Utafunguliwa case ya madai naye atapaswa athibitishe kuwa anakudai then utapewa muda wa kulipa hilo deni mara nyingi huwa ndani ya siku 30 tangia hukumu ilipotoka. Muda ukizidi hapo ataenda mahakamani kukazia hukumu na kupewa wito wa wewe kuitwa mahakamani shauri litasikilizwa tena na kama itashindikana kulipa basi mali zako zitakamatwa kwa mamlaka ya mahakama na kuuzwa ili kulipa hilo deni.
Kwa upande wako kama wamekuachisha kazi nje ya utaratibu wa mkataba wako unavyosema nawe utawafungulia shauri la madai kudai fidia utakayoitaka wewe mwenyewe. Kama una swali jingine uliza