Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Mungu angekua yupo na na ana upendo kuna kitu mimi nina sifa zote za kukipata ila hanipi na anapwapa wengi hawana sifa sp hayupo.
Pia mkuu kuna walokole waaminio wengi hawafuati amri kumi za Mungu ila mimi japo slamini ila kwa misi.amo yangu wakiitwa wanaoziishi nitawapiga gape waaminio wengi sana.

Nina upendo na huruma na mwepesi wa kusamehe kuliko watu wengi unaowajua.

Si imeandikwa asiyefanyw kaz na asile ila kuna waaminio wanalala na kiamkia kanisani badala ya kufanya kazi wkt mimi nafanya kaz kama punda
Katika sifa zake tukufu ni mwenye kufanya mambo kwa hekma, kumpa huyu na kumnyima yule si dalili ya kutokuwepo kwake bali dalili kubwa ya uwepo wake, hekma ni kuweka mambo mahali pake stahiki.

Basi amempa huyu kwa hekma akijua anastahiki kupewa na ndio salama yake, amemnyima huyu kwasababu akipewa ataangamia ijapokuwa sura ya ubaya, ila ndio salama yake, amemfanya huyu mweupe huyu mweusi huyu mrefu huyu mwembamba basi anafanya apendavyo yeye, hivyo anafanya yote kwa hekma anaweka mambo mahali pake, ni wangapi account zikipungua milioni 10 wanaanza kutetemeka kwa hofu, na wangapi akipata laki mbili tu halali nyumbani? wote hawa kila mmoja anapewa kwa hekma.

"Na kwamba kwa mola wako ndio ukomo wa mambo yote, na yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio, na yeye ndiye anayefisha na kuhuisha, na yeye ndiye aliyeumba pea, dume na jike, kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa, na ni juu yake yeye ufufuo wa akherah, na yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha, na hakika yeye ndiye mola
mlezi wa nyota ya shii'ra{Sirius star}, na yeye ndiye aliyewaangamiza aadi wa mwanzo....."
Qur'an 53:42-50


Hivyo kunyimwa hawa na kupewa hawa ni kwa hekma kubwa, kuna watu wangepewa umri mrefu wangetutesa sana, na kuna watu wangenyimwa afya wangeangamia, wengine wangekuwa matajiri tungekoma, kila kitu kwa hekma.
 
Katika sifa zake tukufu ni mwenye kufanya mambo kwa hekma, kumpa huyu na kumnyima yule si dalili ya kutokuwepo kwake bali dalili kubwa ya uwepo wake, hekma ni kuweka mambo mahali pake stahiki.

Basi amempa huyu kwa hekma akijua anastahiki kupewa na ndio salama yake, amemnyima huyu kwasababu akipewa ataangamia ijapokuwa sura ya ubaya, ila ndio salama yake, amemfanya huyu mweupe huyu mweusi huyu mrefu huyu mwembamba basi anafanya apendavyo yeye, hivyo anafanya yote kwa hekma anaweka mambo mahali pake, ni wangapi account zikipungua milioni 10 wanaanza kutetemeka kwa hofu, na wangapi akipata laki mbili tu halali nyumbani? wote hawa kila mmoja anapewa kwa hekma.

"Na kwamba kwa mola wako ndio ukomo wa mambo yote, na yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio, na yeye ndiye anayefisha na kuhuisha, na yeye ndiye aliyeumba pea, dume na jike, kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa, na ni juu yake yeye ufufuo wa akherah, na yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha, na hakika yeye ndiye mola
mlezi wa nyota ya shii'ra{Sirius star}, na yeye ndiye aliyewaangamiza aadi wa mwanzo....."
Qur'an 53:42-50


Hivyo kunyimwa hawa na kupewa hawa ni kwa hekma kubwa, kuna watu wangepewa umri mrefu wangetutesa sana, na kuna watu wangenyimwa afya wangeangamia, wengine wangekuwa matajiri tungekoma, kila kitu kwa hekma.
Endelea kuamini mkuu🙏🏼
Mimi bana siwezi kuamini tena labda nikae board room na Sir God mwenyewe nimuulize maswali yangu ila hayo unayonihubiria huwa nawahubiria watu kila siku kwa hiyo hayana maajabu yoyote kwangu🙏🏼
 
