Nadhani kumiliki iPhone ni utumwa na tunakoelekea utakuwa ni ugonjwa

we call it iPhone disease
 
Ukiona unaathirika na majivuno ya mtu mwenye iPhone ujue una tatizo la saikolojia, nowdays simu zipo Kali tena zenye rank zaidi ya iPhone mkuu
Ni kweli mkuu, mfano Huawei ni simu moja nzuri sana, angalia jana nao wamezindua simu mpya inayokunjika mara tatu, pia inatumia akili mnemba (AI), na unaweza kuipata kwa $2,800, 🙌🏽
 
Nipo na iPhone 6s na hakuna ninachokosa kwenye mawasiliano. Ukishajua michezo ya ulimwengu huu raha sana!
 
Simu yenyewe mtu unakuta anaitumia kwa asilimia 30 tu ya inavyotakiwa kutumia lkn anakomaa mpka awe nayo atakwambia security issue ilhali hana cha maana chochote ambacho ni confidential kwamba amekitunza humo

Akili za jumla zinasumbua sana ukiwa unazitumia tena hyo 16 wayauzie milioni 9 hayo mateja yao
 
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…