Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Ndio destiny yako ....ila ? Mie sio mdini Yesu Hana dini ukijua Hilo badilika katika mtazamo wako kuhusu Mungu . Wewe hujawah ona malaika au mashetan ila mie nawaona
 
Habari wapendwa.

Leo naanza kwa kumshukuru Maxence Melo kwa kuanzisha hii platform ambayo leo nitaitumia kusema kitu ambacho nikikisema ktk maisha yangu halisi nitaonekana wa ajabu na nina hakika kuna wapendwa wangu watanitenga hivyo nitawaambia nyie japo najua mtanipopoa sana leo ila nataka nione nitajisikiaje baada ya kusema coz nimekua natamani sana nipate mtu wa kumwambia.

Kwa nitakayoyaorodhesha hapa chini nadhani mimi nitakua ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote hapa Jamii forums🙈🙈.

MIMI NI SINGLE MAZA wa one smart little boy mwenye ndoto za kuwa Astronaut na mchungaji.Katika vitu nimefaulu kwa max nyingi maishani ni malezi bora ninayompatia huyu mtoto.Nimefanikiwa kumfanya ashike namba 1 miaka yote shuleni.Nimefanikiwa kumfundisha maadili kiasi kwamba amekua mtoto anayetolewa mfano na kupendwa na majirani na kila anayekua nae karibu.Kikubwa nimefanikiwa kumfanya aupende na kujivunia uanamme wake kiasi kwamba anasema ikitokea achague kufa au kuishi kama msichana atachagua kufa.👍👍.Mwanangu ni kembamba karefu ila ukikaona kanavyotembea kibabe huku kametanua mikono utasema baunsa😂na nimefanikiwa kumfanya aamini style nzuri ya nywele ni ya kipolisi tu na kuchukia tule tu jeans twenu twa kubana.Mwanangu pigo zake ni suruali za kisabato na hata kwa risasi humvalishi hivyo vimodel.Ikitokea vaseline yake imeisha yuko tayari kupaka mafuta ya kula kuliko kupaka lotion yangu.

Najivunia kuweza kumudu ada ya over 10M ili mwanangu apate elimu ktk mazingira bora na salama na yatakayompa connection hapo badae.Najivunia kuweza kumpa maisha mazuri na exposure ambazo watoto wengi hawawezi kupewa na baba zao.He can drive and ride(nyumbani tu),anapika vitu simple,ni marufuku dada kumfulia au kumsafishia chumba chake ,he can paint,he can put tiles na vitu vingi vya ufundi hadi kunyoosha koplo at only 12..

Najivunia kufanya ampende baba yake kwa kumwambia story nzuri kuhusu babake na hilo limefanya wawe karibu na yeye kufaidi malezi ya baba na mama.

Najivunia baba watoto wangu anavyonisifia kwa mtoto kuwa “your mum is a darling queen” hadi mtoto huwa anauliza(ga) sasa mbona hatuishi kama one big family na huwa anaambiwa muulize mama yako na hii ni kwa sbb mimi ndio niliyeomba tutengane tukiwa bado tunapendana ili nipambanie ndoto zangu na sijutii hilo coz nikifa leo mwanangu atakua miongoni mwa mabilionea watoto hivyo pamoja na kwamba kuna siku za upweke ila SIJUTII maamuzi yangu yaliyopelekea niwe SINGLE MOTHER.💕

MIMI NI ATHEIST.🙈

Nimekua na doubt uwepo wa Mungu tokea nikiwa primary.Nimebatizwa kilutheri lkn mpaka siku napata kipaimara tayari nilishaanza kujiuliza uliza vitu.

Ninakubaliana na Kiranga na wenzie kuwa Mungu,Allah,shetani,mbinguni,akhera,uchawi,majini,Firdaus na mapepo ni hadithi tu zilizotungwa na binadamu kwa lengo lakuweka hofu ndani ya watu.

Hata hivyo mimi ni tofauti na kina Kiranga kwa sababu mimi(mnisamehe sana) ni “mtumishi wa Mungu”. Ninasimama madhabahuni kuhubiri na pia ninaimba nyimbo za injili.Nyimbo zangu ziko youtube,nina account kubwa tu Insta na wapendwa wanakiri “kubarikiwa “sana na huduma yangu na wengine wanakiri hadi kupona magonjwa kupitia nyimbo zangu au “maombi” ninayofanya ila hiyo iko kisaikolojia zaidi hakuna anayepona kimiujiza.

KWANINI MIMI NI ATHEIST ila nasimama MADHABAHUNI?

1)Sitaki mwanangu ajue mimi ni atheist sbb akifikia ule umri wa ujana wa kusumbua biblia itakua moja ya silaha zangu kumtuliza wenge.

2)Napenda kufundisha (nina ualimu ndani yangu)!hasa wanawake wenzangu ila huwa sihubiri mambo ya kufikirika ya miujiza ila kwq vile jukwaa langu ni madhabahuni inabidi nitumie bible na kutaja Yesu na kukemea mapepo na mimi ni muhubiri mzuri sana ukiniona nikiwa nahubiri jinsi “nawasha moto wa upako” na ninavyonena kwa lugha halafu uambiwe mimi ni atheist na ninakunywa wine hutaamini🙈🙈.

3)Vile vile napenda kuimba so naimba gospel kama hobby tu ila ndo hivyo siamini ninachokiimba ila naburudika.

4)Kanisa limenipa heshima.Najisikia raha zile VIP treatments ninazopata ninapoitwa sehemu kuhubiri/kuhudumu.

5)Kanisa ndio sehemu pekee nimekua na socialize toka niwe na akili.Sijui bar wala clubs wala sehemu nyingine ya starehe.Marafiki na ndugu zangu nimewapatia kanisani na ndo mana siwezi kamwe kuruhusu wajue mie ni atheist.

6)Sehemu ya kipato changu inatoka madhabahuni.(Sio unavyodhani).

MIMI NI YATIMA ila sina uhakika.

Hii na uatheist ndo vitu sitaki kabisa watu wajue.

Najihesabu kama yatima ila ukweli ni kwamba sijui kama wazazi wangu wako hai au wamekufa.Sijui majina yao,dini,kabila wala sina uhakika kama ni watanzania au la ila mama yangu kwa kigezo cha umri anaweza kuwa bado hai sbb nahisi alifanya aliyofanya sbb nahisi alipata mimba yangu akiwa mtoto na inawezekana aliificha mimba na hata kuzaa.Nashukuru hakupata wazo la kutoa mimba.

Wakati niko mdogo nilidhani mama aliyekua akinilea ndo mamangu mzazi kwa jinsi alivyonipenda kuliko hata wanae na wanae nilijua ni ndugu zangu wa kuzaliwa ila alipofariki ndo nikajua ukweli.Watoto wake wakagawanywa kwa ndugu ila mimi sasa hakuna aliyenitaka ila ndo hakuna aliyejua yule mama alinitoa wapi ili wanirudishe.

Hivyo Ikawa leo nakaa kwa huyu kesho yule akiwa hana dada wa kazi napelekwa kwake,kesho kutwa nitaadhibiwa niseme kwanini baba mwenye nyumba ananiangalia sana then nitafukuziwa kwa yule anayeaminiwa ni mkali aninyooshe eti nina tabia chafu n.k.

Kwa kifupi niliteseka sana sana sanaaaaaa ktk umri mdogo na sehemu pekee niliruhusiwa kwenda ni kanisani maana walikua walokole ukoo mzima😂.Walikua watu wa Mungu😀.

Kuna nyakati kuna vitu nilikua napitia nikafunga sana nikiomba Mungu anipumzishe navyo.Kuna siku nilitoroka usiku nikakimbilia kanisani nikapiga goti nikawa nasali huku machozi yanatiririka mashavuni hadi pakakucha,Nilisali nikimlalamikia Mungu usiku mzima bila kupumzika hadi miguu ikafa ganzi kwa kupiga goti.Nilikua namuomba Mungu kuwa ikimpendeza aidha aichukue roho yangu niende kwake nikapumzike au kama anataka niendelee kuishi basi aniondoe kwenye mateso niliyokua napitia.

Kufa sikufa ila cha moto niliendelea kukiona.Kuna siku nakumbuka niliropoka kwa mchungaji kuwa kama Mungu wetu sio kiziwi au kipofu basi hana huruma.

Wale ndugu zangu niliolelewa na mama yao wakati tuko wadogo kila tulipokutana tuliendelea kupendana ila tulipokua wakubwa na nikaanza kuwapiga gape la maendeleo wakanitenga kwa chuki kuu.

Ilifika sehemu nilifukuzwa kwenye msiba kwa madai kuwa kuna mtu wa Mungu ameoneshwa eti mimi ndio nimemtoa yule mtu kafara na kwamba wasiposimama kwenye maombi watarajie misiba zaidi.Nilikua nimetoa pesa nyingi ili mpendwa wetu azikwe kwa heshima ila nilirudishiwa zile pesa na kuombwa nikae mbali nao na niache kutumia ubini wao.

Niliheshimu hilo na nikawafuta maishani mwangu japo bado natumia ubini wao.

Kuna siku natamani na mimi niwe na shangazi,mjomba,mama mkubwa na mdogo,wapwa na mabinamu nikawatembelee na wao wanitembelee au tukutane kwenye sherehe za ndugu au niungwe group la ukoo ila ndo hata sijui ndugu zangu wa kweli wako upande gani wa dunia hii.

Mwanzoni nilikua nikipata mwanaume hata anitende vipi nakua king’ang’anizi sbb nilikua naona ndo kama baba,kaka ,mama mjomba na kila kitu so mpaka na let it go mtu anakua keshajuta kunijua😀au nipate mtu anichukulie kama ndugu yake yaani nitakavyojitoa na kumspoil na ikitokea akanitenda huwa naumia sana.

