DOKEZO Nadai fidia kutoka Mgodi wa Barrick North Mara toka 2023 bila mafanikio, naomba msaada nipate haki yangu

DOKEZO Nadai fidia kutoka Mgodi wa Barrick North Mara toka 2023 bila mafanikio, naomba msaada nipate haki yangu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hadi nimetokwa jasho billion 100 hio hela ndefu sana asee usishangae ukapotezwa na hao hao unaenda kuwaomba msaada
Maswali ulifuata utaratibu wa kisheria kipindi mnakabidhiana hio ardhi?
Ardhi ikikutwa na madini ni ya serikali ukikutwa na bangi ni zako 😂
Huena kuna kigogo alikuzunguka akalipwa yeye
 
Una miaka 80 na unadai sh bilioni 100!!😇😇
Mzee kwakweli kesi ikishafika mahakamani huwezi tena kupeleka kwa wanasiasa.
Hapo ni mapambano ya kisheria tu mpaka haki ipatikane.
 
Habari ndugu watanzania,

Naiomba serikali yangu tukufu iliangalie hili jambo ambalo mgodi wa barrick north Mara unatangaza wazi wazi kuiweka mahakama ya tanzania na serikali mfukoni kwamba najisumbua kwenye swala langu ambalo mwaka2013 walinifanyia tathimini na 2023 nilifanya makumbaliano na kampuni kulipwa lakini nambiwa kwamba wao mgodi wa Barrick North Mara wameiweka mahakama na serikali mfukoni na wanazo pesa za kumwaga ili nisipate haki yangu maana wana wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi mgodini sasa niwatumishi wa serikali

Nimekuwa nikiomba mazungumzo na kampuni ya Barrick North Mara ilikumaliza suala hili nje ya mahakama lakini naishiwa kuambiwa nieende popote sehemu yoyote napojuwa mimi ili nipate haki yangu kulipwa billion 100 pesa nayo dai baada ya kufanya makubaliano kwenye kata na mgodi

Muheshimiwa rais wa tanzania mama Samia Suluhu Hassan naomba unisaidie maana wewe ndiye msaada wangu mimi na mimi ni mzee wa miaka 80 na mstaafu wa jeshi la wananchi

Nimekuwa nikitumia gharama nyingi kuendesha suala hili lakini nanyimwa haki yangu wazi wazi kabisa
Kama walikuja kwangu kuhitaji aridhi yangu nikakubali kwanini hawataki kunilipa
Swala hili limenifanyia madeni makubwa sana nahitaji msaada

AUGUSTINO NESTORY SASI NYAMONGO TARIME
0765426281

Mahakama ya Tanzania Tanganyika Law Society samia Suluhu Hassan ubalozi wa Canada Tanzania Wote wapenda haki
Millioni 1000. afu uizidishe mara mia moja Dah 😆😆
 
Wewe mzee!! Tundu lissu angekua uraiani angekutetea mahakamani buuure, kwani alishafanya kwa wengi enzi za nyuma.

Lakini wajeda wenzio ndio walisababisha aendelee kushikiliwa.
 
Mzee wa miaka 80 unahangaika na maandiko mitandaoni, mufilisi kabisa

Ofisi za Serikali zote zipo wazi kuanzia kitongoji mpaka taifa

Unashindwa kwenda Dodoma hapo wizara ya madini ili hata shutuma zako zipate uzito kuwa hata huko umebezwa?

Hayo madeni unayoyasemea yametokana na nini?
 
Mzee wa miaka 80 unahangaika na maandiko mitandaoni, mufilisi kabisa

Ofisi za Serikali zote zipo wazi kuanzia kitongoji mpaka taifa

Unashindwa kwenda Dodoma hapo wizara ya madini ili hata shutuma zako zipate uzito kuwa hata huko umebezwa?

Hayo madeni unayoyasemea yametokana na nini?
sure
 
Tena nyie watumishi wake ndio raia wanawachukia balaa. Hapo dua na sala za raia ni kwa Barrick wafanikiwe kutokukulipa ufe na maumivu kama wale raia walivyofua wakidai taifa lao kuwa huru kutoka kwa Magaidi.
 
Umenikumbusha kuna bibi mmoja wa kichina alikuwa anamadai ya bilioni 1 alikuwa anazunguka mahakamani mpaka akafariki anadai tu.

Kubali kupokea one lump sum na isiwe pesa yote.

Dai hata 5 % ya award yako.

Utakufa bila senti.
 
OMBI LA KUONANA NA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KUHUSU MADAI DHIDI YA BARRICK NORTH MARA & NORTH MARA GOLD MINE

Mheshimiwa Rais ninaomba kwa unyenyekevu nikutane na kukuelezea kibinafsi mateso yangu makubwa yanayosababishwa na Kampuni ya Barrick North Mara na North Mara Gold Mine.

Madai yangu halisi dhidi yao hayajapata ufumbuzi wa kudumu licha ya njia zingine za kutatua migogoro.

Ninakuomba Mheshimiwa unisikilize mwenyewe ili unifanyie haki na msaada wa haraka.

Ahsante.

MZEE AUGUSTINO NESTORY SASI. MSTAFU WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA
+255611586281
 
Kwa wakati huu sijui kama utapata utatuzi wa shida yako.
......... wana nguvu sana.
Sasa hivi bora upambane na maskini wenzio nafasi ya kupata haki yako inakuwa 50/100.
Nakuombea ufanikiwe mzee.
 
Back
Top Bottom