Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Status
Not open for further replies.
Katika kuipa "meno" ni lazima kuwe na uweled na mipango yakinifu, unaweza kuipa meno ikawa na uwezo wakumuondoa rais (kupindua nchi) kirahisi sana.
Mkuu hiyo ndiyo moja ya kazi yao hasa Rais kama hatakuwa mzalendo kwa maana ya kulinda maslahi ya Taifa lake...... Taasisi itakuwa inamonitoring utendaji wa Viongozi kwa upande fulani........Nakubaliana nawe pia watakao kuwa kwenye Taasisi ni lazima wawe tayari kupoteza familia zao kwa ajili ya taifa na siyo kama ifanyavyo sasa kurithishana........hata kama mtu ana mambo na malengo yake kichwani........Taasisi ni lazima ipendekeze nani? awe Mkuu wa Nchi........
 
Ninakupata vema kabisa, fursa yakumuondoa kiongozi (rais) asiyewajibika hili ndilo nasisitiza liwekwe kwa umakini, kwakuwa ikiwa mkuu wa tiss tunaweza kumpata asiyemweledi na mwenye hulka binafsi za husda aweza kuitumia fursa hiyo vibaya.
 
Mengi yatasemwa kuhusu Taasisi hiyo nyeti, lakini nadhani wengi hatujui inavyofanyakazi zake unajua jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, nakumbuka kuna kipndi fulani jamaa mmoja aliposti Kitabu chake hapa JF akielezea namna ambavyo idara ya usalama wa taifa ilivyofanyakazi zake na akatahadharisha kuwa watu tusiojua namna ambavyo taasisi hiyo inafanyakazi tunaweza kufikiri kuwa imelala jambo ambalo si kweli. Binafsi nilipenda sana ile post, sijui yule jamaa yuko wapi ingefaa atuekee tena kile kitabu hapa ili tuwe angalau tunapata uwelewa badala ya kupaki tunalalama tu.

Kaka, Yerricko ametoa maoni na sio kulalama. Unayelalama ni wewe. Nathani maoni yake ni ya kujenga na sio kubomoa.

The king.
 
Idara ya usalama ya Tanzania ipo imara sana kuliko watu wanavyofikiri,

Tatizo la hapa nchini ni sheria tu inayoinyima mamlaka kamili idara hii,

Hatua hiyo inapelekea watawala/wanasiasa kupuuza ushauri mwingi unaotolewa na idara hii kama sheria inavyotaka na kujiwekea matakwa yao wanasia hawa.

Hapo umenena mkuu. Wako watanzania wanafanya kazi usiku na mchana. Siasa ndio zinaharibu hii nchi.

The king.
 
Ninakupata vema kabisa, fursa yakumuondoa kiongozi (rais) asiyewajibika hili ndilo nasisitiza liwekwe kwa umakini, kwakuwa ikiwa mkuu wa tiss tunaweza kumpata asiyemweledi na mwenye hulka binafsi za husda aweza kuitumia fursa hiyo vibaya.
Mkuu kuna wakati huwa unaongea Point sana........Kweli Baniani mbaya Kiatu chake Dawa..........get ma thanks a million.....Mura
 
Taasisi hii ambayo ndio uhai wa taifa letu imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi wataungana nami kuwa TISS ndicho chombo pekee cha nchi hii kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa hapa lilipo, Naelewa wengi watanishangaa na kuhamaki, kwanini naisifia taasisi hii ambayo wengi wapo nayo mlengo wakushoto.
Kama si uimara wa taasisi hii leo tungalikuwa tunanena kwa lugha yake kila mmoja wetu hapa nchini.

Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote kuanzialeadership,watendaji,teknolojia na sheria.

Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia,

Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,

Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"

Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.

Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,

Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi hii ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo nafikiri ihuishwe sheria hii imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii hawajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa ya kivyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kiakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi.TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Is rael,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa miakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii nikwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa tajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI yakutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate fisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi
Malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)

Malengo makuu yanatakiwa kujikita katika:

Mosi,Kuongeza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

Pili,Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis

Tatu,Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

Nne,Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

Tano,TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

Sita,Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,k iulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa ‘Corroboration codification’
Saba,kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndichokinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

Nane,Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa ‘pyramid execution’.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

Tisa,Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

Kumi,mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa, kiuchumi na machafuko ya kiroho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki TISS.

Congratulations for being so patriotic, Yericko keep it up!
 
Hapo umenena mkuu. Wako watanzania wanafanya kazi usiku na mchana. Siasa ndio zinaharibu hii nchi.
The king.

