Nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania ni ipi, Kwanini Rais wa Zanzibar awe Msaidizi wa Rais Samia?

Nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania ni ipi, Kwanini Rais wa Zanzibar awe Msaidizi wa Rais Samia?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wataalam wa Masuala ya Protokali na Katiba ya Nchi tunaomba Maelezo yenu ili tuelewe, Siku tutakuja kuambiwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake au Kizimkazi Kamwakilisha Rais Nchi Fulani.

Ikiwa Makamu wa Rais wa Tanzania yupo na ni mzima wa Afya, inakuwaje mtu asiye na cheo chochote Tanzania amwakilishe Rais wa Tanzania?

Screenshot_2024-08-30-22-35-57-1.png
 
Wataalam wa Masuala ya Protokali na Katiba ya Nchi tunaomba Maelezo yenu ili tuelewe, Siku tutakuja kuambiwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake au Kizimkazi Kamwakilisha Rais Nchi Fulani...
Kitendo hiki ni Cha Uvunjaji mkubwa zaidi wa Katiba ya nchi hii ya Tanzania.

Rais wa Zanzibar hana mamlaka ya ki-Urais ya kuweza kumwakilisha Rais wa Tanzania huko nje ya nchi kwani hana mamlaka ya kikatiba kwa upande wa Tanganyika. Aidha, Makamu wa Rais wa Tanzania anayo mamlaka ya kiutendaji u-Rais) hata kwa upande wa Zanzibar, lakini nashangaa ni kwa nini Makamu wa Rais mara nyingi sana amekuwa akienguliwa katika kupewa nafasi ya kumwakilisha Rais wa Tanzania katika ziara za kikazi huko nje ya Tanzania na badala yake nafasi yake imekuwa ikiwaklishwa na Rais wa Zanzibar, mtu ambaye mwenye Cheo kidogo ukilinganisha na cheo Cha Makamu wa Rais.

Nafikiri ndani ya Ikulu ya Rais wa Tanzania kuna tatizo kubwa Sana hususani kuhusiana na Mambo ya masuala ya Itifaki (Protocol). Kuna shuhuda nyingi sana za wazi kabisa ambazo zimedhihirisha kwamba Masuala haya ya Itifaki ndani ya Ikulu ya Rais wa Tanzania yamekuwa hayazingatiwi wala kutiliwa maanani. Mara nyingi Itifaki hii imekuwa ikivunjwa hadharani, na tatizo hili limekuwa likijirudia rudia.

Kwa kuzingatia Muundo wa Utendaji ndani ya Ikulu ya Rais wa Tanzania, Je, mtu mwenye Cheo gani hasa ndani ya Ikulu ambaye anahusika moja kwa moja na Usimamizi wa masuala ya Itifaki katika nchi hii???
 
Wataalam wa Masuala ya Protokali na Katiba ya Nchi tunaomba Maelezo yenu ili tuelewe, Siku tutakuja kuambiwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake au Kizimkazi Kamwakilisha Rais Nchi Fulani...
Unaanza kupoteza "focus" [emoji1787][emoji1787]

Rais anaweza kukutuma hata WEWE ukamwakilisha huko nje....ndio "presidential decree" hiyo...

Haya mambo ya kidiplomasia yana mengi....

Waindonesia na utamaduni wao Rais Mwinyi anaweza kuujua kwani kaishi sana " UTURUKI".....

Ningeshangaa tu kama Rais Mwinyi angemwakilisha Rais Italy na isiwe mh.Makamu wa Rais....

Hujiulizi ni kwanini kule DAVOS alikwenda Dr.Mpango badala ya Dr.Mwinyi ?!!

Kwa kuwa DAVOS kunahusisha "mabepari" na Dr.Mpango alikaa nao sana kule IMF.....

#Anyigulile Kyala[emoji7]
 
Kitendo hiki ni Cha Uvunjaji mkubwa zaidi wa Katiba ya nchi hii ya Tanzania.

Rais wa Zanzibar hana mamlaka ya ki-Urais ya kuweza kumwakilisha Rais wa Tanzania huko nje ya nchi kwani hana mamlaka ya kikatiba kwa upande wa Tanganyika...
Ulipotaja tu Tanganyika.....hoja zako zote zikawa "null and void"...

Tanganyika haipo....imeshajiozea huko kaburini...
 
Wataalam wa Masuala ya Protokali na Katiba ya Nchi tunaomba Maelezo yenu ili tuelewe, Siku tutakuja kuambiwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake au Kizimkazi Kamwakilisha Rais Nchi Fulani...
Watanzania wanahitaji sana kufundishwa katiba yao, Rais wa Tanzania ni executive president na sio ceremonial leader, amepewa mamlaka inayoitwa presidential appointment ya kumteua mtu yeyote kumsaidia au kumwakilisha popote as long as ni Mtanzania and sometimes sio lazima awe Mtanzania!. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!

