Nadaiwa na kampuni wameacha kufanya kazi na mimi na sina mchongo wa kupata hela ya kuwalip kwa sasa je endapo nitapelekwa mahakamani sheria inasemaje

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Kama mada inavyojieleza, nilikua nafanya kazi na kampuni flani sasa kuna hela kidogo nliitumia kwa kutegemea nitailipa kadri ninavyoendelea kufanya kazi
Sasa ghafla jamaa wakaniachisha kazi wakati bado sijamaliza lile deni na sikuwa nalipwa mshahara ni commision tu ambayo ndo nlikua naitumia kulipa deni.
Sasa jamaa wamekomaa nilipe hela yao na mimi kwa sasa sina mchongo wowote wa kuingiza hata buku 10 kwa siku

Je wakinipeleka mahakamani utaratibu ukoje kisheria namna ya kulipa hili deni??
 
Kawashtaki wewe kwanini wakufukuze kazi wakati wanakudai, utapata fidia then utawalipa hela zao!
 
Utafunguliwa case ya madai naye atapaswa athibitishe kuwa anakudai then utapewa muda wa kulipa hilo deni mara nyingi huwa ndani ya siku 30 tangia hukumu ilipotoka. Muda ukizidi hapo ataenda mahakamani kukazia hukumu na kupewa wito wa wewe kuitwa mahakamani shauri litasikilizwa tena na kama itashindikana kulipa basi mali zako zitakamatwa kwa mamlaka ya mahakama na kuuzwa ili kulipa hilo deni.
Kwa upande wako kama wamekuachisha kazi nje ya utaratibu wa mkataba wako unavyosema nawe utawafungulia shauri la madai kudai fidia utakayoitaka wewe mwenyewe. Kama una swali jingine uliza
 
  • Thanks
Reactions: 7ve

Mkuu kama sina mali yoyote ya kukamatwa inakuaje
 
Back
Top Bottom