Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Mkuu huu uzi kabisa ujue, ungefungua ili waungwana watoe maoni yao.!!

Una kitu
Asante sana kwa ushauri Dada(nisamehe kama nimekosea). Nitazingatia maoni yako. Poleni kwa kuwachosha.
Asante sana my friend. Nilikuwa nina hofu kubwa sana, sipendi kumkwaza mtu hasa kama naweza kujiepusha kufanya hivyo.
Maisha yangu yote nafanya bidii kujiepusha kuwa chanzo cha matatizo kwa wengine, na inapotokea hata kwa bahati mbaya lazima ni take responsibility.
Naipenda amani yangu ya moyo kuliko chochote na ninailinda daima.
Sometimes sisi wanaume ni trouble makers kwenye jamii kutokana na mifumo ya kijamii ilivyotulea na kutuaminisha.

Lakini kila mtu anaweza kuyatafakari upya maisha yake kuona amekuwa sababu ya maumivu kwa wangapi na kwa nini? Na inawezekana akawajibika kuziondoa au kupunguza changamoto alizozisababisha kwa wengine at least wakapata ahueni.
Kila mtu anaweza kuwa chombo cha amani na upendo kwa wengine.

Nje ya topic.
Mwaka 2007 nilitembelea kituo cha Good Samaritan pale Arusha ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza, kituo hiki kilikuwa kule Moshono sijui kama bado maana mimi nilihamishiwa mkoa mwingine. Somo nililojifunza kutokana na maumivu niliyopata.

Niliapa kuwa nikuwa kwenye position fulani au madaraka makubwa au ushawishi kwa wenye dhamana ya kutunga sera na sheria... NITASHAURI KUWEPO NA DATABASE YA DNA ZA WATU WOTE NCHINI TANZANIA.. KILA MTOTO ANAYEZALIWA CHA KWANZA ACHUKULIWE DNA IWEKWE KWENYE DATA BASE(inakuwa secret and retricted access isipokuwa kwa sababu za kisheria na haki za makundi maalum). WATU WENGINE WOTE WANAPOJIANDIKISHA KWENYE NATIONAL ID(NIDA) IAMBATANE NI DNA.
Lengo ni maelfu au mamia ya watoto au watu wasiotambulika identity zao kupitia data base hiyo tunaweza kutambua at least ndugu zake au jamii anatotokea.

Natamani sana lifanyike hata kesho, maana wapo watoto tunawasaidia wa changamoto hiyo ya identity na kutojua origin yao.

Swali mwisho ni nani kati yetu humu ambaye anauhakika yeye wa ukoo huo anaojitambulisha?? Au kabila hilo analodhani ni origin yake?
Labda babu alidanganya, labda bibi, labda, labda, labda. Kwa hiyo sote ni ndugu hakuna aliye na ndugu kuliko mwingine maana uhakika wala ushahidi. Rafiki, jirani, workmate na yeyote mwenye kukuheshimu na kukupenda ni ndugu kuliko ndugu wanaoitwa ndugu.
Aaah nimekosea tenaa nimeandika sana dah im sorry again and again.
 
No need to say sorry dear🙏
Once again,thank you.
Wazo lako la DNA DATABASE limaweza kufanyiwa kazi wakuu wa nchi huwa wanapita huku.

Kuhusu ndugu uko sahihi kabisa na kuna mdau alisema ndugu wanatengenezwa,unaweza kukuta ningekua na hao ndugu zangu wa damu wangekua mwiba zaidi
 
Uvunguni tena?
Mara nyingi napenda kunywa nikiwa kwa bathtub nacheki movie.

Ila hata wewe kuna siri unaficha watu wasijue,mchepuko au kitimoto kwa waislam wanaokula😀
 
N
Iko tayari nikuoe tujenge familia uwe ndugu kwa ndugu zangu
 
🤣🤣🤣🤣Mateso yote hayo ya nini da padri ana visa nyie!mbona Yesu alibadili maji kuwa divai kule kana y galilaya ye anakwama wapi?
Wapendwa ni ngumu kuelewa hayo😀
Ila nishazoea mateso yangu na labda huwezi jua labda ningekua free kinywa ningekua alcoholist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…