Naenda Kanisani lakini naenda kwa Shekhe kuloga ili mambo yangu yaende sawa

Kwa hiyo tusiweke walinzi Wala kuchanja chanjo,na Wala kumuomba mtu msaada!?..au kumtegemea binaadam hapa imekaaje?
 
Naomba namba za huyo sheikh
 
We nenda kokote ilimradi unatimiza agenda zako ovu za kujiponya, maana hata hao viongozi wa hizo dini ni waovu vile vile.

Dini zote na wasimamizi wa hizi dini wote huwa na Nguvu hasi za kufanya miujiza ambayo ndiyo hiyo hiyo inayofanywa na waganga wa kienyeji, tofauf zao ni nguvu tu.

Ukishindwa kwa shekhe basi nenda kwa mchungaji, na ukishindwa kwa mchungaji basi nenda kwa mganga wa kienyeji, they are both sharing the same energies of satanic in difference names[emoji16][emoji23]
 
Wakristo wengi hapa ndipo wanapokosea na kupotea. Kama katika maisha ya kawaida huwezi kuchanganya Chumvi na Sukari na kupata ladha inayoeleweka

Iwaje kwenye maswala ya Imani.. Uchanganye giza na mwanga kutengemea mambo yako kwenda sawa??

Maandiko yanasema usiwe katikati yani vuguvugu na baridi. Amua moja.

Madhara ya hayo unayofanya.

1. Kwa sasa biashara zako zitasimama ila baada ya muda mfupi zitayumba. Kama safari hii umetoa sadaka ya elfu 10 basi awamu inayokuja utatoa sadaka ya namna tofauti. Kuku, unga.

2. Unaweka maagano kati yako,familia yako na hizo nguvu za giza. Kwa sasa unaweza usielewe ila kwenda kwa waganga ndio itakuwa njia yako. Na kamwe hutakaa upumzike na kufurahia jitihada zako
 
Huwa wanaanza hivyohivyo.Mwisho masharti ya mganga yanawashinda hadi wanakufa.Chunga sana.
 
Kama wewe ungekuwa ni Mungu ndio umekomenti hii hakika ningeogopa kumbe ni binadamu tu kama mimi, Mungu afikirii kama unavyofikiria wewe, acha niendelee kuweka mambo yangu sawa simlogi mtu lakini, naweka mambo sawa binadamu wabaya sana.
Unasema huendi kumroga mtu ila hapo hapo unasema binadamu wabaya, sasa unaenda kumroga nani au shetani?
 
Sijui nimeleweka simlogi mtu naweka mambo yangu sawa.
Hayo mambo unayotaka kuyaweka sawa umeona Mwenyezi-Mungu hayawezi. So umemtafutia back up ambaye ni Sheikh.

Kosa lako ni lile lile...la kutilia shaka uweza wa Mungu na kuwaendea waganga. Kwenye biblia hili kosa liliwaondoa wafalme kama Sauli. Alienda kwa mganga badala ya kutafuta msaada kwa Mungu.

Nakushauri baki kwa Mungu na umuamini, hao unaowaogopa wanaotaka kukutikisa hawataweza kukugusa. Unazo nguvu za kuwashinda, sema hujajua tu kuwa unazo na hujui namna ya kuzitumia.

Mjue sana Mungu, ndivyo mema yatakavyokujia.
 
Huyu hategemei mwanAdamu anategemea uchawii tuuu

Ni saw aendae hospital. Mawawa mkuu hakun bay
Hayo ndio maarfa uliyoyafut ili usingamie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…