Kimataifa Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania ambao Watanzania wote wa pande zote wana haki sawa za Utanzania hivyo kiuraia Wanzanzibari wote wana haki sawa za Utanzania kama wabara, hivyo wana haki ya kuteuliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi popote ndani ya JMT na Rais wa JMT yuko huru kumteua mtu yoyote kumwakilisha popote katiba jambo lolote!.

Inapotokea Rais hayupo kabisa au hawezi kutekeleza majukumu yake ya urais kwa sababu yoyote ile ikiwemo kifo, then hierarchy ya Katiba ya JMT inafuatwa
No.1 ni Rais wa JMT
No.2 ni VP
No.3 ni PM
No.4 ni Spika
No. 5 ni CJ

Lakini inapotokea Rais yupo busy, anaweza kumteua mtu yoyote kumwakilisha popote.

Pia kuna hierarchy ya ki Protokali
No. 1. Rais
No. 2 VP
No. 3 ZnZ President
No. 4 PM
No. 5. DPM
No. 6 VP 1- ZnZ
No. 7 VP 2- ZnZ
No. 8 -Spika
No. 9- CJ
No. 10- CDF

P
 
Dada yangu unaanza kupoteza "focus" [emoji1787][emoji1787]

Rais anaweza kukutuma hata WEWE ukamwakilisha huko nje....ndio "presidential decree" hiyo...

Haya mambo ya kidiplomasia yana mengi....

Waindonesia na utamaduni wao Rais Mwinyi anaweza kuujua kwani kaishi sana " UTURUKI".....

Ningeshangaa tu kama Rais Mwinyi angemwakilisha Rais Italy na isiwe mh.Makamu wa Rais....

Hujiulizi ni kwanini kule DAVOS alikwenda Dr.Mpango badala ya Dr.Mwinyi ?!!

Kwa kuwa DAVOS kunahusisha "mabepari" na Dr.Mpango alikaa nao sana kule IMF.....

#Anyigulile Kyala[emoji7]
Kwahy umesema ndugu mtoa mada ni dada yako au siyo 😎
 
Watanzania wanahitaji sana kufundishwa katiba yao, Rais wa Tanzania ni executive president na sio ceremonial leader, amepewa mamlaka ya kumteua mtu yeyote kumwakilisha popote as long as ni Mtanzania...
Uwanda wa kisheria.

Mwanasheria UMEONGEA.

Dadangu Erthyrocytes yeye kutwa kuwaza biashara na uwekezaji....ya fikra za uchumi pale katika mabanda yake ya sabasaba anatuletea ndani ya wigo wa sheria za nchi [emoji1787][emoji1787]
 
Kitendo hiki ni Cha Uvunjaji mkubwa zaidi wa Katiba ya nchi hii ya Tanzania.

Rais wa Zanzibar hana mamlaka ya ki-Urais ya kuweza kumwakilisha Rais wa Tanzania huko nje ya nchi kwani hana mamlaka ya kikatiba kwa upande wa Tanganyika. Aidha...
Hii comment yako naomba uiandalie thread yake tushushe nondo zote ..
 
Nafasi ya Makamu wa Rais ni ipi?
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, nafasi ya VP ni just only if President hayupo, kama vile ile ya March 17, lakini president akiwepo, VP hana any executive powers zozote zaidi ya kusubiria just in case rais ata nanilii!, hivyo Rais anaweza kumpangia mtu yeyote kumwakilisha popote na hajakiuka katiba!.
Tujifunze katiba ya JMT.
Mimi nimejitolea kusaidia Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
P
 
1 Je, unaelewa Nini kuhusu neno ITIFAKI kuhusiana na masuala ya utendaji kazi au uwajibikaji kwenye Ofisi za kiserikali kama hiyo Ofisi Kuu katika nchi???

2. Je, unaelewa maana na kazi za Muundo wa Utendaji katika taasisi kama hiyo taasisi ya Ikulu??
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, nafasi ya VP ni just only if President hayupo, kama vile ile ya March 17, lakini president akiwepo, VP hana any executive powers zozote zaidi ya kusubiria just in case rais ata nanilii!, hivyo Rais anaweza kumpangia mtu yeyote kumwakilisha popote na hajakiuka katiba!.
Tujifunze katiba ya JMT.
Mimi nimejitolea kusaidia Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel TT
 
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, nafasi ya VP ni just only if President hayupo, kama vile ile ya March 17, lakini president akiwepo, VP hana any executive powers zozote zaidi ya kusubiria just in case rais ata nanilii!, hivyo Rais anaweza kumpangia mtu yeyote kumwakilisha popote na hajakiuka katiba!.
Tujifunze katiba ya JMT.
Mimi nimejitolea kusaidia Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
P
Hiyo Channel uliyoichagua Wananchi wakiangalia wanaumia macho
 
Back
Top Bottom