Wanabodi,
Teuzi za Sifa na Vigezo na Teuzi Ambazo Hazina Sifa wa Vigezo.
Teuzi zote za rais, hufanyika kwa mujibu wa katiba, ila katika teuzi hizo, kuna teuzi za aina mbili, kuna teuzi zinazohitaji sifa na vigezo, na kuna teuzi ambazo hazihitaji sifa wala vigezo. Nafasi za uteuzi zinazohitaji sifa na vigezo, zimeainishwa katika katiba na sifa hizo na vigezo pia zimeainishwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, yaani prescribed kwa kumuelekeza rais atateua watu wenye sifa gani katika nafasi zipi, mfano Jaji Mkuu lazima awe mwanasheria, Mwenyekiti wa NEC lazima awe Jaji Mstaafu, CDF lazima awe ni mwanajeshi, IGP lazima awe polisi, Director wa TISS lazima awe ni "wale jamaa", Msajili wa vyama ni Jaji, CAG mtu wa mahesabu, au wakurugenzi wakuu wa taasisi za umma katika positions za utendaji, lazima wawe na sifa fulani za kielimu na kitaaluma. Baadhi ya teuzi hizi hazifanyiki at presidents pleasures bali rais huzifanya kwa kufuata maelekezo, mfano Jaji Mkuu, ni kwa maelekezo ya Tume ya Majaji, Katibu wa Bunge, tume ya Bunge, na pia zina kitu kinachoitwa " a security of tenure" kumaanisha rais anaweza kuteua tuu not at his pleasure bali kwa maelekezo na akiishamteua hawezi kumfukuza anavyojisikia, not at his pleasure bali kwa utaratibu maalum, hawa ni pamoja na Jaji Mkuu, Gavana wa BOT, CAG etc.
Paskali.