Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Yaani mkuu huyu analaana ya kuzimu, ndio maana ni singo maza
Mkuu ujue si mnasemaga kila siku hapa kuwa singo maza ni laana?
Sasa singo maza anayekana uwepo wa Mungu si zaidi ya laana?
Hata hivyo asante🙏🏼 Kwa kuona sio tatizo
 
sijawahi ona singo maza mwenye akili timamu na hapa umethibitisha..... unaleta chai kumsifia mwanao huna uwezo wa kutoa malezi hayo kwa akili zako unavyojionyesha kwenye uandishi wako. singo maza wote mirembe kiongozi wao kathibitisha hapa
Singo maza ni tatizo Sana mkuu
 
Habari wapendwa.

Leo naanza kwa kumshukuru Maxence Melo kwa kuanzisha hii platform ambayo leo nitaitumia kusema kitu ambacho nikikisema ktk maisha yangu halisi nitaonekana wa ajabu na nina hakika kuna wapendwa wangu watanitenga hivyo nitawaambia nyie japo najua mtanipopoa sana leo ila nataka nione nitajisikiaje baada ya kusema coz nimekua natamani sana nipate mtu wa kumwambia.

Kwa nitakayoyaorodhesha hapa chini nadhani mimi nitakua ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote hapa Jamii forums🙈🙈.

MIMI NI SINGLE MAZA wa one smart little boy mwenye ndoto za kuwa Astronaut na mchungaji.Katika vitu nimefaulu kwa max nyingi maishani ni malezi bora ninayompatia huyu mtoto.Nimefanikiwa kumfanya ashike namba 1 miaka yote shuleni.Nimefanikiwa kumfundisha maadili kiasi kwamba amekua mtoto anayetolewa mfano na kupendwa na majirani na kila anayekua nae karibu.Kikubwa nimefanikiwa kumfanya aupende na kujivua uanamme wake kiasi kwamba anasema ikitokea achague kufa au kuishi kama msichana atachagua kufa.👍👍.Mwanangu ni kembamba karefu ila ukikaona kanavyotembea kibabe huku kametanua mikono utasema baunsa😂na nimefanikiwa kumfanya aamini style nzuri ya nywele ni ya kipolisi tu na kuchukia tule tu jeans twenu twa kubana.Mwanangu pigo zake ni suruali za kisabato na hata kwa risasi humvalishi hivyo vimodel.Ikitokea vaseline yake imeisha yuko tayari kupaka mafuta ya kula kuliko kupaka lotion yangu.

Najivunia kuweza kumudu ada ya over 10M ili mwanangu apate elimu ktk mazingira bora na salama na yatakayompa connection hapo badae.Najivunia kuweza kumpa maisha mazuri na exposure ambazo watoto wengi hawawezi kupewa na baba zao.He can drive and ride(nyumbani tu),anapika vitu simple,ni marufuku dada kumfulia au kumsafishia chumba chake ,he can paint,he can put tiles na vitu vingi vya ufundi hadi kunyoosha koplo at only 12..

Najivunia kufanya ampende baba yake kwa kumwambia story nzuri kuhusu babake na hilo limefanya wawe karibu na yeye kufaidi malezi ya baba na mama.

Najivunia baba watoto wangu anavyonisifia kwa mtoto kuwa “your mum is a darling queen” hadi mtoto huwa anauliza(ga) sasa mbona hatuishi kama one big family na huwa anaambiwa muulize mama yako na hii ni kwa sbb mimi ndio niliyeomba tutengane tukiwa bado tunapendana ili nipambanie ndoto zangu na sijutii hilo coz nikifa leo mwanangu atakua miongoni mwa mabilionea watoto hivyo pamoja na kwamba kuna siku za upweke ila SIJUTII maamuzi yangu yaliyopelekea niwe SINGLE MOTHER.💕

MIMI NI ATHEIST.🙈

Nimekua na doubt uwepo wa Mungu tokea nikiwa primary.Nimebatizwa kilutheri lkn mpaka siku napata kipaimara tayari nilishaanza kujiuliza uliza vitu.