Wanasiasa ni Players wa muhimu sana katika jambo hili hapo lazima nikubali. Lakini wanapaswa kujua siyo kazi yao! Maana naona wamechukua role ya kutoa maagizo kwa TISS. Nadhani maslahi yakikaa sawa sawa watendaji katika idara hii nyeti wataondokana na vishawishi vya wanasiasa na kubaki katika core integrity.
 
Kwasisi watu wa kawaida tunaweza ona Yericho anahoja lakini kwa Fikra za upande Wa pili kile ni kitengo cha siri, utajuaje kama haya anayosema ukiondoa sheria yamefanyiwa kazi au yanafanyiwa kazi? Secondly, tulifundishwa shule ya msingi kuwa jukumu la kulinda nchi ni la wananchi wote. Je, Yericho amelinda nchi kwa Uzi huu. JF inasomwa karibia pande zote za dunia. Kwa mtazamo wangu wasiotutakia memo kwa kusoma Uzi huu wanatoka na kitu. Nadhani hii sio forum mwafaka kujadili maswala ya Usalama wa taifa.
 
Nikupe mtazamo wa taasisi za kijasusi zilivyo na miundo yake ya kiutendaji.

Today's CIA

The CIA is an independent agency responsible for providing national security intelligence to senior U.S. policymakers.

The Director of the Central Intelligence Agency (D/CIA) is nominated by the president with the advice and consent of the Senate. The D/CIA manages the operations, personnel, and budget of the CIA.

The CIA is separated into four basic components:
•the National Clandestine Service
•the Directorate of Intelligence
•the Directorate of Science & Technology
•and the Directorate of Support.

They carry out “the intelligence cycle,” the process of collecting, analyzing, and disseminating intelligence information to top U.S. government officials.

In addition, the D/CIA has several staffs that deal with public affairs, human resources, protocol, congressional affairs, legal issues, information management, and internal oversight.
 
Mndugu Mpitagwa

Nimekuongezea na hii,

An intelligence agency is a government agency responsible for the collection, analysis, and exploitation of information and intelligence in support of law enforcement, national security, defence and foreign policy objectives. Means of information gathering are both overt and covert and may include espionage, communication interception, cryptanalysis, cooperation with other institutions, and evaluation of public sources. The assembly and propagation of this information is known as intelligence analysis or intelligence assessment.

Intelligence agencies can provide the following services for their national governments.
◾Provision of analysis in areas relevant to national security;
◾give early warning of impending crises;
◾serve national and international crisis management by helping to discern the intentions of current or potential opponents;
◾inform national defence planning and military operations;
◾protect sensitive information secrets, both of their own sources and activities, and those of other state agencies;
◾may act covertly to influence the outcome of events in favour of national interests, or influence international security; and
◾Defence against the efforts of other national intelligence agencies (counter-intelligence).

There is a distinction between "security intelligence" and "foreign intelligence". Security intelligence pertains to domestic threats (e.g. terrorism, espionage). Foreign intelligence involves information collection relating to the political, or economic activities of foreign states.

Some agencies have been involved in assassination, arms trafficking, coups d'état, and the placement of misinformation (propaganda) as well as other covert operations, in order to support their own or their governments' interests.
 
Last edited by a moderator:

Mhe. Yericko, ushauri wako ni mzuri kwa ustawi wa Taifa letu. Ninapenda kukufahamisha kuwa TISS ipo imara kuliko tunavyodhani baadhi yetu. Mambo mengi unayoyaona yanatendeka au yanaendelea kutendeka, wakubwa "wenye nchi yao" ushauriwa kabla au wameishashauriwa, juu ya athari au faida zake. Ushauri kama ulivyo unaweza kupokelewa au kukataliwa na Waheshimiwa hao.....TISS ipo kazini muda wote, na wanafanya kazi nzuri sana! Kimuundo na kiutendaji, TISS inauwezo wa kunusa na kujua jambo na athari zake katika hatua za awali kabisa! Amini usiamini, ukweli ndo huo. Naomba tuwape moyo na tuwaunge mkono TISS mara zote, maana ulizi wa Taifa ni wetu sote kama raia wa nchi hii. Mungu ibariki TISS na Mungu ibariki Tanzania!
 
Hujawa mbali na mawazo yangu, lakini kusudio langu ni kudhibiti hawa "wenye nchi" wanaopewa ushauri na kutokufanyia kazi, sheria ikiwekwa sawa, hawa hawatadharau ushauri wa tiss
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom