Kutokuwa na imani katika jambo lolote , inakuwa ni imani juu yako, hivyo usipo amini uwepo wa Mungu imani yako hiyo imekuwa ni imani juu yako.
Ni kawa wasio na sheria , kutokuwa na sheria kunakuwa sheria kwao pia, Na wewe usiyekuwa na imani juu ya Mungu , imekuwa ni imani kwako.
Kwani ni nani anayejua maisha ya mtu? Kila jambo linalotokea katika maisha ya mtu huwa kuna sababu nyuma yake, iwe mateso, iwe magonjwa, iwe kifo, uwe utajiri , iwe umasikini, iwe kukosa wazazi, iwe mimba za utotoni , iwe utu wema , iwe ubaya nk.
Hakuna kitu kisicho na sababu ya uwepo wake, Sisi wanadamu tuna ukomo wa fikra, ndio maana hatuwezi kujua hata lini tutakufa au kutoweka. Hatujui hata daikika moja mbele yetu nini kitatokea.
Fikra za mwanadamu zikikosa ufumbuzi huanza kufumbua mambo yaliyo ndani ya fikra yake .
Hakuna jambo zuli kama kuishi kwa kuamini kuwa yupo aliye bora zaidi yako, kama wewe umekuwa hivyo ulivyo basi kuna mwingine aliyepo ambaye yupo zaidi yako na anauwezo wa kukusimamia wewe, awe miungu , awe malaika awe ibilisi au hayawani. Ila zaidi ya yote yupo Mwenyezi Mungu mwenye uwezo zaidi ya vyote.
Yule asiye amini Mungu ataamini miungu, ndo mana mnajitukuza nakujiita nyie ni miungu na wengine wana wasadiki watoto wao au viumbe kwa kawaida kama mbwa na paka nk.Na hilo sio jambo geni kwenu.
Ila mwanadamu yoyote anapokosa uwepo wa Mungu katika fikra zake ,yeye huyo hana taofauti na mnyama . Ndo mana watu siku izi wanafanya mambo ya ajabu kupita kiasi, wana lala na wanyama , wana lala na ndugu zao, na wengine hata na wazazi wao.
Usiende katika madhabahu yoyote kwenda kuigiza. kama huna imani nayo bora usiende, mana kila madhabahu ina msimamizi wake, na kwa hilo watu ndio wameitiwa hapo, iwe ni jema au baya, watu wapo pale.
Kwa hiyo kama huamini uwepo wa Mungu endelea kutokuamini kabisa,na kama unaamini jikite hapo kabisa,tana zaidi .Maisha ya mtu ni yake mwenyewe na wanao mzunguka.
Hakuna kitu cha bahati mbaya,na kukosa wazazi ina sababu zake pia kama nilivyo kwisha sema, ila Mungu ni mwaminifu atatuinua tukiwa waaminifu katika mioyo yetu.
Wapo wana wa upotevu ambao roho ya yule mwovu inafanya kazi ndani yao.Jiepusheni nao na wala wasiwanyakue kwa elimu zao na ujuzi wao usio na maana hata mkapotea pamoja nao,maana wao mungu wao ni dunia ,wakila wakashiba na pesa ipo mfukoni basi habari imekwisha.