Ninakubaliana na Kiranga na wenzie kuwa Mungu,Allah,shetani,mbinguni,akhera,uchawi,majini,Firdaus na mapepo ni hadithi tu zilizotungwa na binadamu kwa lengo lakuweka hofu ndani ya watu.

Hata hivyo mimi ni tofauti na kina Kiranga kwa sababu mimi(mnisamehe sana) ni “mtumishi wa Mungu”. Ninasimama madhabahuni kuhubiri na pia ninaimba nyimbo za injili.Nyimbo zangu ziko youtube,nina account kubwa tu Insta na wapendwa wanakiri “kubarikiwa “sana na huduma yangu na wengine wanakiri hadi kupona magonjwa kupitia nyimbo zangu au “maombi” ninayofanya ila hiyo iko kisaikolojia zaidi hakuna anayepona kimiujiza.

KWANINI MIMI NI ATHEIST ila nasimama MADHABAHUNI?

1)Sitaki mwanangu ajue mimi ni atheist sbb akifikia ule umri wa ujana wa kusumbua biblia itakua moja ya silaha zangu kumtuliza wenge.

2)Napenda kufundisha (nina ualimu ndani yangu)!hasa wanawake wenzangu ila huwa sihubiri mambo ya kufikirika ya miujiza ila kwq vile jukwaa langu ni madhabahuni inabidi nitumie bible na kutaja Yesu na kukemea mapepo na mimi ni muhubiri mzuri sana ukiniona nikiwa nahubiri jinsi “nawasha moto wa upako” na ninavyonena kwa lugha halafu uambiwe mimi ni atheist na ninakunywa wine hutaamini🙈🙈.

3)Vile vile napenda kuimba so naimba gospel kama hobby tu ila ndo hivyo siamini ninachokiimba ila naburudika.

4)Kanisa limenipa heshima.Najisikia raha zile VIP treatments ninazopata ninapoitwa sehemu kuhubiri/kuhudumu.

5)Kanisa ndio sehemu pekee nimekua na socialize toka niwe na akili.Sijui bar wala clubs wala sehemu nyingine ya starehe.Marafiki na ndugu zangu nimewapatia kanisani na ndo mana siwezi kamwe kuruhusu wajue mie ni atheist.

6)Sehemu ya kipato changu inatoka madhabahuni.(Sio unavyodhani).

MIMI NI YATIMA ila sina uhakika.

Hii na uatheist ndo vitu sitaki kabisa watu wajue.

Najihesabu kama yatima ila ukweli ni kwamba sijui kama wazazi wangu wako hai au wamekufa.Sijui majina yao,dini,kabila wala sina uhakika kama ni watanzania au la ila mama yangu kwa kigezo cha umri anaweza kuwa bado hai sbb nahisi alifanya aliyofanya sbb nahisi alipata mimba yangu akiwa mtoto na inawezekana aliificha mimba na hata kuzaa.Nashukuru hakupata wazo la kutoa mimba.

Wakati niko mdogo nilidhani mama aliyekua akinilea ndo mamangu mzazi kwa jinsi alivyonipenda kuliko hata wanae na wanae nilijua ni ndugu zangu wa kuzaliwa ila alipofariki ndo nikajua ukweli.Watoto wake wakagawanywa kwa ndugu ila mimi sasa hakuna aliyenitaka ila ndo hakuna aliyejua yule mama alinitoa wapi ili wanirudishe.

Hivyo Ikawa leo nakaa kwa huyu kesho yule akiwa hana dada wa kazi napelekwa kwake,kesho kutwa nitaadhibiwa niseme kwanini baba mwenye nyumba ananiangalia sana then nitafukuziwa kwa yule anayeaminiwa ni mkali aninyooshe eti nina tabia chafu n.k.

Kwa kifupi niliteseka sana sana sanaaaaaa ktk umri mdogo na sehemu pekee niliruhusiwa kwenda ni kanisani maana walikua walokole ukoo mzima😂.Walikua watu wa Mungu😀.

Kuna nyakati kuna vitu nilikua napitia nikafunga sana nikiomba Mungu anipumzishe navyo.Kuna siku nilitoroka usiku nikakimbilia kanisani nikapiga goti nikawa nasali huku machozi yanatiririka mashavuni hadi pakakucha,Nilisali nikimlalamikia Mungu usiku mzima bila kupumzika hadi miguu ikafa ganzi kwa kupiga goti.Nilikua namuomba Mungu kuwa ikimpendeza aidha aichukue roho yangu niende kwake nikapumzike au kama anataka niendelee kuishi basi aniondoe kwenye mateso niliyokua napitia.

