick North Mara toka 2023 bila mafanikio, naomba msaada nipate haki yangu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
Jun 4, 2026
Posts
3
Reaction score
9
Habari ndugu watanzania,

Naiomba serikali yangu tukufu iliangalie hili jambo ambalo mgodi wa barrick north Mara unatangaza wazi wazi kuiweka mahakama ya tanzania na serikali mfukoni kwamba najisumbua kwenye swala langu ambalo mwaka 2013 walinifanyia tathimini na 2023 nilifanya makumbaliano na kampuni kulipwa lakini naambiwa kwamba wao Mgodi wa Barrick North Mara wameiweka mahakama na serikali mfukoni na wanazo pesa za kumwaga ili nisipate haki yangu maana wana wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi mgodini sasa ni watumishi wa serikali.

Nimekuwa nikiomba mazungumzo na kampuni ya Barrick North Mara ili kumaliza suala hili nje ya mahakama lakini naishia kuambiwa niende popote, sehemu yoyote ninapojua mimi ili nipate haki yangu kulipwa billion 100, pesa ninayodai baada ya kufanya makubaliano kwenye kata na mgodi.

Pia soma Mgodi wa barrick north mara washinda tuzo kubwa za mwajiri bora 2024

Mheshimiwa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan naomba unisaidie maana wewe ndiye msaada wangu mimi na mimi ni mzee wa miaka 80 na mstaafu wa Jeshi la Wananchi.

Nimekuwa nikitumia gharama nyingi kuendesha suala hili lakini nanyimwa haki yangu wazi wazi kabisa.

Kama walikuja kwangu kuhitaji ardhi yangu nikakubali kwanini hawataki kunilipa? Swala hili limenifanyia madeni makubwa sana nahitaji msaada.

AUGUSTINO NESTORY SASI
NYAMONGO TARIME
0765426281

Mahakama ya Tanzania Tanganyika Law Society, Samia Suluhu Hassan, Ubalozi wa Canada Tanzania, na wote wapenda haki.
 
1780578857773.png
 
Back
Top Bottom