Nilichokiona kwenye maandishi yako ni hiki. Umepitia kwenye maisha yenye mapito magumu, na umefanikiwa.
Una ka uselfish flani ambako kwakuwa ulipitia magumu basi hata ulichokipata hutaki sharing nanukuhu, " Hutaki kuingia kwenye ndoa kwa sababu hutaki kugawana mali". Huwezi jua utakayempata, anaweza asiwaze hizo mali zako akajitosheleza mwenyewe.

Cha mwisho fungua kitu kingine ufanye nje na madhabahu ili uwe na amani maana unachokifanya hakijakupa amani maana kipo nje na u Atheist wako.

Ni ushauri tu ninaouona .
Asante kwa ushauri mkuu🙏🏼 Ila sio ubinafsi ila tu inauma siku uachwe hlf aolewe mwingine kwa nguvu ya jasho lako.Hata wewe ungekubali?
Si bora wakafurahie yatima?

Mimi nina kazi zangu siishi kwa kutegemea madhabahu ndo mana nikasema “sehemu ya kipato” .

Siwezi kushuka madhabahuni sbb nina mafundisho mazuri yanayowasaidia watu.
 
Nilitaka nijue hilo kwanza ili nikujibu kuhusiana na utendaji kazi wa MUNGU. Nikuambie Jambo.

Unaamini kwamba MUNGU hayupo ksbb kila ukimuomba kwa juhudi kubwa wewe unatamani kupata majibu hapo hapo. MUNGU hayuko hivyo. MUNGU hapendi akuvute kwake ksbb ya kile anachokutendea papo hapo ili umuamini yupo. Ingekuwa kwa kutoa majibu kwa papo kwa papo basi ni wengi wangeamini MUNGU bila shida.

Ila MUNGU ameweka mizania moyoni mwako umtafute kwa nguvu (kama hivyo unavyomuomba kwa goti na kumuimbia na kumuabudu). MUNGU anataka umuamini Kwanza pasipo kukutendea makuu ya wazi moyoni mwako (yale ya papo kwa papo). Kwa kufanya hivyo ni sawa na kukuhonga ili umuamini. MUNGU wetu sio wa upendeleo wala rushwa .
MUNGU anakujibu maombi yako saa na wakati usiotarajia. Anakujibu ulichokiomba kwa njia nyingine kabisa,tofauti na njia unayoitaka wewe mwanadamu.

Nakuja kwako sasa. Umemuomba sana MUNGU,ukatamani akujibu hapo hapo. Je huoni mafanikio uliyonayo ya kipato kikubwa chako,ya uelewa wako,ya kumuongoza mtoto wako kwa namna hiyo. Ili-hali ukiwa yatima. BADO HUWEZI KUONA NGUVU YA MUNGU KWAKO? BADO HUWEZI KUONA MUNGU ANAVYOKUSIMAMIA KWA MAMBO YAKO MENGI YAFANIKIWE?. HUWEZI KUONA HIYO NI MIUJIZA YA MUNGU?

Anaeufanya moyo wako uwe mgumu ni nguvu ya shetani. Inajaribu kukupoteza usiamini ktk MUNGU.

Mwisho ni wewe mwenyewe kuona uyatima wako,kutengwa kwako,kunyanyaswa kwako. LAKINI KATIKA HAYO YOTE MUNGU AMEKUPA NGUVU,AMEKUPA MAFANIKIO HAYO YAKO KATIKATI YA MAADUI ZAKO. KATIKATI YA MATESO YAKO. MUNGU HAJAWAHI KUKUACHA NA HAWEZI KUKUACHA MILELE.

MAFANIKIO YOTE ULIYONAYO SI KWA UJANJA WAKO,WALA UWEZO WAKO BINAFSI,WALA AKILI ZAKO. AMINI MUNGU AMEKUONA UYATIMA WAKO ANAKUFUTA MACHOZI YAKO KWA KUKUPA MAFANIKIO HAYO.
Asante mkuu kwa kunihubiria kwa upendo mkuu🙏🏼 .Tatizo ukifikia level ya kujua Mungu hayupo ni ngumu sana kishawishika tena kuwa yupo.
 