Kufa sikufa ila cha moto niliendelea kukiona.Kuna siku nakumbuka niliropoka kwa mchungaji kuwa kama Mungu wetu sio kiziwi au kipofu basi hana huruma.

Wale ndugu zangu niliolelewa na mama yao wakati tuko wadogo kila tulipokutana tuliendelea kupendana ila tulipokua wakubwa na nikaanza kuwapiga gape la maendeleo wakanitenga kwa chuki kuu.

Ilifika sehemu nilifukuzwa kwenye msiba kwa madai kuwa kuna mtu wa Mungu ameoneshwa eti mimi ndio nimemtoa yule mtu kafara na kwamba wasiposimama kwenye maombi watarajie misiba zaidi.Nilikua nimetoa pesa nyingi ili mpendwa wetu azikwe kwa heshima ila nilirudishiwa zile pesa na kuombwa nikae mbali nao na niache kutumia ubini wao.

Niliheshimu hilo na nikawafuta maishani mwangu japo bado natumia ubini wao.

Kuna siku natamani na mimi niwe na shangazi,mjomba,mama mkubwa na mdogo,wapwa na mabinamu nikawatembelee na wao wanitembelee au tukutane kwenye sherehe za ndugu au niungwe group la ukoo ila ndo hata sijui ndugu zangu wa kweli wako upande gani wa dunia hii.

Mwanzoni nilikua nikipata mwanaume hata anitende vipi nakua king’ang’anizi sbb nilikua naona ndo kama baba,kaka ,mama mjomba na kila kitu so mpaka na let it go mtu anakua keshajuta kunijua😀au nipate mtu anichukulie kama ndugu yake yaani nitakavyojitoa na kumspoil na ikitokea akanitenda huwa naumia sana.

Hata hivyo kwa sasa rafiki zangu ndio ndugu zangu japo sitaki wajue kuwa sina ndugu sababu nahisi wataniona wa ajabu .Sometimes wakihadithia kuhusu ndugu zao na mimi nahidithia vya uongo 😃ila ukweli ni kuwa

ikitokea mimi na mwanangu tumekufa leo mali zangu zitakuwa chini ya kanisa katoliki zikawafae yatima.

MIMI NI KATAA NDOA🤪ila naaamini ndoa ni kitu kizuri ila kwa upande wangu nikifikiria kuanza kuchanganya mambo ya uchumi na ikitokea tumeachana nawaza itakuwaje ktk kugawana mali na vitu kama hivyo basi naona acha niwe nungayembe😀.

NB: Atakayenisaidia kudaka risasi za watakatifu na za anti-single mothers nina vocha yako😃
Huna hata akili singo maza wewe🚜🚜🚜🚜 huna tofauti na trekta
 
Nimependa umeongea bila kunukuu biblia mkuu..

Naomba bila kunukuu biblia unieleweshe ni kwa nini kama Mungu ameweza kuumba hivyo vyote ulivyovitaja ameshindwa kuumba binadamu asiye na kasoro.?
Hongera kwa yote Dada na pole kwa yoye. Yapo ya kukuonea huruma sana, yapo ya kukupongeza sana, yapo ya kukutia moyo, yapo mengi sana nimejifunza kwako. La kukuonea huruma sana lakini linatibika kiurahisi sana ni la identity.
Suala la magumu uliyopitia linagusa sana moyo na kutufunza mengi hasa juu ya makosa ambayo binadamu tunayafanya hapa duniani na kuacha alama mbaya kwa wasiohusika.

Kuhusu majaribu na mateso makubwa uliyopitia ambayo ndiyo chanzo cha kufikia maamuzi ya kutafakari juu ya uwepo wa Mungu, kwa hilo nakupa pole sana sana. Kila mtu ana namna yake ya kutafakari masahibu yanayomkuta, yupo anayeona yeye labda ndiyo chanzo, au wazazi, au ndugu, au jamii, au kanisa lake au dini yake, au mazingira, au rangi, au jinsia, umbile, elimu na hata muumba kwa wale waamini.