Hata hivyo kwa sasa rafiki zangu ndio ndugu zangu japo sitaki wajue kuwa sina ndugu sababu nahisi wataniona wa ajabu .Sometimes wakihadithia kuhusu ndugu zao na mimi nahidithia vya uongo 😃ila ukweli ni kuwa

ikitokea mimi na mwanangu tumekufa leo mali zangu zitakuwa chini ya kanisa katoliki zikawafae yatima.

MIMI NI KATAA NDOA🤪ila naaamini ndoa ni kitu kizuri ila kwa upande wangu nikifikiria kuanza kuchanganya mambo ya uchumi na ikitokea tumeachana nawaza itakuwaje ktk kugawana mali na vitu kama hivyo basi naona acha niwe nungayembe😀.

NB: Atakayenisaidia kudaka risasi za watakatifu na za anti-single mothers nina vocha yako😃
Tuanzie hapa Nungayembe! Alafu umezingua sema chama cha kataa ndoa ni kujaza ujinga vijana wadogo utandawazi ni hovyo kabisa nauchukia
 
Shusho
 
Be proudly
Unajua kitendo cha kuamua kuongea ukweli ni ujasiri wa kipekee na uwezo mkubwa sana wa kiakili.

Maoni yetu yanaweza yasikufae ssna lakini yapo baadhi utayaona yana faida unayaapply.

Kikubwa, nimeona somo kubwa kwenye ushuhuda wako. Naamini umeongea moyo wako
Kabisa mkuu🙏
Asante
 
Nimeisoma mpaka mwisho, kinachokutesa ni moyo wenye majeraha na ulioumizwa, Natamani nikupatie kitabu changu wenda kikakuganga, kumbuka mungu anakupenda sana ndio maana badala ya machozi uliokuwanayo sasa unatamba kwa maisha safi, kufa tutakufa...nani anatangulia?, ni hatima isiyofahamika.
Asante kwa kujali mkuu ila Mungu hayupo mkuu ndo mana mambo anayohusishwa nayo yanafikirisha.

Umesema ananipenda ndo mana badala ya machozi kanipa ahueni.Sasa hebu niambie wale wanaotesmezaliwa mpaka wanakufa hao anakuwq hawapendi?
 
Hongera kwa ujasiri mtoa mada. Ni hivi karibuni nimeamua kwa amani na akili zangu timamu kuwa atheist. Na mimi nimetokea kwenye mwamvuli wa Dini, na mimi nilitawazwa kuwa Mchungaji na ni mhubiri mzuri japo si maarufu. Simu yangu imejaa gospel za worship tena zile za kuugumia lakini maisha haya yamenifundisha kuwa hayupo Mungu wa kuja kuniokoa kwenye shida yangu yoyote ile. Wala sijifariji kuwa eti atalipa mabaya kwa wale walioniumiza, hayupo Mungu huyo 😂

He's too busy I guess. Nimeamua kujisifu mimi mwenyewe maana nina uungu ndani yangu. Nimeamua kuumba mwenyewe uhalisia wa maisha yangu. Kilichobaki ni Kuangalia namna ya kumsaidia mwanangu wa kiume kukua katika maadili mema awe na manufaa kwenye jamii yake. Hivyo nakuelewa.

It's a painful reality knowing kuwa hayupo huyo Mungu tunayemtegemea.
Hongera kwa kuwa na akili kiadi cha kung'amua ukweli mkuu na kuacha kuamini ujinga tuliolezewa na wakoloni hlf wao washautupilia mbali.Wana makanisa mazuri ila hayana waumini.Wako busy na vitu halisi ndo mana wako mbali kimaendeleo tofauti na sisi choka mbaya wategemea miujiza ya Mungu ambae hayupo.

Kwa upande wangu mimi kama nina Mungu basi mtoto wangu ndie Mungu wangu sbb yeye ndie ameweza tenda "muujiza" wa mimi kufanya vitu ambavyo kabla sijamzaa sikudhani ningeweza kuvifanya.
 
Natamani nikutane na ww niongee mimi pia kuna vitu vinanichanganya kwenye maisha yangu sana
 
🤣🤣🤣dada padri anakunywa chupa moja siku nne,atatuzingua huyu
Afu nilitaka niwaletee wine kutoka titanic wreck 😜😜😜 ila acha iendelee kupendezesha wine cellar coz Joannah bila kidumu cha gongo sidhani kama utapata stimu🏃😀🏃🏃
 
Ndio destiny yako ....ila ? Mie sio mdini Yesu Hana dini ukijua Hilo badilika katika mtazamo wako kuhusu Mungu . Wewe hujawah ona malaika au mashetan ila mie nawaona
Ukinisaidia na mimi niwaone mashetani au malaika nitaamini Mungu yupo na kama unaweza kunichukulia japo video inayomuonesha jini au malaika😀😀 nitakupa 5M ukale bata this week end mkuu.
NB: Usiniletee tu Nsuka wa bongo movie😀.
 
Mama samia unapenda kunikalia kooni.!!
Uzi ulishafika tamati toka page ya 10.
Kilichobaki ni kumsaidia mama mchungaji kumuwezesha apate wine kwa wakati..
Halafu week end ndio hiyooo unifanyie wepesi ile stock ya divai
 
Back
Top Bottom