Kama watu wanabarikiwa na kupona kupitia nyimbo zako na mafundisho yako siyo ishu ya saikolojia ni ishu ya faith, ujue Mungu yupo kupitia Imani kama unaamini Mungu yupo basi atakuwepo kama hauamini ni kweli Mungu hayupo, imarisha Imani yako, then hongera Kwa kuwa mama Bora . Nicheki kupitia dexondek@gmail.com au PM, we share some character
Asante mkuu🙏🏼 Ila fahamu kuwa wachungaji kinachowabeba ni kucheza na saikolojia na hiyo ndio inayoletq “miujiza”
 
Habari wapendwa.

Leo naanza kwa kumshukuru Maxence Melo kwa kuanzisha hii platform ambayo leo nitaitumia kusema kitu ambacho nikikisema ktk maisha yangu halisi nitaonekana wa ajabu na nina hakika kuna wapendwa wangu watanitenga hivyo nitawaambia nyie japo najua mtanipopoa sana leo ila nataka nione nitajisikiaje baada ya kusema coz nimekua natamani sana nipate mtu wa kumwambia.

Kwa nitakayoyaorodhesha hapa chini nadhani mimi nitakua ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote hapa Jamii forums🙈🙈.

MIMI NI SINGLE MAZA wa one smart little boy mwenye ndoto za kuwa Astronaut na mchungaji.Katika vitu nimefaulu kwa max nyingi maishani ni malezi bora ninayompatia huyu mtoto.Nimefanikiwa kumfanya ashike namba 1 miaka yote shuleni.Nimefanikiwa kumfundisha maadili kiasi kwamba amekua mtoto anayetolewa mfano na kupendwa na majirani na kila anayekua nae karibu.Kikubwa nimefanikiwa kumfanya aupende na kujivua uanamme wake kiasi kwamba anasema ikitokea achague kufa au kuishi kama msichana atachagua kufa.👍👍.Mwanangu ni kembamba karefu ila ukikaona kanavyotembea kibabe huku kametanua mikono utasema baunsa😂na nimefanikiwa kumfanya aamini style nzuri ya nywele ni ya kipolisi tu na kuchukia tule tu jeans twenu twa kubana.Mwanangu pigo zake ni suruali za kisabato na hata kwa risasi humvalishi hivyo vimodel.Ikitokea vaseline yake imeisha yuko tayari kupaka mafuta ya kula kuliko kupaka lotion yangu.

Najivunia kuweza kumudu ada ya over 10M ili mwanangu apate elimu ktk mazingira bora na salama na yatakayompa connection hapo badae.Najivunia kuweza kumpa maisha mazuri na exposure ambazo watoto wengi hawawezi kupewa na baba zao.He can drive and ride(nyumbani tu),anapika vitu simple,ni marufuku dada kumfulia au kumsafishia chumba chake ,he can paint,he can put tiles na vitu vingi vya ufundi hadi kunyoosha koplo at only 12..

Najivunia kufanya ampende baba yake kwa kumwambia story nzuri kuhusu babake na hilo limefanya wawe karibu na yeye kufaidi malezi ya baba na mama.

Najivunia baba watoto wangu anavyonisifia kwa mtoto kuwa “your mum is a darling queen” hadi mtoto huwa anauliza(ga) sasa mbona hatuishi kama one big family na huwa anaambiwa muulize mama yako na hii ni kwa sbb mimi ndio niliyeomba tutengane tukiwa bado tunapendana ili nipambanie ndoto zangu na sijutii hilo coz nikifa leo mwanangu atakua miongoni mwa mabilionea watoto hivyo pamoja na kwamba kuna siku za upweke ila SIJUTII maamuzi yangu yaliyopelekea niwe SINGLE MOTHER.💕

MIMI NI ATHEIST.🙈

Nimekua na doubt uwepo wa Mungu tokea nikiwa primary.Nimebatizwa kilutheri lkn mpaka siku napata kipaimara tayari nilishaanza kujiuliza uliza vitu.