Namna ya kutoka kwenye hicho kifungo cha changamoto na mateso ndio huwa fumbo kwake. Hivyo hujikuta anatumia njia ambazo katika uhalisia ni wrong au zinazomuongezea shida zaidi. Miongoni mwa wale unaohisi ndio chanzo cha matatizo mara nyingi hata majawabu hutoka huko huko endapo ukijua njia sahihi na process ya kuyapata.
Lakini tunapokosa kutambua njia sahihi au tunapokosa watu sahihi wa kutuongoza katika njia sahihi wakati wa magumu hayo basi chochote cha afadhari hata kama ni risk kiasi gani tutakichagua ili kitupunguzie maumivu tunayopitia bila kujali ni kwa muda gani.

Kila binadamu anayepitia magumu sana sana akatumia njia zote anazozijua na zisimfae huingiwa na hasira sana na anaweza kufanya lolote iwe kudhuru au kujidhuru. Hatua ya kukata tamaa ni hatua ngumu sana sana kwa yeyote ambaye anapitia au amepitia situation ngumu zisizojibika kwenye maisha yake.

Watu wa nje huhukumu matokeo badala ya kutafuta chanzo cha mtu kufikia hatua ambayo jamii nzima inamshangaa na kumnyooshea kidole(kumhukumu). Wapo wengi wamepitia magumu kama yako au wanayapitia magumu muda huu na baadhi wameamua kufanya lolote na jamii inawahukumu badala ya kuwasaidia kwa upendo nasema tena upendo, upendo wa kweli unaweza kuokoa maelfu ya wanaoteseka muda huu bila kuhitaji muujiza kutoka popote, faraja ni tiba, wengi wanaihitaji haipati popote bali hukumu na kunyoshewa vidole na kuwaongezea maumivu makali.

Ushauri wangu kwa kuhusu huduma unayofanya.
-Tafuta namna uiache taratibu bila kuacha ishara yeyote kwa yeyote kuwa unaacha au kupunguza hizo huduma kwa sababu ya kutoamini. Sababu ni kuwa dhamiri ipo kwa kila mwanadamu anayeamini na asiyeamini hivyo kuendelea kufanya jambo ambalo moyoni mwako unajua unarubuni au kulaghai halitakupa furaha wala amani ya kweli moyoni(peace of mind).
Kisha taratibu jikite kwenye yale unayoyapenda na yanayokupa furaha na amani bila kuwa na deni la nafsi na mtu yeyote.

2..La pili kubwa kuliko yote.
Haijalishi kupitia hili jukwaa umetoa ya moyoni na umepata wa kukuunga mkono, faraja na kukutia moyo but never never ever try this in real world.

NARUDIA MY BELOVED SISTER. USIJARIBU USIJARIBU USIJARIBU KWENDA KWENYE ULIMWENGU HALISI YAANI UKATOKA HADHARANI KWA UWAZI UKASEMA WEWE NI ATHEIST MY FRIEND MY FRIEND ISHIA HUKU HUKU MAFICHONI.

NAKUHAKIKISHIA UKITOKA HADHARANI UKATHUBUTU KUTAMKA HAYO NAKWAMBIA AT THE END UTA COMMIT SUICIDE(UTAKUTA KUJIUA).
Nasema haya kwa kuzingatia background yako, na kazi unayoifanya sasa. Utajuta kwa nini ulitamka hayo trust me my sister.
Dunia haina huruma, itakutafuna hadi nywele.

Wote walio upande wako nyakati hizi watageuka kuwa chui na fisi hatari mno. Nchi yetu bado haitafikia hatua ya ukomavu wa kuheshimu maamuzi na personl feelings za mtu.
Tanzania bado sana na sheria zetu ni dhaifu mno.

Watu wapo tayari kuzitetea dini na imani zao hata ikibidi kufa au kuua hata kama kwenye maisha ya kawaida hawazifuati hata kidogo wala kutii mafundisho ya imani hizo.