Ninakubaliana na Kiranga na wenzie kuwa Mungu,Allah,shetani,mbinguni,akhera,uchawi,majini,Firdaus na mapepo ni hadithi tu zilizotungwa na binadamu kwa lengo lakuweka hofu ndani ya watu.

Hata hivyo mimi ni tofauti na kina Kiranga kwa sababu mimi(mnisamehe sana) ni “mtumishi wa Mungu”. Ninasimama madhabahuni kuhubiri na pia ninaimba nyimbo za injili.Nyimbo zangu ziko youtube,nina account kubwa tu Insta na wapendwa wanakiri “kubarikiwa “sana na huduma yangu na wengine wanakiri hadi kupona magonjwa kupitia nyimbo zangu au “maombi” ninayofanya ila hiyo iko kisaikolojia zaidi hakuna anayepona kimiujiza.


KWANINI MIMI NI ATHEIST ila nasimama MADHABAHUNI?


1)Sitaki mwanangu ajue mimi ni atheist sbb akifikia ule umri wa ujana wa kusumbua biblia itakua moja ya silaha zangu kumtuliza wenge.


2)Napenda kufundisha (nina ualimu ndani yangu)!hasa wanawake wenzangu ila huwa sihubiri mambo ya kufikirika ya miujiza ila kwq vile jukwaa langu ni madhabahuni inabidi nitumie bible na kutaja Yesu na kukemea mapepo na mimi ni muhubiri mzuri sana ukiniona nikiwa nahubiri jinsi “nawasha moto wa upako” na ninavyonena kwa lugha halafu uambiwe mimi ni atheist na ninakunywa wine hutaamini🙈🙈.


3)Vile vile napenda kuimba so naimba gospel kama hobby tu ila ndo hivyo siamini ninachokiimba ila naburudika.

4)Kanisa limenipa heshima.Najisikia raha zile VIP treatments ninazopata ninapoitwa sehemu kuhubiri/kuhudumu.

5)Kanisa ndio sehemu pekee nimekua na socialize toka niwe na akili.Sijui bar wala clubs wala sehemu nyingine ya starehe.Marafiki na ndugu zangu nimewapatia kanisani na ndo mana siwezi kamwe kuruhusu wajue mie ni atheist.

6)Sehemu ya kipato changu inatoka madhabahuni.(Sio unavyodhani).


MIMI NI YATIMA ila sina uhakika.

Hii na uatheist ndo vitu sitaki kabisa watu wajue.

Najihesabu kama yatima ila ukweli ni kwamba sijui kama wazazi wangu wako hai au wamekufa.Sijui majina yao,dini,kabila wala sina uhakika kama ni watanzania au la ila mama yangu kwa kigezo cha umri anaweza kuwa bado hai sbb nahisi alifanya aliyofanya sbb nahisi alipata mimba yangu akiwa mtoto na inawezekana aliificha mimba na hata kuzaa.Nashukuru hakupata wazo la kutoa mimba.


Wakati niko mdogo nilidhani mama aliyekua akinilea ndo mamangu mzazi kwa jinsi alivyonipenda kuliko hata wanae na wanae nilijua ni ndugu zangu wa kuzaliwa ila alipofariki ndo nikajua ukweli.Watoto wake wakagawanywa kwa ndugu ila mimi sasa hakuna aliyenitaka ila ndo hakuna aliyejua yule mama alinitoa wapi ili wanirudishe.

Hivyo Ikawa leo nakaa kwa huyu kesho yule akiwa hana dada wa kazi napelekwa kwake,kesho kutwa nitaadhibiwa niseme kwanini baba mwenye nyumba ananiangalia sana then nitafukuziwa kwa yule anayeaminiwa ni mkali aninyooshe eti nina tabia chafu n.k.

Kwa kifupi niliteseka sana sana sanaaaaaa ktk umri mdogo na sehemu pekee niliruhusiwa kwenda ni kanisani maana walikua walokole ukoo mzima😂.Walikua watu wa Mungu😀.