Kama kweli uliyosema kuwa wewe ni Gospel Singer na Unahubiri na unafahamika na upo mitandaoni aisee my friend never try this at home..
UTAANDAMWA UTAANDAMWA UTAANDAMWA, UTATUKANWA, UTALAANIWA, UTAITWA TAPELI, MWIZI, FREEMASON, PICHA NA VIDEO ZAKO ZITASAMBAA NCHI NZIMA NDANI YA MASAA MACHACHE.
RADIO ZITAKUFANYA WEWE NDIYO TOPIC, TELEVISHENI ZA KAWAIDA NA YOUTUBE, INSTAGRAM, TIKTOK MITANDAONI HASA HUMU JAMII FORU. UTAGEUKWA NA KUTUKANWA..
ZITAANZISHWA THREAD ZA KILA NAMNA KWA KUTUMIA JINA LAKO.

MWISHO MAAMUZI NI YAKO.

ILA ngoja nikukere kidogo.
Yaani baada kukusoma weee hoja zako na majibu ya nimegundua
WEWE SIO ATHEIST HATA KIDOGO YAANI HATA ASILIMIA 0.5 HUJAFIKA INGAWA UNAJITUTUMUA KWA VIMANENO NA VIHOJA YAANI WEWE BADO SANA SANA SANA.

Changamoto yako ni ndogo kuliko ukubwa unaoipatia. INAONEKANA UMEKOSA TUU MAJIBU YA MASWALI AMBAYO KWAKO UNAYAITA MAGUMU AISEE NGOJA NICHEKE TUU.
PILI UMEPITIA STAGE YA HASIRA BAADA YA KUTOJIBIWA ULIYOTARAJIA.

NIKISEMA NIANDIKE NIYOPITIA MIMI HUMU AISEE WE YA KWAKO MMH NI NURSERY TUU. JUA KUNA MAELFU WAPO KAMA WEWE NA MPAKA LEO HAWANA PA KUSHIKA, HANA MIA, HANA NYUMBA WALA MAKAZI, ANAUMWA, ANANYANYASWA, WENGINE MPAKA JELA HALAFU WEWE SIJUI UMEPAMBANA AU UMEFANYAJE MPAKA UKAFANIKIWA KUFIKA HAPO.... LAKINI UNAHASIRA TO UNKNOWN POWER.
RELAX MY FRIEND FANYA LINALOKUPA AMANI MAANA YA KESHO HUYAJUI. LEO UNAWEZA UKASHUHUDIA KWA VIAPO HADHARANI KUWA HIKI KIPO AU HAKIPO THEN BAADA YA MIAKA KADHAA UKAKUTANA NA YATAKAYOKUFANYA UANZE KUTAFAKARI UPYA TENA,

MAISHA NI SAFARI HAKUNA AUJUAYE MWISHO WAKE NI LINI NA NAMNA GANI NA KWANINI. MAMBO YASIYOJULIKANA TUYAACHE HIVYO HIVYO MPAKA SAA YETU YA MWISHO.

POLE KWA MAELEZO MENGI YASIYO NA MSINGI. NAKUHESHIMU NA KUKUBALI SANA. UME NI ADMIRE MENGI YA KUJIFUNZA. ASANTE SANA.

WITO WANGU KWAKO SOMA SANA SOMA SANA DUNIA NI ZAIDI YA UIJUAVYO. USIJIFUNGIE KWENYE BIBLE TU, SOMA SOMA SOMA.

ALWAYS JIULIZE HILI SWALI (NANI ANATAWALA DUNIA?? NA KWA NINI AITAWALE?? NGUVU KAZITOA WAPI??)
soma na kujua watu wanaoitawala dunia ni kina nani na kwanini? Ili wapate nini, mwisho wao ni nini? Na kwa nini wanafanya kila aina ya uovu kufanikisha nia yao?? Kuna nini nyuma yake.
Astronaut👨‍🚀 wanatumwa kutafuta nini huko juu, na kila wachokitafiti au majibu wanayoyapa who is the consumer na kwa nini??
👽 wapo au hawapo, kwa nini wapo au kwa nini hawapo scientifically.
Why all rulers are believers of either dark or light, black or white.
And why most of them are black believers and even those from white origin became black kwa hiari au kwa lazima.
 
He,huu nao ni uzi kamili japo sijasoma.
 
Back
Top Bottom