Kuna nyakati kuna vitu nilikua napitia nikafunga sana nikiomba Mungu anipumzishe navyo.Kuna siku nilitoroka usiku nikakimbilia kanisani nikapiga goti nikawa nasali huku machozi yanatiririka mashavuni hadi pakakucha,Nilisali nikimlalamikia Mungu usiku mzima bila kupumzika hadi miguu ikafa ganzi kwa kupiga goti.Nilikua namuomba Mungu kuwa ikimpendeza aidha aichukue roho yangu niende kwake nikapumzike au kama anataka niendelee kuishi basi aniondoe kwenye mateso niliyokua napitia.

Kufa sikufa ila cha moto niliendelea kukiona.Kuna siku nakumbuka niliropoka kwa mchungaji kuwa kama Mungu wetu sio kiziwi au kipofu basi hana huruma.

Wale ndugu zangu niliolelewa na mama yao wakati tuko wadogo kila tulipokutana tuliendelea kupendana ila tulipokua wakubwa na nikaanza kuwapiga gape la maendeleo wakanitenga kwa chuki kuu.

Ilifika sehemu nilifukuzwa kwenye msiba kwa madai kuwa kuna mtu wa Mungu ameoneshwa eti mimi ndio nimemtoa yule mtu kafara na kwamba wasiposimama kwenye maombi watarajie misiba zaidi.Nilikua nimetoa pesa nyingi ili mpendwa wetu azikwe kwa heshima ila nilirudishiwa zile pesa na kuombwa nikae mbali nao na niache kutumia ubini wao.

Niliheshimu hilo na nikawafuta maishani mwangu japo bado natumia ubini wao.

Kuna siku natamani na mimi niwe na shangazi,mjomba,mama mkubwa na mdogo,wapwa na mabinamu nikawatembelee na wao wanitembelee au tukutane kwenye sherehe za ndugu au niungwe group la ukoo ila ndo hata sijui ndugu zangu wa kweli wako upande gani wa dunia hii.

Mwanzoni nilikua nikipata mwanaume hata anitende vipi nakua king’ang’anizi sbb nilikua naona ndo kama baba,kaka ,mama mjomba na kila kitu so mpaka na let it go mtu anakua keshajuta kunijua😀au nipate mtu anichukulie kama ndugu yake yaani nitakavyojitoa na kumspoil na ikitokea akanitenda huwa naumia sana.

Hata hivyo kwa sasa rafiki zangu ndio ndugu zangu japo sitaki wajue kuwa sina ndugu sababu nahisi wataniona wa ajabu .Sometimes wakihadithia kuhusu ndugu zao na mimi nahidithia vya uongo 😃ila ukweli ni kuwa

ikitokea mimi na mwanangu tumekufa leo mali zangu zitakuwa chini ya kanisa katoliki zikawafae yatima.

MIMI NI KATAA NDOA🤪ila naaamini ndoa ni kitu kizuri ila kwa upande wangu nikifikiria kuanza kuchanganya mambo ya uchumi na ikitokea tumeachana nawaza itakuwaje ktk kugawana mali na vitu kama hivyo basi naona acha niwe nungayembe😀.

NB: Atakayenisaidia kudaka risasi za watakatifu na za anti-single mothers nina vocha yako😃
Rubbish
 
Kabisa mkuu🙏🏼
Kufa sikufa ila cha moto niliendelea kukiona.Kuna siku nakumbuka niliropoka kwa mchungaji kuwa kama Mungu wetu sio kiziwi au kipofu basi hana huruma.🥺🤔😭🙇🏿‍♂
u
 
Pole Sana

Ilimradi humdhuru Mtu, huibu cha Mtu, huchukui Mali ya Wengine kama Mume, n.k furahia Maisha
Nashukuru Mtibel.
Tena maisha yangu ni kama ya mtu anayeishi akizifuata amri 10 za Mungu huku nikiwashuhudia wanaoamini uwepo wa Mungu wakizivunja vunja bila hofu
 
Back
Top Bottom